Tathmini ya Ukatili wa Kijinsia Tanzania Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuingilia Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia Tathmini ya Ukatili wa Kijinsia Tanzania : Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuingilia Ripoti No: AUS0002786 © 2017 Benki ya Dunia Anuani: 1818 H Street NW, Washington DC 20433 Simu: 202-473-1000; Barua – pepe: www.worldbank.org Baadhi ya Haki Zimehifadhiwa Kazi hii ni zao la wafanyakazi wa Benki ya Dunia. Matokeo, tafsiri, na hitimisho yanayoelezwa kwenye kazi hii si lazima yaakisi maoni ya Wakurugenzi Watendaji wa Benki ya Dunia au Serikali wanazowakilisha. Benki ya Dunia haitoi dhamana ya usahihi wa data zilizojumuishwa kwenye kazi hii. Mipaka, rangi, kiwango cha fedha, na taarifa nyingine zinazoonyeshwa kwenye ramani yoyote kwenye kazi hii haimaanishi maamuzi yoyote kwa upande wa Benki ya Dunia kuhusu hadhi ya kisheria ya nchi yoyote au kuidhinisha, au kukubali mipaka hjyo Haki na Ruhusa Maudhui kwenye kazi hii hutegemea Haki miliki. Kwa sababu Benki ya Dunia huhimiza utawanyaji wa maarifa yake, kazi hii inaweza kudurusiwa, ikiwa kamili au sehemu yake, kwa ajili ya madhumuni yasiyo ya kibiashara, ilimradi sifa kamili zinatolewa kwa kazi hii. Sifa —Tafadhali taja kazi hii kama ifuatavyo: “Benki ya Dunia. Machi 2022. Tathmini ya Jinsia Tanzania © Benki ya Dunia.” Maombi ya leseni, pamoja na haki tanzu yatumwe kwa Machapisho ya Benki ya Dunia,Taasisi za Benki ya Dunia 1818 H Street NW, Washington, DC 20433, USA; Nukushi: 202-522-2625; Barua pepe: pubrights@worldbank.org Machi 2022 3 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania Yaliyomo Shukrani 6 Vifupisho 8 Ufafanuzi wa Istilahi Kuu 10 Muhtasari Rasmi 12 1. Usuli wa Tathmini ya Ukatili wa Kijinsia 15 1.1 Madhumuni ya Tathmini 15 1.2 Mbinu ya Tathimini 15 1.2.1 Mapitio ya Dawati 15 1.2.2 Mashauriano ya Wadau 15 1.2.3 Ukomo 16 2. Jinsia na Maendeleo nchini Tanzania 17 2.1 Muktadha wa Maendeleo 17 2.2 Kukosekana Usawa wa Kijinsia 17 3. Upeo wa Tatizo la GBV 19 3.1 Data Zilizopo 19 3.1.1 Ukatili wa Kimwili na Kingono wa Wato 20 3.1.2 Ukeketaji 20 3.1.3 Ndoa za Utotoni 22 3.1.4 Ukatili wa Mwenza wa Karibu 23 3.1.5 Ukatili wa Kingono 25 3.1.6 Desturi za Kitamaduni Zinazodhuru 26 3.1.7. Tabia za Kutafuta Msaada Miongoni mwa Wahanga wa GBV 27 3.2 Makundi Ambayo Hususani yapo Kwenye Hatari ya GBV 27 3.3 GBV na KOVID-19 28 4. Mazingira ya Kisheria na Kisera ya Kushughulikia GBV 30 4.1 Mazingira ya Kutunga Sheria 30 4.1.1 Sheria Kuu 30 4.1.2 Mapungufu na Fursa Muhimu katika Kutunga Sheria 31 4.2 Mazingira ya Sera 32 4.2.1 Sera Muhimu 32 4.2.2 Mapungufu na Fursa Muhimu katika Sera 34 4 Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia 5. Taratibu za Mifumo na Uratibu wa GBV 37 5.1 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 37 5.1.1 Mifumo ya Taifa Tanzania 37 5.1.2Mifumo Midogo Tanzania 38 5.2 Taratibu na Uratibu wa Mifumo ya GBV Zanzibar 38 5.3 Mapungufu Muhimu na Fursa katika Mifumo na Uratibu 40 6. Mwitikio wa GBV na Programu za Kuzuia 41 6.1 Programu za Mwitikio 41 6.1.1 Mwitikio wa Sekta ya Afya 41 6.1.2 Mwitikio wa Sekta ya Saikolojia 42 6.1.3 Mwitikio wa Sheria/Haki 43 6.1.4 Mwitikio wa Usalama 44 6.1.5 Njia za Rufaa na Usimamizi wa Habari 44 6.2 Programu za Kuzuia GBV 45 7. Mapendekezo 47 7.1 Sheria na Sera 47 7.2 Mifumo na Uratibu 47 7.3 Mwitikio na Kuzuia 47 Kiambatisho 1: Maswali ya Kuongoza Mahojiano ya Mtoa Habari Muhimu 49 Kiambatisho 2: Watoa Habari Muhimu Waliohojiwa 50 Kiambatisho 3: Sheria za Taifa Kuhusiana na GBV 51 Kiambatisho 4: Mifumo ya Kimataifa na Kitaifa inayohusu Ahadi za Tanzania kuhusu GBV 53 Kiambatisho 5: Kanuni na Mbinu za NPA 54 Kiambatisho 6: Mifano ya Programu za Kuzuia GBV nchini Tanzania 56 Kiambatisho 7: Utendaji Bora katika Muktadha wa Kulinganisha 58 5 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania Shukrani Ripoti hii ilitayarishwa na Timu ya Pamoja ya Benki ya Dunia ya Maendeleo Endelevu na Desturi za Maendeleo ya Binadamu Duniani. Timu hiyo iliongozwa na M. Yaa Oppong, Mkuu wa Sekta, SD; Inaam Ul Haq, Mkuu wa Programu, HD, (wote wa Tanzania CMU (Country Management Unit)), na Gemma Joan Nifasha Todd, Mbobezi wa Elimu. Utafiti wa awali ulifanywa na Ruth Ndesanjo Meena, Mshauri wa Jinsia. Uandishi wa Ripoti uliongozwa na Daniel John Kirkwood, Mshauri wa Jinsia, na Laurel Elizabeth Morrison, Mshauri wa Jinsia (wote wa Africa Gender Innovation Lab). Wajumbe wafuatao wa Timu ya Msingi walichangia kwa sehemu kubwa kwa maendeleo, mapitio,na ukamilishaji wa Tathmini ya Jinsia, na kwa ujumla wanapongezwa Tanya Lynn D’Lima, Mchambuzi wa Programu; Chiho Suzuki, Mbobezi wa Afya Mwandamizi; Francisco Obreque, Mbobezi wa Kilimo Mwandamizi; Nicholas Meitaki Soikan, Mbobezi wa Afya Mwandamizi; Callie Phillips, Mbobezi wa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi; Rob Swinkels, Mbobezi wa Uchumi wa Jamii Mwandamizi; Toyoko Kodama, Mbobezi wa Ugavi wa Maji na Majitaka; Laura Campbell, Mbobezi wa Hifadhi ya Jamii; Clifton John Cortez, Mshauri; Nyambiri Nanai Kimacha, Mshauri wa Miji/DRM; Victoria Stanley, Mbobezi wa Utawala wa Ardhi Mwandamizi; Paula Lorena Gonzalez Martinez, Mshauri wa Jinsia Mshauri wa Jinsia; Elia Petro Boe, Mshauri wa Jinsia; Sibani Karki, Mshauri wa Jinsia; Aida Mwajua Sykes, Mshauri wa Jinsia na Ujumuishi Kiuchumi, Toni Joe Lebbos, Mshauri; Hilda Jacob Mwakatumbula,Mshauri; Rachel Cassidy, Mchumi, na Jacob Omondi Obongo, Mshauri wa Jinsia, Sera za Usalama. Wachambuzi wa Rika wamechangia kwa sehemu kubwa kwenye kufikia Dhana na matayarisho ya Tathmini Rika: Verena Phipps, Mbobezi wa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi; Naoko Ohno, Mbobezi wa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi; Peter Lafere, Mbobezi wa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi; na Nazaneen Ali, Mbobezi wa Utawala Bora Mwandamizi. Allison Louise Vale alihariri Ripoti hii. Judith Elimhoo Matemba, Msaidizi wa Programu, alitoa msaada wa kiutawala na uratibu wa mchakato mzima. Priscilla Simbisayi Zengeni, Msaidizi wa Programu, alitoa msaada wa kiutawala wa ziada. Ripoti hii ilitayarishwa kwa ushirikiano wa karibu na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (MoHCDGEC) chini ya uongozi wa Dk. John Jingu, Katibu Mkuu – Maendeleo ya Jamii; Bi. Mwajuma Mwagiza, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia; na Bi. Grace Mwangwa, Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Jinsia. Mashauriano ya Wadau yalifanyika na kutolewa muhtasari katika Ripoti ya ziada, na pongezi ziende kwa Watoa Habari wakuu: Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (Bara); MoHCDGEC (Zanzibar); (Jumuiya ya Wanawake wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA); Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC); Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA); Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP); Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM); Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya Watu (UNFPA); Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF); Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake (UN-Women); Taasisi ya UONGOZI; na Wanawake kwenye Sheria na Maendeleo katika Afrika. (WilDAF). Timu inashukuru msaada wa kiufundi kutoka kwa wenzetu wa UN Women, chini ya uongozi wa Hodan Addou, Mwakilishi wa Nchi, na Lucy Tesha, Mbobezi wa Programu – Tokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Wasichana (EVAWG). 6 Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia Pamoja na shukrani maalumu kwa Markus Goldstein, Mchumi Mkuu, Africa Gender Innovation Lab na Timu yake. Kazi hii ilitekelezwa kwa uangalizi kutoka kwa Helene Carlson Rex, Meneja wa Desturi, Uendelevu na Ujumuishi wa Kijamii. Mara K. Warwick, Mkurugenzi Mkazi kwa Tanzania, Malawi, Zambia na Zimbabwe; na Preeti Arora, Meneja Uendeshaji wa CMU, walitoa uongozi wa kimkakati katika kipindi chote cha matayarisho ya Ripoti hii. 7 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania Vifupisho AFNET Mtandao wa Kupambana na Ukeketaji nchini Tanzania AUC Tume ya Umoja wa Afrika CARE Ushirika wa Misaada na Faraja CEDAW Mkataba kuhusu Utokomezaji wa Aina Zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake CDF Jukwaa la Utu wa Mtoto CSO Asasi za Kiraia (AZAKi) CHRAGG Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora CIDO Azimio la Amri ya Sheria ya Kimila CSW Tume ya Hadhi ya Wanawake DRC Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DCMS Mfumo wa Wilaya wa Usimamizi wa Mashauri DV Ukatili wa Nyumbani EC Udhibiti kiuchumi FBOs Mashirika ya Dini FGM Ukeketaji FYDP Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano GBV Ukatili wa Kijinsia GII Kielekezi cha Kutokuwepo kwa Usawa wa Kijinsia HTP Desturi Mbaya za Kienyeji HBS Utafiti wa Bajeti ya Kaya HDI Kielekezi cha Maendeleo ya Binadamu HDR Ripoti ya Kielekezi cha Maendeleo ya Binadamu IPV Ukatili wa Mwenza wa Karibu KII Mahojiano ya Watoa Habari Muhimu LHRC Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LMA Sheria ya Ndoa MoALF Wizara ya Kilimo, Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi MoCLA Wizara ya Katiba na Sheria MoEST Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia MoFP Wizara ya Fedha na Mipango MOHSW Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii MoHCDGEC Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto MoHA Wizara ya Mambo ya Ndani MoITI Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji MoLEYWC Wizara ya Kazi, Kuwezeshwa, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto MTAKUWWA Kamati za Kitaifa za Kulinda Wanawake na Watoto (Kamati za MTAKUWWA) NGO Shirika Lisilo la Kiserikali 8 Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia NPSC Kamati Elekezi ya Taifa ya Ulinzi NPTC Kamati ya Taifa ya Ufundi ya Ulinzi NC-VAWC Kamati ya Taifa kuhusu Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto NPA-VAWC Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto NBS Ofisi ya Taifa ya Takwimu NELICO Shirika la Mwanga Mpya kwa Watoto OHCHR Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu OSC Kituo Kimoja cha Huduma PO-RALG Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa PCCB Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa PMO Ofisi ya Waziri Mkuu RITA Wakala wa Usajili, Kufilisi and Uthamini SDG Malengo ya Maendeleo Endelevu SEA Utumwa wa kingono na matumizi mabaya SH Unyanyasaji wa Kingono SHIVYAWATA Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania SOSPA Sheria ya Makosa ya Kingono TASAF Mfuko wa Ustawi wa Jamii TPF Jeshi la Polisi Tanzania TFF Tackle Africa na Shirikisho la Mpira Tanzania TACAIDS Tume ya Kupambana na Ukimwi Tanzania TDHS-MIS Utafiti wa Demografia Tanzania na Afya kwa Tanzania na Utafiti wa Viashiria vya Malaria TWG Vikundi Kazi vya Maendeleo TAWLA Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania TFNC Kituo cha Chakula na Lishe Tanzania UNFPA Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya Watu UN Women Shirika la Umoja wa Mataifa ya Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake URT Jamhuri ya Muungano wa Tanzania VAC Ukatili Dhidi ya Watoto VAW, Ukatili dhidi ya Wanawake VAWC Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto WB Benki ya Dunia WiLDAF Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika WHO Shirika la Afya Duniani ZAFELA Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar 9 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania Faharasa ya Istilahi Muhimu Jinsia: Inamaanisha sifa na fursa za kijamii ambazo zlnaambatana na kuwa mwanaume au mwanamke na mahusiano baina ya wanawaKe na wanaume , na wasichana na wavulana, pia na mahusiano baina ya wanawake na yale baina ya wanaume. Sifa hizi, fursa, na mahusiano hujengwa kijamii na hufunzwa kupitia michakato ya kijamii. Na ni mahususi kimuktadha na muda, na huweza kubadilika. Jinsia huamua nini kinachotarajiwa, kuruhusiwa, na kuthaminiwa kwenye mwanamke au mwanaume katika muktadha husika. Katika jamii nyingi kuna tofauti na kukosekana usawa baina ya wanawake na wanaume katika majukumu wanayopewa, shughuli wanazofanya, kupata na kudhibiti rasilimali, pia na fursa ya kufanya maamuzi. Jinsia ni sehemu ya muktadha mpana wa kijamii na kitamaduni.1 Istilahi hii pia hutumika kwa upana zaidi kumaanisha uwanda wa utambulisho ambao hauendani na fikra zilizo zoeleka za mwanaume na mwanamke. Ukatili wa Kijinsia: GUkatili wa Kijinsia (GBV) ni Istilahi mwavuli kwa kitendo chochote kinachodhuru ambacho kinafanywa dhidi ya matakwa ya mtu na ambacho kinasababishwa na tofauti za kijamii (kwa maana ya jinsia) baina ya wanaume na wanawake. Unajumuisha vitendo ambavyo vinasababisha madhara ya kimwili, kingono, au kiakili au mateso, vitisho vya vitendo hivyo, kulazimisha kwa nguvu, na vitendo vingine vya kunyima uhuru. Vitendo hivi vinaweza kutokea hadharani au kwa faragha. Istilahi ya ‘GBV’ hutumika mara nyingi kusisitiza jiinsi mfumo wa kukosa usawa baina ya wanaune na wanawake – ambao upo katika katika kila jamii duniani – hufanya kazi kama sifa ya kuunganisha na ya msingi ya aina nyingi za ukatili unaotekelezwa dhidi ya wanawake na wasichana. Azimio la Umoja wa Mataifa la Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake (DEVAW) linafafanua Ukatili dhidi ya wanawake kama ni “kitendo chochote cha ukatili wa kijinsia ambacho kinasababisha, au kinaweza kusababisha madhara ya kimwili, kingono au kisaikolojia au mateso kwa wanawake.” Azimio la DEVAW linasisitiza kwamba ukatili ni “dalili za kihistoria za mahusiano ya nguvu yasiyo sawa baina ya wanaume na wanawake, ambazo zimepelekea kutawaliwa na ubaguzi dhidi ya wanawake unaofanywa na wanaume unaozuia maendeleo kamili ya wanawake.” Ubaguzi wa kijinsia sio tu sababu ya aina nyingi za ukatili dhidi ya wanawake na wasichana, bali pia huchangia kukubalika kwenye maeneo mengi na ubabe wa vitendo hivi – kiasi kwamba watekeiezaji hawawajibishwi, na wahanga wanakatishwa tamaa kupaza sauti na kupata msaada.2 Desturi za Kitamaduni zenye Madhara: Hizi ni desturi za kimila, kijamii, na kitamaduni ambazo zinaweza kuleta madhara kwa afya ya kiakili au kimwili ya mtu. Mifano inajumuisha ukeketaji/ kutahiri, ndoa za utotoni, ukunga wa jadi , kurithi mke, kuogopa kunenepa, kuchanjwa chale, kuua vichanga vya kike, bei ya mahari, kupungwa mashetani, au uchawi. Ukatili wa Mwenza wa Karibu: Ukatili wa Mwenza wa Karibu ni mojawapo ya aina ya ukatili dhidi ya wanawake unaofanyika sana, na hujumuisha vitendo vibaya vya kimwili, kingono, na kisaikolojia na tabia za kudhibiti za mwenza wa karibu. Vitendo Vibaya vya Ngono: Kutishia kuingilia kimwili, kingono, iwe kwa nguvu au katika mazingira ya kutokuwepo kwa usawa au kwa kushinikiza.3 Utumwa wa Kingono: Matumizi yoyote mabaya yawe halisi au ya kujaribu kutumia vibaya 1 2 UN Wanawake, 2001. https://www.un.org/womenwatch/osagi/pdf/factsheet1.pdf 2 Angalia Mwongozo 2015 uk.5 wa Kitaasisi kuhusu Kamati ya Kudumu kuhusu Ukatili wa Kijinsia na DEVAW, 1993. 3 Ibid. 10 Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia nafasi ya udhaifu, tofauti kubwa katika nguvu, au Imani kwa madhumuni ya kingono, ikiwa bila kikwazo, kunufaika kifedha, kijamii, au kisiasa kutokana na utumwa wa Kingonio wa mtu mwingine.4 Unyanyasaji wa kingono: Aina yoyote ya kutongoza, kuomba upendeleo wa kingono usiotakiwa, na aina nyingine za matusi au tabia za kimwili zenye asili ya ngono.5 Ukatili wa Kingono: Ukatili wa kingono ni kitendo chochote cha tendo la ngono, jaribio la kufanya tendo la ngono, vitisho vya kudhuru au nguvu ya kimwili, kinachofanywa na mtu yeyote bila kujali mahusiano yake na muhanga, na maneno yoyote ya kingono yasiyotakiwa au kutongoza, au vitendo vya kumuuza mtu kingono, kwa kutumia nguvu. Ukatili Dhidi ya Watoto: Umefafanuliwa kuwa ni madhara ya kimwili, kingono, kihisia na/ au kisaikolojia, kutelekezwa, kuhudumia watoto kizembe (hawa ni watu chini ya miaka 18), pamoja na kukabiliana na madhara hayo, ambayo yanasababisha madhara halisi au yanayoweza kutokea kwa afya ya mtoto, maisha, maendeleo au utu katika muktadha wa mahusiano ya majukumu, kuaminiana na madaraka. Hii inajumuisha kuwatumia watoto kwa faida, kazj na kujifurahisha kingono au aina nyingine ya faida binafsi au kifedha. 4 Sekretariati ya Umoja wa Mataifa. 2003. ‘Jarida la Katibu Mkuu kuhusu hatua maalumu za Ulinzi dhidi ya Utumwa wa Kingono na vitendo vibaya’. ST/SGB/2003/13,, 5 6 Idara ya mambo ya nje ya Marekani. na. Sera ya Unyanyasaji wa Kijinsia,, 11 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania MUHTASARI RASMI Malengo ya Tathmini Malengo ya tathmini hii ni kutoa habari za usuli kuhusu masuala ya Ukatili wa Kijinsia (GBV),Sera, Programu, na mapungufu nchini Tanzania, kwa madhumuni ya kuisaidia Benki ya Dunia (WB) 1) kufikiria jinsi ya kusaidia moja kwa moja juhudi za kushughulikia GBV nchini Tanzania; 2) kuelekeza mikakati ya kuunganisha usikivu kwa GBV katika Programu za maendeleo; na 3) kuelewa upeo wa Programu za mwitikio za GBV. Pamoja na kutoa habari za jumla za data kuhusu upeo wa GBV nchini Tanzania, inachunguza: ulinzi wa kisheria na Sera kuhusiana na GBV; taratibu za mifumo na uratibu zilizopo kwa ajili ya kushughulikia GBV nchini Tanzania; na Programu za mwitikio na kuzuia GBV. Tathmini inachambua mapungufu muhimu katika maeneo ya uchunguzi kutegemea taarifa kutoka kwa wadau wakuu, pia na mapitio ya dawati, na kuhitimisha na mapendekezo kadhaa kwa WB, ili iweze kufikiria kusaidia kwenye kushughulikia mapungufu haya muhimu. Mbinu ya Tathmini Ripoti hii inaamuliwa na mapitio ya dawati kuhusu kuenea kwa GBV na mazingira ya kisheria na Sera nchini Tanzania, pia na mahojiano na watoa habari muhimu (KIIs), pia na mashauriano ya wadau na maafisa wa Serikali na wasiokuwa wa Serikali wanaohusika kwenye kuzuia na kupunguza GBV, ili kuelewa mitazamo na vipaumbele vyao. Tathmini inachukuliwa kuwa mapitio mepesi ili kutoa maoni ya jumla. Matokeo Muhimu Maeneo ya Maendeleo Mapungufu Muhimu uchunguzi Sheria na Sera Mfumo ambao kwa Haja ya maboresho katika za GBV wastani ni wa maendeleo Sheria mahususi zinazohusiana ulianzishwa juu ya Katiba na ukatili wa majumbani na yenye maendeleo na kubaka ndani ya ndoa. vifungu husika vya Sheria. Kutengwa kwa rasilimali finyu Mpango Kazi wa Taifa katika kusaidia utekelezaji wa (NPA) Zanzibar kuhusu NPA. Ukatili Dhidi ya Wanawake (VAW) na Ukatili Dhidi Hakuna ushahidi wa ufuatiliaji ta Watoto (VAC) ni kiini wa mifumo, inayochangU*wa cha kuendeleza juhudi za zaidi na viwango vidogo vya kitaifa za kushughulikia pesa. GBV. 12 Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia Mifumo na Mifumo jumuishi ya Uratibu haujapata rasilimali Uratibu wa uratibu iliyoandaliwa na za kutosha kutoka ngazi za taifa GBV NPA, kuanzia ngazi ya taifa hadi maeneo husika. hadi eneo husika. Mfumo wa kizamani Michakato ya rufaa kidogo wa kukusanya data inayotokana na jamii unaotumia karatasi kuhusu kupitia Kamati za Takwimu za utoaji huduma Kuwalinda Wanawake utoaji wa huduma za GBV, na Watoto (Kamati zinazuia kuelewa mielekeo na za MTAKUWWA) mahitaji. Ukusanyaji wa data zimeboresha uratibu za GBV hauonekani kwamba katika ngazi ya eneo zinakusanywa kwa utaratibu husika. maalumu, uliopangwa, na kuunganishwa vyema ili kuwezesha kufanya maamuzi. Programu za Programu za mwitikio Kuna mapungufu muhimu Mwitikio na zipo kwenye sekta zote kwenye sekta zote za mwitikio, Kuzuia GBV muhimu za mwitikio hususani kwa maana ya ubora wa sekta nyingi (afya, wa huduma na kuhakikisha saikolojia, sheria/haki na huduma zinamlenga muhanga. usalama (Polisi). Kuna mashauri machache Nyaraka za Msingi za ya GBV yanayofikishwa kuongoza zimeboresha mahakamani kutokana na mwitiko miongoni mwa kukosa ushahidi, kushindwa sekta hizi muhimu kukusanya na/au kuhifadhi kutoa kitini cha huduma ushahidi wa tukio, uchunguzi muhimu. mbovu, au rushwa kwenye mfumo.. Pamekuwepo na hatua kadhaa za kinga Haieleweki kama afua za zikizochukuliwa nchini kuzuia zimefanyiwa tathmini Tanzania, hususani na kwa matokeo na/ au zinaweza NGOs/ AZAKi. kuongezwa. Mapendekezo Sheria na Sera Juhudi za ziada za NPA za kuzifanyia maboresho Sheria ambazo zinadhoofisha haki za wanawake na wasichana kuwa huru kutoka kwenye ukatili na ubaguzi, hususani kwa kukuza utetezi kwenye vifungu mahususi vya Sheria vya ukatili majumbani na kubaka kwenye ndoa katika makosa ya jinai. Zingatia kuwezesha mkakati ambao unasaidia ufadhili endelevu kwa NPA na utekelezaji wake ulioharakishwa, kama vile kupitia kuanzishwa kwa mfuko mkubwa wa pamoja unaoongozwa na Serikali, ukisadiwa na sekta binafsi na Wadau wa Maendeleo. Hakikisha kwamba mkakati huu unajenga ahadi na uwezo wa Serikali wa kukidhi majukumu yake ya kibajeti kupitia maendeleo na utekelezaji wa mikakati ya kuhamasisha rasilimali fedha unaoendelea. Saidia tathmini ya NPA kwani wanakaribia kumaliza na wanaweza kutumika kama msingi wa maendeleo ya mpango unaokuja. 13 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania Kujenga juu ya mfano wa Shinyanga, (mkoa pekee nchini waliotiririsha ngazi NPA za Tanzania kwa kujenga mpango wake wenyewe ambao unaitikia juhudi za kusaidia kwa muktadha). Kutiririsha NPA za Tanzania hadi ngazi ya mkoa kama njia ya kujenga umiliki wa mkoa na utekelezaji wa NPA. Kusaidia kufanya mapitio ya Utekelezaji wa Mpango wa Sera ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii; kutathmini juhudi za sasa za kuongeza uwezeshaji kiuchumi wa wahanga wa GBV, na wanawake na wasichana walio katika hatari ya Ukatili na kubuni afua za ziada zinazolenga utulivu wa kiuchumi unaotokana na matokeo ya tathmini hii. Mifumo na Uratibu Kuimarisha mifumo ya taifa ya uratibu kwa kuwezesha mapitio ya haraka ya uekelezaji wa mfumo wa uratibu kwa kulenga msaada wa mapungufu muhimu katika ngazi ya Taifa, kama vile Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazaa na Watoto Jamii, (MoHCDGEC), pia na Sektariati ya Kamati Elekezi ya Taifa ya Ulinzi. Jumuisha katika uwezo kukuza ufuatiliaji na kuripoti kuhusu uratibu katika ngazi zote za mfumo wa uratibu. Wekeza katika maboresho ya mifumo ya usimamizi wa habari ya GBV ili kuhakikisha data za GBV zinazokusanywa nchi nzima ni za viwango na bora. Hii inaweza kufanyika kwa kukuza Mfumo wa Wilaya wa Kusimamia Mashauri (DCMS) katika wilaya ambako hazijaanzishwa. Mwitikio na Kuzuia Ongeza uwekezaji katika maendeleo au kuimarisha uwezo wa mifumo, miundo, na taratibu za mwitikio/huduma za GBV ili kuhakikisha upatikanaji, kufikiwa, utumiaji, mwitikio,na uwajibikaji wa huduma hizo katika mnyororo mzima wa utoaji wa huduma, hii ni katika sekta za Sheria, afya na ustawi wa jamii. Badilisha desturi za kijamii ambazo zinachangia katika uhaba wa kuripoti GBV kwa kukuza tabia za kutafuta msaada na kujenga uwezo wa watoa huduma ili kuwawezesha kuhakikisha mbinu zinazomlenga muhanga zinatumika katika GBV. Kusaidia maendeleo ya mfumo wa Taifa wa kufuatilia ubora na uendelevu wa utoaji huduma kwenye vituo vya Kutolea Huduma Mahali Pamoja (huduma za afya), pamoja na tathmini ya wafanyakazi na mrejesho kutoka kwa wahanga waliopata huduma. Wekeza katika mafunzo ya wafanyakazi kuhusu mbinu zinazomlenga muhanga and kupanua upatikanaji wa huduma kwa watu wanaopata huduma duni katika jamii kupitia Kamati za MTAKUWWA. Endeleza mkakati wa kujenga nguvukazi ya ustawi wa jamii na kuboresha uwezo wa maafisa ustawi wa jamii wa kutoa huduma za kisaikolojia kama sehemu ya usimamizi wa mashauri. Wezesha mafunzo ya Polisi kupitia Chuo cha Polisi pia kupitia mafunzo maalumu kwa Polisi na Dawati la Jinsia kuhusu Mwongozo uliopo wa Polisi, Jinsia na Dawati la Watoto.. Fikiria kufanya majaribio ya modeli ya Mahakama Maalumu ya Familia Zanzibar huku Tanzania Bara ili kujemga uaminifu, na katika michakato ya Mahakama na kuharakisha mashauri. Kujenga ufahamu wa kisheria miongoni mwa jamii kupitia tafsiri ya Sheria na Sera pia na kuunga mkono kampeni kubwa za jamii za uhisishaji. Unganisha hili na kuunga mkono msaada wa bure wa kisheria kwenye maeneo ambayo kwa sasa haupo kwa wahanga. Saidia kufanya mapitio ya Mkakati wa Kitaifa wa Jamii na Huduma za Mkoba wa NPA kuhakikisha kwamba mbinu yake inaendana na utendaji bora kwa ajili ya kuzuia GBV, kwa kubadili desturi za kijamii na fikiria kuongeza vipengele vya Mkakati ili kusaidia mabadiliko ya tabia yanayopimika. 14 Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia 1. Usuli wa Tathmini ya Ukatili wa Kijinsia 1.1 Madhumuni ya Tathmini Tathmini hii iliamriwa na Benki ya Dunia ili kutoa habari za msingi kuhusu masuala ya GBV, Sera, Programu, na mapungufu kwa mtazamo wa kuisaidia Benki ya Dunia kufanya yafuatayo: a) kufikiria jinsi ya kusaidia moja kwa moja juhudi za kupambana na GBV nchini Tanzania; b) kuelekeza mikakati kwa kuunganisha usikivu kwa GBV katika Programu za Maendeleo; na c) kuelewa upeo wa Programu za mwitikio wa GBV ndani ya Jamhuri ya Muungano. Hii haitairuhusu Benki ya Dunia tu kuweka mkazo kwa Programu za GBV kimkakati zaidi (zaidi ya msingi wa mradi mmoja mmoja) ili kuongeza kwa kiwango cha juu uwekezaji, lakini pia kusaidia kuelewa asili na uwanda wa huduma za GBV zinazoweza kupatikana kwa wahanga wa utumwa wa kingono (SEA) na vitendo vibaya, na/au unyanyasaji wa kingono (SH) katika miundombinu na miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Benki ya Dunia.6 Kwa umahususi zaidi, tathmini inachunguza: Data zilizopo kuhusu GBV na kuenea kwa aina tofauti za GBV Mfumo wa kitaifa wa sheria na Sera ambazo zinashughulikia GBV Mipangilio ya kitaasisi na taratibu za uratibu kwa ajili ya mwitikio wa GBV Programu za mwitikio wa GBV kwa sasa zinapatikana kwa afua za kuzuia GBV kwa wahanga. Tathimini inachambua mapungufu muhimu kwenye maeneo yote haya ya uchunguzi kutokana na michango kutoka kwa wadau muhimu pia na mapitio ya dawati na kuhitimisha na mapendekezo kadhaa kwa Benki ya Dunia ili ifikirie kusaidia katika kushughulikia mapungufu haya muhimu. 1.2 Mbinu ya Tathimini Jumuisho la mbinu lilitumika katika uchunguzi huu, pamoja na mapitio ya dawati na mahojiano na wadau wakuu. 1.1.1 Mapitio ya Dawati Mapitio ya dawati yanajumuisha uchunguzi wa fasihi juu ya kuenea na vichochezi vya GBV nchini Tanzania pia Sheria na Sera zinazohusiana na GBV na utendaji mzuri ambao unaweza kuelekeza mapendekezo ya kuchukuliwa hatua. 1.1.2 Mashauriano ya Wadau Mapitio ya dawati yaliongezewa na mashauriano na wataalamu wa GBV waliochaguliwa kutoka ngazi za kitaifa na kimkoa wakati wa kongamano la mashauriano ya wadau ya siku 2 kisiwani Zanzibar, mwezi Novemba 2019, ukiwa na wawakilishi kutoka Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto-Zanzibar; Maafisa wa Polisi kutoka Madawati ya 6 Tathmini hii hailengi kwenye Ukatili wa Kingono au Utumwa wa Kingono (SEA/SH) katika Miradi inayofadhiliwa na Benki ya Dunia (WB). Hata hivyo, kwa kutambua kwamba matunzo na msaada kwa Muhanga ni jukumu kuu la Mpango kazi wa SEA/SH, Habari zilizomo kwenye Ripoti hii zinaweza kutumika kama rejea kwa miradi ya kuelewa upatikanaji wa, na mapungufu ya huduma za Ukatili wa Kijinsia (GBV) nchini Tanzania. Tathmini hii pia haichunguzi kiwango ambacho miradi ya maendeleo ya WB inavyounganisha mikakati ya kupunguza GBV kutokea katika ngazi ya jamii wakati wa utekelezaji wa Mradi. Ripoti hii itafuatiwa na utafiti kuhusu uwekezaji wa WB nchini Tanzania ambao utatoa Mwongozo mahususi kuhusu kuboresha uwezo wa mradi kushughulikia SEA na SH, pamoja na rufaa za Muhanga, pia itazingatia mikakati inayowezekana kwa ajili ya kupunguza hatari ya GBV katika baadhi ya miradi ya maendeleo iliyochaguliwa. 15 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania Jinsia na Watoto; Mashirika ya UN; na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar. Maswali yaliwakilishwa ili kuwezesha michango kuhusu mazingira ya GBV, changamoto na na fursa. Aidha, mahojiano ya watoa habari muhimu kwa kutumia mwongozo wa mahojiano yalifanyika jijini Dar es Salaam na kuhusisha Huduma za Ustawi wa Jamii, Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Mashirika ya UN, na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali. Mashauriano ya ziada yalifanyika na wabia waliochaguliwa kufanya mapitio ya mapendekezo yaliyotolewaa. Mwongozo wa mahojiano umejumuishwa katika Kiambatisho 1 na orodha ya watoa habari muhimu katika Kiambatisho 2. 1.1.3 Ukomo Data kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na wasichana nchini Tanzania zimeongezeka kwa wingi katika miaka ya hivi karibuni. Hata hivyo, data kuhusu asili na ukubwa wa Programu za GBV haijakusanywa au kupatikana kwa urahisi. Upeo finyu wa KII pia athari za uwezo wa kukusanya habari kuhusu upeo kamili wa Programu za GBV kwenye nchi nzima ya Tanzania. Hivyo basi, habari zilizowakilishwa katika tathmini hii sio kamilifu, bali ni mfano mdogo unaokusudia kutoa picha ya baadhi ya miundo muhimu iliyopo kuwezesha kuzuia GBV na mwitikio nchini, na kusisitiza baadhi ya mapungufu muhimu ya miundo hii. 16 Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia 2. Jinsia na Maendeleo nchini Tanzania 2.1 Muktadha wa Maendeleo Tanzania imeshuhudia zaidi ya miaka 20 ya ukuaji endelevu wa uchumi, na mnamo Julai 2020, rasmi ilipewa hadhi ya kuwa nchi yenye kipato cha kati ngazi ya chini kuliko nchi yenye kipato cha chini. Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025 inalenga kufikia hadhi ya kipato cha kati ifikapo 2025 na kusisitiza hatua muhimu kuelekea kuongeza maendeleo ya binadamu na mtaji wa miundombinu, pamoja na usawa wa kijinsia katika muktadha wote wa kijamii, kiuchumi, na kisiasa.7 Kuanzia 2007 hadi 2018, Tanzania kwa mafanikio ilipunguza viwango vya umaskini kwa asilimia 8, kutoka asilimia 34.4 mnamo 2007 hadi asilimia 26.4 mwaka 2018.8 Upungufu huu umepungua kasi, hata hivyo, katika miaka ya hivi karibuni, kulikuwa na wastani wa kupungua kwa mwaka katika viwango vya umasikini vikipungua kutoka asilimia 1 hadi asilima 0.3.9 Wakati kiwango cha ushiriki cha nguvu kazi ya wanawake wa Tanzania ni mojawapo ya juu zaidi kwenye Bara, wanawake wanaonekana wamefaidika kidogo kutoka kwenye mageuzi ya miundo kwenye uchumi hadi sasa, pakiwa na mpito usioenda haraka kutoka kilimo na kuingia kwenye aina nyingine za ajira ukilinganisha na wanaume.10 2.2 Ukosefu wa Usawa wa Kijinsia Kiwango cha uzazi cha jumla nchini Tanzania kiko juu kwa vizazi 4.8 kwa kila mwanamke na hii inachochewa kwa upande mmoja na viwango vya juu vya uzazi kwa vijana waliobalehe na ndoa za utotoni. Kiwango cha juu cha uzazi, uzazi kwa vijana waliobalehe, na ndoa za utotoni zinahusiana kupungua kwa shughuli za kiuchumi, viwango vya chini vya elimu, umaskini, na kupungua harakati. Kiwango cha juu cha uzazi, hususani uzazi kwa vijana waliobalehe, pia unahusishwa na matokeo mabaya ya afya ya wanawake pia na watoto wao. Kwa kiwango cha juu, kiwango kikubwa cha uzazi huzuia nchi kunufaika na faida za kidemografia, suala muhimu ambalo lazima lihusishe kupungua kwa haraka kwa uzazi. WWakati nchi imeelekea kwenye usawa wa kijinsia katika ushiriki wa wasichana na wavulana katika viwango vya chini vya elimu, kwa Tanzania Bara bado kuna mapungufu makubwa ya kijinsia katika ngazi ya juu ya sekondari, ambako ada za shule bado zipo. Upatikanaji wa elimu ya sekondari ya ngazi za chini miongoni mwa wanawake inahusiana na mimba za utotoni, kuongezeka kwa viwango vya uzazi, kupungua kwa fursa za kiuchumi na kupungua kipato cha maisha. Wakati Tanzania imefikia karibu ya usawa wa kijinsia katika elimu ya awali, msingi, na ngazi ya chini ya sekondari, mpito kuelekea ngazi za juu za elimu ya sekondari kunaambatana na ongezeko kubwa kwa wanawake kuacha kujiandikisha kunakoendana na mwanzo wa balehe na kuambatana na hatari za mimba za utotoni, mimba za vijana, na majukumu ya ziada ya kaya.11 7 “Taarifa za jumla kuhusu nchi ya Tanzania,” Text/Html, World Bank, Accessed September 16, 2021, https://www. Worldbank.Org/En/ Country/Tanzania/Overview. 8 “Njia ya Tanzania kuelekea Kupunguza Umaskini na Ukuaji wa Uchumi unao wajali Maskini.” World Bank, Accessed December 11, 2021. https://www. worldbank.org/en/country/tanzania/publication/tanzanias-path-to-poverty- reduction-and-pro-poor-growth. 9 Ibid. 10 Ardina Hasanbasri†, Talip Kilic‡, Gayatri Koolwal# And Heather Moylan. 2021. LSMS+ Programu katika Afrika Kusini mwa Sahara: Matokeo kuhusu Ukusanyaji wa Data kwenye ngazi ya mtu binafsi, inayohusiana na Kazi, Umiliki wa Mali na Haki. World Bank. https:// openknowledge.worldbank.org/bitstream/handle/10986/35544/LSMS-Programu katika Afrika chini ya Sahara - Matokeo kuhusu Ukusanyaji wa Data kwenye ngazi ya mtu binafsi, inayohusiana na Kazi, Umiliki wa Mali.pdf?sequence=5 11 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Muhtasari wa Takwimu za Elimumsingi, 2004-2017; Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ripoti ya Utendaji ya Sekta ya Elimu, 2018/2019. 17 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania Mapato kutoka kwa wanawake wajasiriamali ni asilimia 46 ya yale ya wajasiriamali wanaume. Tofauti hii ni matokeo ya visababishi vingi vinavyochangia kuongeza, vinavyojumuisha malipo ya chini kwenye mishahara ya wafanyakazi waliopo kwenye biashara zao, mapato ya chini kwenye kielekezi cha utajiri, na viwango vya chini vya usajili. Aidha, wanaume wana uwezekano mkubwa zaidi wa kutumia akiba zao kutoka kwenye biashara ambazo sio za kilimo kama mtaji wa kuanzia, wakati wanawake wanaonekana wakitegemea zawadi kutoka kwa familia na marafiki, ambayo inaweza kuzuia uwezo wa wanawake kupata kwa haraka na uendelevu wa kukua kwa biashara katika muda mrefu. Wakulima wanawake hupata mavuno madogo kuliko wenzao wanaume kwa makisio ya asilimia 20 hadi 30. Data za Uchambuzi unaotumia Utafiti Unaopima Viwango vya Maisha (LSMS) unaashiria kwamba sababu za uwepo wa mapungufu ng’ang’anizi ya kijinsia umejikita katika upatikanaji mdogo kwa wanawake wa nguvu kazi ya wanaume shambani, na mapato madogo kutoka kwenye pembejeo za nguvu kazi na zisizo za nguvu kazi, kama vile viuadudu na mbolea.12 Katika uchumi uliotawaliwa na kilimo kwa sehemu kubwa ambako kilimo huchangia asilimia 65 ya nguvu kazi yote, tofauti hizi huakisi na kuimarisha tofauti kubwa za kijinsia.13 Kwa ujumla, wanawake wana uwezo mdogo wa nguvu ya kufanya maamuzi kuliko wanaume nchini Tanzania. Ndani ya kaya, wanawake wana uwezo mdogo kuliko waume zao kuhusika na kufanya maamuzi kuhusu afya zao, manunuzi makubwa ya kaya, na kutembelea familia na ndugu zao. Kwa sasa wanawake walioolewa hivi karibuni ambao wanaingiza kipato kwa kazi wanazofanya, zaidi ya nusu ya wanawake huamua pamoja jinsi ya kutumia mapato yao na waume zao, zaidi ya theluthi hufanya maamuzi huru, na takribani moja ya kumi (1/10) ya wanawake wana ripoti kuwa waume zao ndio wafanya maamuzi wakuu katika jinsi ya kutumia mapato ya mwanamke. Wanawake wana uwezekano wa kushiriki kwenye maamuzi haya kadri umri unavyoongezeka, iwapo wanaishi katika maeneo ya mjini, wameajiriwa kwa mshahara, wana viwango vya juu vya elimu, au ni wanakaya wa kaya tajiri.14 12 Slavchevska, V. (2015). Tofauti za Kijinsia katika Tija za Kilimo: Kisa cha Tanzania. Uchumi wa Kilimo, 46(3), 335-355. 13 “Ajira kwenye Kilimo, Wanawake (Asilimia ya Wanawake kwenye Ajira) (Makisio ya ILO) - Tanzania | Data,” Accessed August 31, 2021, Https://Data.Worldbank.Org/Indicator/SL.AGR.EMPL.FE.ZS?Locations=TZ. 14 Utafiti wa DHS Tanzania 2015/2016. 18 Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia 3. Upeo wa Tatizo la GBV Takwimu Muhimu Kitaifa, asilimia 40 ya wanawake wote wenye umri 15-49 wamepitia ukatili wa kimwili, wakati asilimia 17 wamepitia ukatili wa kingono. Kati ya wanawake wenye umri 15-49, asilimia 44 wamepitia ama ukatili wa kimwili au wa kingono na mwenza wa karibu Kuenea kwa Ukatili wa Mke15 uko juu zaidi katika maeneo ya vijijini, ukiwa na wastani wa asilimia 52 wakati kuenea kwenye maeneo ya mijini ni wastani wa asilimia 45. Takribani asilimia 30 ya wasichana wamepitia ukatili wa kingono kabla ya miaka 18. Wastani wa kuenea kwa ukeketaji (FGM) miongoni mwa wasichana na wanawake wenye umri 15-49 ni asilimia 10. Asilimia 58 ya wanawake na asilimia 40 ya wanaume wanaamini kwamba mume ana haki ya kumpiga mkewe katika mazingira fulani. Miongoni mwa wanawake ambao hawajapata kuolewa, asilimia 16 wamepitia ukatili wa kimwili na asilimia 9 wamepitia ukatili wa kingono. Ni asilimia 54 tu ya wanawake nchini Tanzania ambao hawajapitia ukatili wa kimwili au wa kingono walitafuta msaada. Chanzo: TDHS-MIS 2015-2016 Istilahi ya ‘GBV’ inatumiwa mara nyingi kusisitiza ukosefu wa kimfumo wa usawa baina ya wanaume na wanawake—ambao upo katika kila jamii duniani—ni sifa inayounganisha na ya msingi ya aina nyingi za ukatili unaotekelezwa dhidi ya wanawake na wasichana. Wakati ukosefu wa usawa wa kijinsia daima uko katika mzizi wa GBV, pia kuna visababishi vyingine vinavyochangia ambavyo vinaweza kuongeza hatari hii nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na viwango vya juu vya ndoa za utotoni na kuzaa, viwango vya chini vya kujitegemea kiuchumi na viwango vya chini vya mapato miongoni mwa wanawake, viwango vya chini vya elimu miongoni mwa wanawake, kuwepo kwa tofauti kubwa ya umri baina ya waume na wake, na ndoa za mitala. Visababishi hivi, vikiunganishwa na tofauti nyingine katika ukuaji wa miji, kilimo, hali za kiuchumi, na desturi za kitamaduni, kuchangia katika sehemu kubwa ya tofauti za mikoa kwenye kuenea kwa GBV kulikoelezwa hapa chini. 3.1 Data Zilizopo Wanawake na wasichana nchini Tanzania hupitia ukatili katika maisha yao yote kuanzia utotoni hadi uzee. Sehemu inayofuata imepangwa kuakisi jambo hili. Kwa kutumia vyanzo vingi vya Habari, ikiwemo Utafiti wa Demografia na Afya (DHS 2015-2016), Utafiti wa Taifa kuhusu Ukatili Dhidi ya Watoto Tanzania Bara na Zanzibar (2011), na tafiti nyingine ili kuelezea kwa usahihi upeo na kuenea kwa GBV katika hatua zote za maisha. 15 Ukatili wa Kingono dhidi ya Mwenza unaojumuisha Ukatili wa Kimwili, Kingono au Kisaikolojia. 19 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania 3.1.1 Ukatili wa Kimwili na Kingono dhidi ya Mtoto Utafiti wa Taifa kuhusu Ukatili Dhidi ya Watoto ilitoa ripoti yake mwaka 2011, ilikadiria kwamba asilimia 75 ya Watoto walipitia ukatili wa kimwili uliotekelezwa na ndugu kabla ya kufikisha miaka 38.16 Takribani robo tatu ya wanawake waiipitia ukatili wa kimwili uliofanywa na ndugu, watu wa mamlaka (kama walimu) au mwenza wa karibu kabla ya miaka 18, na zaidi ya nusu ya wanawake wa umri wa miaka 13 hadi 17 waliripoti kwamba walipitia ukatili wa kimwili katika mwaka uliopita.17 Matokeo mengi ya ukatili huu yalifanyika kwa kupigwa ngumi, kuchapwa bakora, au kupigwa mateke. Kiwango cha juu cha ukatili wa kimwili dhidi ya Watoto kinaakisi matumizi makubwa ya adhabu ya kiboko ambayo inaruhusiwa kwenye shule na hutumiwa majumbani nchi nzima. Mnamo Agosti 2019, Serikali ya Tanzania Bara ilichukua hatua muhimu ya kuwakataza walimu katika ngazi za chini za shule za Msingi wasiingie madarasani na bakora. Hata hivyo, matumizi ya adhabu kali ya viboko, pamoja na kupiga, ngumi, na kuwalazimisha wanafunzi kuwa katika hali ya kudhalilisha na inayowatesa darasani, bado inatokea sana, na shirika la haki za binadamu la Human Right Watch linaripoti kwamba ukatili huu wa kimwili pia umeonyeshwa kusababisha ukatili wa kingono baadaye dhidi ya wasichana katika shule za sekondari za wasichana.18 AKulingana na utafiti huo huo wa VAC, takribani wanawake 3 kati ya 10 wanawake wa Kitanzania waliripoti angalau shambulio moja la ukatili wa kingono kabla ya umri wa miaka 18. Aina ya ukatili wa kingono waliyopitia wasichana hao ilikuwa kuwashika kingono, iliyofuatiwa na jaribio la kuwaingilia kingono. Asilimia sita ya wanawake waliripoti kwamba walilazimishwa kimwili kufanya tendo la ngono kabla ya umri wa miaka 18. Walipoulizwa kuhusu uzoefu wao kwa mwaka uliopita kabla ya utafiti, asilimia 14 ya wanawake wa umri wa miaka 13 hadi 17 waliripoti kwamba aina moja ya ukatili wa kingono.. Wakatili watatu walioripotiwa sana walikuwa ni: wageni (asilimia 32.5), majirani (asilimia 24.8), na wachumba (asilimia 24.6), wengi wao (asilimia 70) wakiwa na umri mkubwa kuliko muhanga.19 Kwa wale waliofanya tendo la ngono kwa mara ya kwanza kabla ya umri wa miaka 18, takribani theluthi moja (asilimia 29.1) ya wanawake waliripoti kwamba ngono yao ya kwanza ililazimishwa au kushinikizwa. Asilimia themanini na moja waliripoti kupokea pesa au vitu kwa ajili ya ngono ukilinganisha na asilimia 24.6 ambao hawakupokea.20 3.1.2 Ukeketaji Kulingana na ripoti ya TDHS-MIS 2015-2016, wastani wa kuenea kwa ukeketaji (FGM) miongoni mwa wasichana na wanawake wenye umri 15-49 nchini Tanzania umepungua kutoka asilimia 18 mwaka 1996 hadi asilimia 15 mwaka 2013 hadi asilimia 10 mwaka 2016. TKuenea kwa FGM kunaonekana kuko chini sana (hadi asilimia 1 tu) kwa wasichana wa miaka 14 na vijana zaidi. Hata hivyo, hii inawezekana kuwa ni makadirio ya chini ya ueneaji halisi wa desturi hii kwani wakatili wanaweza kuwa wanaogopa kukubali kushiriki kwenye desturi—na 16 Ukatili dhidi ya Watoto nchini Tanzania: Matokeo kutoka Utafiti wa Taifa, 2009. Muhtasari wa Ripoti kuhusu Ueneaji wa Ukatili wa Kingono, Kimwili na Kisaikolojia; Muktadha wa Ukatili wa Kingono na Afya; na Matokeo ya Ukatili ulio tendeka katika Utoto; Dar es Salaam, Tanzania: UNICEF Tanzania, Kitengo cha Kuzuia Ukatili, Kituo cha Taifa cha Kuzuia na Kudhibiti Majeraha; Vituo vya Kudhibiti na kinga ya Magonjwa; na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Muhimbili, 2011 112009; Utafiti wa Taifa Kuhusu Ukatili dhidi ya Watoto; uk 27. 17 Ibid, 98. 18 Martínez, Elin. (2019) “Tanzania: Kutokomeza Ukatili Shuleni huanza kwa Kupiga marufuku Viboko Madarasani.” (Human Rights Watch). https://www.hrw.org/news/2019/09/03/tanzania-ending-violence-schools-begins-banning- canes-allclassrooms. 19 Ibid, 43. 20 2009, Utafiti wa Taifa kuhusu Ukatili dhidi ya Watoto, uk 76. 20 Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia kwa sababu FGM katika mikoa mingi hufanywa kwa wasichana wa miaka 13 na kuendelea.21 Ueneaji wa FGM kitaifa nchini Tanzania pia unaonyesha tofauti kubwa kimkoa. Kama inavyoonyeshwa katika Kielelezo hapo chini, makadirio ya hivi karibuni ya ueneaji wa FGM ni kutoka asilimia 58 mkoani Manyara hadi chini ya asilimia 1 kwenye maeneo mengi Magharibi ya Tanzania.22 Kwenye mikoa iliyo na ueneaji wa FGM wa juu sana, desturi hii inachochewa na desturi zenye madhara za kitamaduni, imani na mila. Inaaminika kwamba FGM ni lazima kwa sababu wasichana wasiopitia FGM ni wachafu na hawafai na mizimu itawaadhibu wale wanaoacha desturi ya kimila ya FGM.23 FFGM inaonekana kuwa ni mila ya lazima kwa wale wanaotoka rika moja kwenda jingine kuwanigiza wasichana kwenye utu uzima, kuzuia ngono kabla ya ndoa, na kupata mahari ya juu msichana anapochumbiwa.24 Kielelezo 1: Ueneaji wa FGM mwaka 2015-2016 kwa mkoa 21 TDHS-MIS 2015-2016 Page 360 22 Mwelekeo huu wa tofauti baina ya Mikoa umeonekana katika tafiti nyingi, ikiwa ni pamoja na Ukeketaji/Kunyofoa (FGM): Muhkutasari wa Kitakwimu na Uchunguzi wa Matukio umebadilika. UNICEF, Julai 2013, uk 31. Accessed on 30th May 2020. htt ps://www.unicef.org/publicati ons/index_69875.html 23 Ibid. 24 Ibid. 21 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania Wasichana wana aminishwa kutaka kufanyiwa FGM ili wakubaliwe na familia na jamii zao, baadhi wakidai kwamba FGM inawasaidia wasichana kuepuka kupata VVU/UKIMWI, kuzuia magonjwa ya njia ya mkojo na kuhakikisha hawapati ugumba au kuzaa watoto walemavu wa- takapo olewa.25 Kukubalika kwa vitendo vya ukeketaji na jamii kunahakikisha kwamba wale wasiofanyiwa FGM, wanabaki hawaolewi na hulazimishwa kufanyiwa FGM wakiwa watu wazi- ma iwapo wataamua kuolewa.26 Mnamo 2018, Mfuko wa Idadi ya Watu wa Umoja wa Mataifa (UNFPA) ilitoa hitimisho kwam- ba “Kwa ujumla kupungua kunako onekana katika FGM hakutoshi kuondoa ukuaji wa watu unaotarajiwa, kwani mwanamke mmoja kati ya kumi nchini Tanzania (umri 15-49) amefa- nyiwa FGM; kati ya hawa, asilimia 35 walifanyiwa FGM kabla ya umri wa mwaka mmoja.”27 3.1.3 Ndoa za Utotoni Data wa kutoka mwaka TDHSMIS Table 1: Mikoa Mitano ya Juu Zaidi yenye utafiti wa unaashiria 2015-2016 kwamba zaidi ya msichana 1 kati Ndoa za Utotoni (2017) ya wasichana 3 nchini Tanzania wanaolewa kabla ya miaka 18. Hii Mkoa Asilimia ya wahojiwa inawakilisha punguzo dogo, lutoka wanawake waliripoti asilimia 40 mwaka 2010 hadi asilimia kwamba waliolewa 36 mwaka 2015-16. Katika utafiti wa mwaka 2017 kuhusu vichocheo na kabla ya miaka 18 matokeo ya ndoa za utotoni nchini Tanzania, Wizara ya Afya, Maende- Tabora 76% leo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Wato- Shinyanga 64% to (MoHCDGEC) ilithibitisha kwam- Mara 55% ba kuenea kwa ndoa za utotoni bado uko juu katika mikoa mingi ya Dodoma 45% nchi. Jedwali 1 linaonyesha asilimia Manyara 44% ya wahojiwa wanawake wanaoripo- ti kwamba waliolewa kabla ya mia- ka 18 kwenye mikoa mitano (5) nchini Tanzania iliyo na kiwango cha juu zaidi cha kuenea.28 Kiwango cha ndoa za utotoni kiko juu hususani kwenye baadhi ya makabila kama vile Wamasai na Wagogo, ambako ndoa za utotoni zinahusishwa kwa karibu na FGM.29 Wanawake na wana- ume kwenye maeneo ya mijini huoa/huolewa baadaye zaidi kuliko wenzao kwenye maeneo ya vijijini, na wanawake walio na angalau kiwango cha elimu ya sekondari, huolewa baadaye zaidi kuliko wanawake wasio na elimu, wakiwa na wastani wa miaka 23.6 na miaka 17.8, mtawalia.30 25 Ibid. 26 Ibid, 8. 27 Umoja wa Mataifa, Tanzania, UNFPA, Tanzania na Umoja wa Ulaya. FGM Fact Sheet P. 2. Accessed 30th May 2020. https:// tanzania.unfpa.org/sites/default/files/pub-pdf/FGM_FACTSHEET_24sept_highres.pdf 28 Utafiti wa Taifa kuhusu Vichochezi na Matokeo wa Ndoa za Utotoni nchini Tanzania, Februari 2017, uk. 39. 29 “Hakuna Namna: Ndoa za Utotoni na Ukiukaji wa Haki za Binadamu nchini Tanzania” (Human Rights Watch, Oktoba 29, 2014), Https:// Www.Hrw.Org/Report/2014/10/29/No-Way-Out/Child-Marriage-And-Human-Rights-Abuses-Tanzania. 30 TDHS-MIS (2015-2016) 22 Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia 3.1.4 Ukatili wa Mwenza wa Karibu Kiwango kilicho ripotiwa cha ukatili miongoni mwa wanawake walioolewa nchini Tan- zania kinaanzia asilimia 78 katika mikoa ya Mara na Shinyanga hadi asilimia 8 tu Kas- kazini Pemba na asilimia 9 huko Kusini Pemba. Kwa ujumla, asilimia 44 ya wanawake wenye umri 15-49 wamepitia ama ukatili wa kimwili au kingono uliofanywa na mwen- za wa karibu. Kwa kiasi kikubwa hiki ni kiwango cha juu sana kuliko makadirio ya dun- ia ya kuenea kwa Ukatili wa Mwenza wa Karibu (IPV) miongoni mwa wanawake wa umri 15-49 wa asilimia 27, na wastani wa kanda ya Afrika Kusini mwa Sahara wa asilimia 33.31 Wakati mbinu na muda wa vyombo tofauti vya utafiti vikifanya uchunguzi wa IPV vikitofau- tiana, hivyo ulinganisho ufanyike kwa uangalifu, makadirio kutoka tafiti za WHO zinaashiria kwamba IPV inafanyika zaidi nchini Tanzania, kuliko nchi nyingine nyingi ambazo WHO ilifanya utafiti huo huo. Kwa kweli, ukilinganisha data za WHO na nchi nyingine, Tanzania ipo katika 12 bora za kiwango cha juu zaidi cha kuenea kwa IPV katika kanda ya Afrika.32 Ukatili wa kimwili na kingono unaweza usitokee kwa kujitenga; bali wanawake wanaweza kupitia mchanganyiko wa aina tofauti za ukatili wakiwa na wenza wao wa karibu. Kulingana na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), huduma za msaada wa kisheria unaonyesha kwamba IPV inaongezeka, lakini hairipotiwi. Kielelezo 2: Kuenea kwa IPV Dhidi ya Wanawake ambao Hawajapata Kuolewa, kwa Mkoa (2015-2016) 31 Makisio ya Uenezi wa Ukatili wa Mwenza wa karibu dhidi ya Wanawake, WHO, 2018. Uenezi wa Kidunia, Kikanda, na Kitaifa. Ukatili wa Kingono usio kuwa wa Mwenza dhidi ya Wanawake na Uenezi wa Kidunia na Kikanda. htt ps://www. who.int/publicati ons/i/item/9789240022256, pgs. 22, 24. 32 WHO Afaya ya Kingono na Uzazi, na Utafiti. Accessed December 11, 2021. htt ps://srhr.org/vaw-data/ data?region=Africa®ion_class=WHO&violence_type=ipv&violence_ti me=lifeti me&age_group=15_49 23 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania Utafiti wa hivi karibuni wa DHS unaonyesha kuenea kwa ukatili wa kimwili miongoni mwa wanawake baada ya miaka 15 upo katika asilimia 40, miongoni mwa wanawake wa umri 15- 49.33 Asilimia ya wanawake waliopitia ukatili wa kimwili tangu wakiwa na miaka 15 haijabadilika kwa Tanzania Bara tangu utafiti wa TDHS-MIS wa mwaka 2010, lakini umeongezeka kutoka asilimia 10 hadi 14 visiwani Zanzibar.34 Wanawake 7 kati ya 10 waliopitia ukatili wa mwenza wa karibu, walipata aina tofauti za majeraha ambayo ni: kukatwa, michubuko au maumivu; asilimia 15 waliripoti vidonda vikubwa, kuvunjika mifupa au meno, na majeraha makubwa. Wanawake walioolewa wanakumbana zaidi na ukatili zaidi ya wale wasioolewa.35 Kwa vigezo vya mwelekeo, asilimia 16 ya wanawake ambao hawajapata kuolewa, wamepitia ukatili wa kimwili tangu wakiwa na miaka 15, ukilinganisha na asilimia 63 ya wanawake waliotalakiwa, waliotengana, au wajane, na asilimia 44 ya wanawawake walioolewa hivi karibuni.36 Kwa ujumla, asilimia 8 ya wanawake wajawazito wamepitia ukatili wa kimwili wakati wa ujauzito.37 Utafiti uliofanywa mwaka 2017 kuhusu GBV mkoani Mwanza uligundua kwamba asilimia 61 ya wanawake waliohojiwa walipitia ama ukatili wa kimwili na/au ukatili wa kingono kwenye ndoa zao.38 Asilimia Sitini na nane ya wanawake waliripoti kwamba walipitia ukatili wa kimwili katika maisha yao, na asilimia 82 ya nwanawake walipitia tabia za kuwadhibiti ilinayofanywa na mwenza katika maisha yao.39 Utafiti uliongeza kwamba “uwiano mkubwa wa wanawake waliripoti ukatili mkubwa wa kimwili ambao ulitokea mara kwa mara, ukiashiria kwamba hili ni jambo la kawaida miongoni mwa wanawake wa watu hawa.”40 Kukubalika kwa matumizi ya ukatili na waume/wenza uko juu nchini Tanzania, pamoja na miongoni mwa wanawake. Kulingana na utafiti wa TDHS-MIS wa mwaka 2015-2016, asilimia 58 ya wanawake, na asilimia 40 ya wanaume wanaamini kwamba mume ana haki ya kumpiga mkewe chini ya mazingira fulani, mfano, kama mke akiunguza chakula, akibishana naye, akitoka nje bila kumuambia, akitelekeza watoto au kumnyima unyumba; wanawake 3 kati ya 10 wanaamini inakubalika kumpiga mwanamke anayetoka nje bila kwanza kumuambia mume wake; wanaume 3 kati ya 10 wanafikiri inakubalika kwa mume kumpiga mke wake ikiwa hawatunzi watoto au anabishana naye.41 Kuvumilia kupiga wake inaonekana kuwa imebakia kuwa jambo la kawaida. Asilimia ya wanawake wanaokubali kwamba kupiga mke kunakubalika kumepungua kutoka asilimia 60 katika utafiti wa TDHS – MIS mwaka 2004-05 hadi asilimia 54 katika TDHS-MIS ya mwaka 2010, lakini uliongezeka hadi asilimia 58 mwaka 2015- 16. Visiwani Zanzibar, karibu asilimia 60 ya wanawake na zaidi ya asilimia 50 ya wanaume wanaunga mkono wanaume kupiga wake zao katika mazingira yoyote yaliyowasilishwa hapo juu.42 Hata kwenye vizazi kijana zaidi, wanawake, 4 kati ya 10 (asilimia 40.8) na karibu mwanaume 1 kati ya 2 (asilimia 46.0) wa umri wa 13 hadi 24 wanaamini kwamba ilikuwa stahiki kwa mume kumpiga mke wake. Asilimia Sitini na mbili (62%) ya wanawake waliopitia 33 Ibid, 368. 34 Ibid, 368. 35 Kanzi data ya Umoja wa Mataifa kuhusu Ukatili dhidi ya Wanawake 36 TDHS MIS 2015-2016, page 369. 37 Ibid, 369. 38 Ibid, 4. 39 Ibid,. 40 Ibid, 7. 41 Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania 2011, Ukatili dhidi ya Watoto nchini Tanzania: Matokeo kutoka Utafiti wa Taifa 2009, Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF), Vituo vya Kudhibiti Magonjwa Marekani (CDC), Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi. 42 Ibid, 83. 24 Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia ukatili wa kimwili wakiwa watoto, uliofanywa na ndugu, walielezea kuunga mkono kupiga mke, ukilinganisha na asilimia 53.0 ambao hawakupitia ukatili wa kimwili wakiwa watoto uliotekelezwa na ndugu. Kwa wanaume, asilimia 56.4 ya wale waliopitia ukatili wa kimwili uliotekelezwa na ndugu wakiwa watoto, waliamini kwamba ukatili wa kimwili unakubalika, ukilinganisha na asilimia 49.3 ambao hawajapitia ukatili wa kimwili wakiwa wadogo.43 3.1.5 Ukatili wa Kingono Kulingana na utafiti wa DHS wa mwaka 2015-2016 nchini Tanzania, asilimia 17 ya wanawake wote wenye umri 15-49 wamepitia ukatili wa kingono. Asilimia saba (7) ya wanawake wenye umri wa miaka 18 au zaid walipitia ukatili wa kingono kabla ya wenye miaka miaka 18, na asilimia mbili (2) ya wanawake wote wenye miaka 15-49 walipitia ukatili wa kingono kabla ya kufika miaka 15.44 Kielelezo 3: Kuenea kwa Ukatili wa Kijinsia kwa Hadhi ya Ndoa (TDHS-MIS 2015-2016,45) Kuenea kwa ukatili wa kingono kuna tofauti kati ya mikoa na vikundi. Uwiano wa wanawake waliopitia ukatili wa kingono uko juu zaidi kwenye Kanda za Magharibi (asilimia 22) and Ziwa asilimia (21). Kanda zilizo na kiwango cha chini kabisa ni Zanzibar (asilimia 9) na Kanda ya Kaskazini (asilimia 11). Kiwango cha ukatili wa kijinsia hususani uko juu miongoni mwa wanawake wanaofanya biashara ya ngono, ambao kati yao asilimia 51.7 waliripoti vitendo vibaya vya kingono na kimwili, ikiwemo kubwaka.46 Wakatili wa ukatili wa kingono mara nyingi ni watu ambao mwanamke anakuwa na mahusiano ya karibu nao. Asilimia arobaini na nane (48%) ya ukatili wa kijinsia ulitokea mikononi mwa mume/mwenza wa sasa au wa hivi karibuni, wakati katika asilimia 40 (40%) ya mashauri yaliyoripotiwa mkatili alikuwa ni mume/mwenza wa zamani. Asilimia arobaini na mbili (42%) ya wanawake ambao hawajahi kuolewa waliripoti kwamba wakatili wa ukatili wa kingono walikuwa wachumba wa sasa au wa zamani. Asilimia thelathini na moja (31%) waliripoti marafiki/watu waliowazoea kuwa wakatili, wakati asilimia saba (7%) waliripoti wageni kuwa wakatili. Utafiti wa TAWLA katika mwaka 2018 ulifichua kwamba vitendo vya ukatili wa kingono miongoni mwa wanawake waliolewa vinaongezeka wakati wanawake wakiripoti kwamba wenza wao wanawalamisha katika ngono kwa njia ya haja kubwa. Ripoti za kubakwa kwenye ndoa zilibainishwa kwa wingi katika mikoa ya Singida, Tabora, Iringa, Arusha, na Kilimanjaro, lakini wanawake pia wanaogopa kuripoti kwa sababu wanaona aibu au wanaogopa kisasi na waume zao.47 43 Ibid, 84. 44 TDHS-MIS 2015-116, page 369. 45 p. 369 46 Ukatili wa Kijinsia na Ukatili dhidi ya Watoto: Mwongozo wa Huduma ya Afya kwa Watoa Huduma ya Afya na Maafisa Ustawi wa Jamii, Julai 2017, uk 21. 47 Ibid, 162. 25 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania 3.1.6 Desturi za Ziada za Kitamaduni zenye Madhara Sherehe nyingi za kitamaduni na unyago zinahusishwa na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana nchini Tanzania. Wakati wa ngoma za vigodoro, kwa mfano, wasichana wadogo wanatakiwa kuvua nguo kidogo na kuwaruhusu wanaume wawashike wakati wakicheza ngoma za kitamaduni. Ubakaji pia hutokea sana wakati wa ngoma hizi. Katika Mkoa wa Shinyanga, wakati wa sherehe za mavuno bukwilima, wasichana hulazimishwa kuchagua miongoni mwa wanaume wanaostahiki wa kufanya nao ngono kupitia sherehe inayojulikana kama chagulaga na wanaweza kukabiliwa na ukatili wa kimwili au kingono kama watakataa. Desturi nyingine ya kitamaduni yenye madhara iliyoenea ni samba ambayo wasichana hupelekwa kwa mganga wa kienyeji kuwatayarisha kwa ndoa kwa kutumia dawa za kienyeji. Baada ya sherehe hizi, msichana lazima akubali ombi lolote la ndoa analopewa, ama sivyo anahatarisha kutokea kwa aibu na mkosi kwa familia yake.48 Wakati sherehe nyingi za unyago zilitokana na kuwa njia ya kuwatayarisha wasichana kwa FGM na/au ndoa, hizi zimekuwa zinasababisha desturi mbaya zenye madhara ya dhahiri, na mara nyingi zinaendelea kuenea hata kwenye jamii zilizo na viwango vidogo vya FGM na ndoa za utotoni.49 Mfano mmoja wa desturi hii inayofanyika kwa aina tofauti tofauti nchini Tanzania ni unyago, ambayo kwa kawaida huhusisha kuwaweka ndani vigoli kwa muda wa wiki kadhaa wakati wakiwazimisha kula ili waongeze uzito (kwa vile wanawake wanene wanavutia zaidi kingono kuliko wasichana wembamba) na kuwafundisha “jinsi ya kuwamudu wanaume kingono” Baada ya hapo jamii hufanya sherehe kubwa ambapo wasichana wanaruhusiwa nje kwa mara ya kwanza na kuwasilishwa kwa wachumba watarajiwa. Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi, na Mtwara ni maarufu sana kwa sherehe hizi za unyago.50 Wakishaolewa, wanawake wanaweza kukabiliwa na desturi ya kurithi wajane au kusafishwa baada ya kufiwa na waume zao. Kurithi wajane kunahitaji kwamba mwanamke aolewe na shemeji yake kwa marehemu mumewe, ili aendelee kubaki na watoto wake. Vinginevyo, atatakiwa kupitia utakasaji ambapo atafanya tendo la ngono na ndugu au jamaa wa marehemu, ili kumtakasa na mizimu yake.51 Desturi hizi hupatikana zaidi katika mikoa ya Mbeya na Mara. Mwanamke aliyeolewa anaweza kumuoa msichana awe mume “mzimu”. Msichana atazingatia taratibu zote zinazoambatana na ndoa na kuishi na mwanamke huyo aliyempita umri, kama mume na mke. Hata hivyo, hakuna mahusiano ya kingono baina ya wanawake hao wawili, na msichana mara nyingi atalazimishwa kufanya ngono na mumewe mwanaume na kuzaa watoto kwa wenza hao.52 48 Ibid. 49 Utafiti wa Taifa kuhusu Vichocheo na Matokeo ya Ndoa za Utotoni nchini Tanzania, Februari 2017, uk. 51. 50 Ibid, 52. 51 Chama cha Majaji Wanawake Tanzania. (2011). “Kusimamisha, Kuaibisha, na Kuwataja Wahusika wa Matumizi mabaya ya Madaraka kwa Utumwa wa Kingono,” p. 29. https://studyres.com/doc/17729874/tanzania-women-judges-association-s- country-report 52 Norah Hashim Msuya. (2017). “Desturi za Kimila na Kitamaduni zilizo na Madhara: Kikwazo katika Utekelezaji wa Mkataba kuhusu Kutokomeza Ubaguzi dhidi ya Wanawake, na Itifaki ya Maputo kuhusu Haki za Wanawake nchini Tanzania.” PhD Thesis, pp.148-9. https://researchspace.ukzn.ac.za/xmlui/bitstream/handle/10413/14989/Msuya_ Norah_H_2017. pdf?sequence=1&isAllowed=y. 26 Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia 3.1.7. Tabia za Kutafuta Msaada Miongoni mwa Wahanga wa GBV Mara nyingi GBV inaripotiwa kwa uchache. Kulingana na Utafiti wa TDHS-MIS 2015-2016, ni asikimia 54 tu ya wanawake waliopitia ukatili wa kimwili au kingono walitafuta msaada. Kati ya wale waliotafuta msaada, wanawake wengi waliwageukia wanafamilia, wakiwa na asilimia 9 tu walitafuta msaada kutoka Polisi.53 TUtafiti wa VAC wa mwaka 2009, pia uligundua kwamba takribani nusu ya wanawake waliopitia ukatili wa kingono wakiwa wadogo hawakuripoti madhila yao kwa mtu yeyote. Takribani msichana 1 kati ya kila 5 alitafuta huduma kwa madhila yao ya ukatili wa kingono, pakiwa na takribanj mwanamke 1 kati wa 8 wakipata huduma hizo kwa madhila waliyopitia ya ukatili wa kijinsia kabla ya umri wa miaka 18.54 Mwelekeo wa kutafuta msaada kwa ajili ya ukatili wa kingono visiwani Zanzibar unafanana na ule wa Tanzania Bara kwa ujumla.55 Wahanga wanaoripoti madhila yao wako katika hatari ya “kubezwa” kwani jamii huchukulia ukatili wa kingono na IPV kama masuala binafsi.56 Mahojiano na mashirika yanayofanya kazi kwenye usawa wa kijinsia na haki yamethibitisha kwamba mahali pa kwanza kwa wahanga kutafuta msaada mara nyingi ni familia. Katika matukio ya ukatili wa mwenza wa karibu, “hii itahusisha mikutano ya familia baina ya wazazi wa wenza na wazee wengine ambao watasuluhisha na kutoa mstari wa kwanza wa suluhu.”57 Hata hivyo, idadi ya wanawake waliopita vyote, ukatili wa kimwili na kingono waliotafuta msaada iliongezeka kwa takriba ni asilimia 20 kutoka Utafiti wa DHS wa 2010 hadi 2015/2016. Asilimia sitini na nne (64%) ya wanawake waliopitia ukatili wa kimwili na kingono waliripoti kutafuta msaada ukulinganisha na asilimia 53% ya wale waliopitia ukatili wa kimwili pekee, na asilimia 29% kwa wale waliopitia ukatili wa kingono pekee58. Kimkoa, tabia ya kutafuta msaada inonekana kwa wingi Mikoa ya Iringa (asilimia 72) na Morogoro (asilimia 70). Kutafuta msaada kuko juu kwa pia wanawake ambao huko nyuma waliolewa au waliopo kwenye ndoa kwa sasa, wanawake wenye watoto wengi, na wanawake walioajiriwa kwa mshahara.59 3.2 Vikundi Ambavyo Mahususi Viko Hatarini na GBV Bila kujali umri au hadhi ya kijamii au kiuchumi, wanawake na wasichana nchini Tanzania wanaweza kukabiliwa na GBV maisha yao yote, lakini baadhi ya makundi yapo katika hatari zaidi kiuwiano kwa sababu ya masuala mengi mtambuka ambayo ni pamoja na: umasikini, ujinga, mwelekeo wa kingono, utambulisho kijinsia, umri, au ulemavu, miongoni mwa visababishi vingine. Kuna data chache kuhusu vikundi hivi mahususi nchini Tanzania. Hata hivyo, sehemu zifuatazo zitaangazia baadhi ya changamoto mahususi na aina za GBV zinazovikabili vikundi hivi. Aina ya ukatili wa nguvu ulioibuka unaowalenga wanawake wazee na wajane aumeshuhudiwa na unaongezeka. Tangu mwaka 2016, kikundi cha wabakaji Mkoani Kigoma maarufu wanajulikana kama TELEZA huvunja nyumba za watu na kuwabaka kikatili mfululizo wanawake wazee na wajane, na wengi wa wahanga hao kushindwa kuripoti.60 Ujumbe wa kuchunguza 53 TDHS-MIS 2015-2016, page 367. 54 Ukatili dhidi ya Watoto nchini Tanzania: Matokeo kutoka Utafiti wa Taifa 2009, uk 27. 55 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2011, Ukatili dhidi ya Watoto nchini Tanzania: Matokeo ya Utafiti wa Kitaifa 2009, uk10 56 Mahojiano ya Mtoa Habari muhimu. 57 Mtoa Habari muhimu, LHRC. 58 TDHS-MIS 2015-16, p. 398. 59 Ibid. 60 Diana Rubanguka, “Kundi la wabakaji laibuka Kigoma” 25,Mei 2016 na Fadhili Abdallah “ Teleza azidi kuchafua hali ya hewa Kigoma.” Teleza azidi kuchafua hali ya hewa Kigoma.” 27 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania ukweli wa mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali (LHRC na Twaweza) yalifichua mazingira ya kutisha kama vile kubakwa kwa mwanamke aliyerudi nyumbani usiku kutoka kuchota maji, kubakwa mfululizo kwa mwanamke wa miaka 60 baada ya kupigwa na nondo, na kubakwa kwa mwanamke mwenye mimba ya miezi nane.61 Wasichana balehe na wanawake vijana wanaweza kuwa katika hatari mahususi ya kunyanyaswa na kushambuliwa kingono. Ushahidi kutoka kwenye utafiti wa Unyanyasaji Kingono na GBV kwenye usafiri wa umma umegundua kwamba wanawake kati ya miaka 18 na 25, walikuwa asilimia 22 zaidi wa uwezekano wa kukabiliwa na unyanyasaji au ukatili kuliko wanawake wazee.62 Kama ilivyoonekana hapo juu, wasichana balehe pia wapo katika hatari ya desturi za kitamaduni zenye madhara, kama vile bukwilima au samba. Wanawake na wasichana walemavu wana uwezekano zaidi wa kukabiliwa na viwango vikubwa vya GBV kutokana na kunyanyapaliwa na jamii na hali hatarishi. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu lnaeleza kwamba ulemavu unanyanyapaliwa zaidi nchini Tanzania, na kufanya iwe vigumu sana kukusanya data sahihi juu ya kuenea kwa GBV miongoni mwa watu hawa.63 Data za ziada zinahitajika ili kuelewa vizuri kuenea kwa GBV miongoni mwa makundi mengine yaliyo kwenye hatari nchini Tanzania, hii inajumuisha wasagaji, wasenge, na wanawake wenye jinsi zote, makahaba, wanawake waliotalakiwa na wajane. 3.3 GBV na UVIKO-19 Serikali ya Tanzania imechukua mbinu ambayo ni tofauti sana kwenye janga la KOVID 19 kuliko nchi nyingine jirani. Data kuhusu matokeo ya mbinu hii – na matokeo ya KOVID 19 kwa upana zaidi – kuhusu kuenea kwa GBV, ni kidogo sana. Tukio la kwanza la KOVID-19 nchini lilitokea Machi 16, 2020. Hata hivyo, ilipofika Mei 2020, Serikali iliacha kutangaza data za KOVID – 19, na aliyekuwa Rais John Magufuli alitamka kwamba Tanzania “Haina KOVID – 19” mnamo Juni, 2020. Baada ya kifo cha Rais Magufuli mnamo Machi, 2021, mwelekeo wa nchi kuhusu KOVID – 19 ulibadilika, na Serikali mpya inayoongozwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan tangu hapo alikubali hadharan uwepo wa virusi nchini Tanzania na kutekeleza mpango wa mwitikio mpya. 64 Uchambuzi wa haraka wa Jinsia uliofanywa na CARE mnamo Aprili 2020 uligundua kwamba wengi wahojiwa wanawake katika Afrika Mashariki, Kati na Kusini waliripoti kwamba kuongezeka kwa GBV na unyanyasaji na kupungua kwa rasilimali pamoja na kufanya maamuzi wakati wa janga la UVIKO-19.65 TMatokeo haya yanaungwa mkono na ushahidi wa kidunia kuhusu athari za janga kwenye viwango vya GBV na matokeo ya visa kutoka kwenye mashirika yanayoongozwa na wanawake nchini Tanzania, pamoja na Stella Nziku, kiongozi wa Mtandao wa Wanawake Mufindi. Akizungumza na Shirika la Umoja wa Mataifa, UN Women, Nziku alitamka, 61 Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (Bara) Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (Zanzibar), Ripoti ya Haki za Binadam: Ukatili wa Kingono: Tishio kwa Haki na Ustawi wa Mtoto nchini Tanzania, uk 162. 62 Taasisi za Benki ya Dunia: “Kuelewa na Kushughulikia Ukatili wa Kijinsia kwenye Usafiri wa Umma, kwa Makundi yaliyo Hatarishi zaidi katika Dar es Salaam.” https://thedocs.worldbank.org/en/doc/179331603898899363-0050022020/ original/15653WBDIMEPolicyBriefTRATanzaniaGBV.pdf. 63 OHCHR. “Ulemevu na Ukatili wa Kijinsia Tanzania.” https://www.ohchr.org/documents/issues/women/wrgs/ girlsanddisability/governments/tanzania.doc. 64 CARE International. Tanzania UVIKO-19 Ripoti ya Mwitikio kwa ajili ya Ufadhili wa Bloomberg, uk. 3. https://reliefweb.int/ sites/ reliefweb.int/files/resources/Tanzania-COVID-19-Bloomberg-Report-Final.pdf. 65 Mahuku, E, Yihun, K.L., Deering, K, & Molosani, B. (2020). CARE: Uchambuzi wa haraka wa Jinsia kuhusu UVIKO 19 Afrika Mashariki, Kati, na Kusini. CARE International: https://careevaluations.org/wp-content/uploads/ECSA-RGA-_- FINAL-30042020. pdf. 28 Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia “Nilifahamu kwamba gharama za Afua ambazo hazizingatii Jinsia ambazo zinawatenga wanawake zitakuwa juu sana…. Baada ya kifo cha mume wangu, nilikuwa muhanga wa Ukatili wa kisaikolojia na kiuchumi wakati baadhi ya ndugu walipora mali zetu zote. Kwa sababu ya uzoefu wangu mgumu, sikupenda kuona wanawake na wasichana wakipitia hali hii ngumu ya maumivu ya kisaikolojia, kutokana na athari za janga la UVIKO-19.”66 Kufungwa kwa Shule nchini Tanzania kumewaweka wasichana balehe katika hatari kubwa ya GBV, pamoja na ndoa za Utotoni na ukatili wa kingono. Ubalozi wa Ireland nchini Tanzania uliripoti kuongezeka kwa viwango vya mimba za utotoni wakati wa janga na kuonyesha wasiwasi wake kuhusu Sera za Serikali ambazo zinazuia upatikanaji wa Elimu kwa wasichana waliopata mimba na akina mama vijana.67 Kwa sababu ya hili na mambo mengine ya utetezi, mnamo Novemba 2021, Serikali ya Tanzania ilitamka juhudi mpya za kupanua upatikanaji wa Elimu kwa makundi haya, iliyowakilisha hatua muhimu na mwitikio kwa athari za UVIKO-1968. 66 UN Women. (2020). “Wanawake wanachukua Uongozi katika Mapambano dhidi ya GBV wakati wa Janga la UVIKO -19 nchini Tanzania.” https://africa.unwomen.org/en/ news-and-events/stories/2020/09/women-take-a-lead-to-fight-gbv- during-covid19-in-tanzania. 67 Ubalozi wa Ireland, Tanzania. (2020). “Mwitikio kwa UVIKO-19, na Kukosa Usawa wa Kijinsia kupitia Redio za Jamii.” https:// www.dfa.ie/irish-embassy/tanzania/news-and-events/latestnews/responding-to-covid-19-and-genderinequalities- through-community-radio.html 68 “Maelezo ya Benki ya Dunia kuhusu Tangazo la Serikali ya Tanzania kuhusu Upatikanaji Sawa wa Elimu kwa Wasichana Wajawazito na Wamama Vijana.” (2021) https://www.worldbank.org/en/news/statement/2021/11/24/world-bank- statementon-the-announcement-by-government-of-tanzania-on-equal-access-to-education-for-pregnant-girls-and-y 29 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania 4. Mazingira ya Kisheria na Sera za Kushughulikia GBV Mwitikio wa Kitaifa kwa GBV nchini Tanzania umejikita katika Mifumo Muhimu ya Maendeleo katika Sheria na Sera ambazo zinaonyesha maboresho ya ahadi kwa haki na ulinzi wa wanawake na wasichana katika kipindi cha miaka 20 iliyopita. 4.1 Mazingira ya Kisheria 4.1.1 Sheria Muhimu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) na Katiba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (1994) kwa uwazi kabisa zinakataza ubaguzi kwa misingi ya Jinsia na kutoa usawa wa Kijinsia.69 Muswada wa Haki na Wajibu uliotamkwa kwenye Katiba unasisitiza uhuru wa Mtu, usawa na haki. Ibara 12 (1) inahakikisha usawa wa watu wote, ikitamka kwamba “wanadamu wote wamezaliwa wakiwa huru na wote wako sawa.” Katiba inasisitiza kanuni za kutokubagua na usawa kupitia Ibara 13 ambayo inatamka katika kifungu kidogo 1 kwamba “watu wote wako sawa mbele ya Sheria na wana haki, bila ubaguzi wowote kwa ulinzi na usawa mbele ya Sheria.” Ibara 29 (1) inaakisi haki ya ulinzi sawa, na kutamkwa kwamba “kila mtu ndani ya Jamhuri ya Muungano ana haki ya kufurahia haki za msingi za Binadamu na kufurahia matunda yanayotokana na Kuridhika kwa kila mtu kwa wajibu huu kwa jamii.” Miundombinu ya Kisheria na Kisera ambayo inaitikia kwa GBV inapatikana katika baadhi ya Sheria Mahususi ambazo zinajumuisha: Sheria ya Mtoto, Sheria ya Ndoa, Sheria ya kuzuia Usafirishaji wa Watu, Sheria ya Adhabu, Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi, Sheria ya Elimu, Amri ya Azimio la Sheria za Kimila ya Mwaka 1963, Sheria ya VVU na UKIMWI (Kuzuia na Kudhibiti), Sheria ya Ardhi, Sheria ya Mirathi ya India, Sheria ya Mirathi, Sheria ya Haki kwa Watu Wenye Ulemavu, na Sheria ya Ardhi ya Kijiji. Sheria hizi zimeandikwa kwa Muhtasari katika Kiambatisho 3.70 Sheria ya Adhabu (iliyopitiwa 2002) imefanya ma kosa mbalimbali ya GBV kuwa Jinai kupitia Marekebisho ya Sheria mbalimbali ya Mwaka 1998, pia inajulikana kama Sheria ya Sheria Maalumu ya Makosa ya Kingono (SOSPA). SOSPA imeongeza adhabu za Kijinsia kwa Ukatili wa Kijinsia na kufanya iwe haramu, Jinai za kusafirisha watu, unyanyasaji wa Kingono, na Ukeketaji. Sheria ya Adhabu 7/2018 kifungu 151 (1) kinazuia mtu yeyote aliyetuhumiwa kwa makosa ya kingono asipate dhamana na pia kimeongeza adhabu. Matokeo yake, Mahakam za Mkoa zinaweza kutoa hukumu ya miaka 7 hadi 14, wakati hukumu kutoka Mahakama Kuu zinaanzia miaka 30 hadi kifungo cha maisha. Marekebisho ya Sheria ya Msaada wa Kisheria, 2017 imetoa mfumo kwa ajili ya utekelezaji wa upatikanaji wa haki kwa wote, pamoja na masikini na wanawake na wasichana walio katika mazingira magumu. Sheria hii imeundwa ili kuratibu utoaji wa huduma za msaada wa Kisheria kwa watu masikini na imeanzisha Daftari la watoa huduma za Msaada wa Kisheria, washauri wa Kisheria, ambao hutoa msaada wa kisheria bure katika nchi nzima. Sheria ya Ndoa (LMA), 1971 inapiga marufuku kupiga Mke/Mume katika Kifungu 66 ambacho kinatamka, “ili kuepuka mashaka, hapa inaazimiwa kwamba, bila ya kujali mila ya aina yeyote, 69 Ibara 12 hadi 24, Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. 70 Tanzania pia ni Mtia Saini wa Mikataba mbalimbali ya Kimataifa na Kikanda ambayo inaendeleza dhamila zake za kushughulikia GBV, imewekwa kwa muhtasari katika kiamabatisho 4. 30 Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia hakuna mtu aliye na haki ya kumusababishia adhabu ya viboko kwa Mke/Mume wake.” Hata hivyo, Sheria ya Ndoa inaruhusu Mitala chini ya Desturi za Kimila, Kiisilamu na Kiraia.71 Kulingana na Sheria hii, kuna aina mbili za ndoa: Ndoa ya Mke/ Mume mmoja na Mitala. Ndoa za Kiisilamu na Kimila zinachukuliwa kuwa ni ndoa za Mitala au zinaweza kuwa za mitala, wakati Ndoa za Kikristu zinachukuliwa kuwa za Mke/Mume mmoja. Kuanzia mwaka 2019, umri wa chini Kisheria wa Ndoa ni miaka 18 kwa wavulana na wasichana, wakati Mahakama ya Rufaa ilipokazia hukumu ya Mahakama Kuu ambayo iliongeza umri wa chini wa ndoa kwa msichana na mvulana kuanzia miaka 14 na 15 mtawalia.72 Marekebisho ya Sheria ya Elimu 2016 pia imepiga marufuku ndoa za utotoni kwa kutamka wazi kabisa katika Kifungu 60 (1) kwamba ni kinyume cha Sheria chini ya mazingira yeyote yale kwa a) mtu yeyote kumuoa msichana au kuolewa na mvulana wa shule ya msingi au sekondari b) mvulana wa shule ya msingi au sekondari kumuoa mtu yeyote yule. 4.1.2 Mapungufu na Fursa Muhimu kwenye Sheria Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inanufaika kwa sehemu kubwa na mazingira wezeshi yanayo weza kuwezesha kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Hata hivyo, tathmini imegundua mapungufu kadhaa muhimu katika Sheria za ulinzi kuhusiana na GBV, pamoja na: Kushindwa kwa ufafanuzi wa Kikatiba wa Ubaguzi kujumuisha upigaji marufuku thabiti wa ubaguzi wa moja kwa moja na usio kuwa wa moja kwa moja dhidi ya wanawake kwenye maeneo ya hadharani na faragha;73 Kuendelea uwepo wa Sheria za Kibaguzi kama vile Sheria ya Kimila ya Mirathi, (Amri ya Sheria ya Kimila ya 1963); Uwepo wa aina mbali mbali za kibaguzi na vikwazo wanavyokabiliana navyo wanawake katika ukahaba; na Kukosekana kwa kupiga marufuku kwa ubakaji kwenye ndoa na ukatili wa majumbani chini ya Sheria za Jinai na Madai za Tanzania Bara au Zanzibar. Kukosekana kwa Sheria ya Mahakama ya Kadhi ya mwaka 1985 inayotoa matunzo ya talaka wakati wa kipindi cha “edda” au wakati wa mgawanyo wa mali za wanandoa. Aidha, kutekelezwa kwa Sheria kunaendelea kuwa Changamoto kwa sababu ya: Uchunguzi dhaifu, Ushahidi usiotosheleza, Desturi za kimila dhidi ya kuripoti matukio, Ucheleweshaji katika mfumo wa Mahakama, kukosekana mafunzo kwa Maafisa wanaotekeleza Sheria, gharama kubwa za Mahakama, na rushwa miongoni mwa Polisi na Mahakama, kama itakavyo jadiliwa baadaye hapo chini katika mapitio ya Programu. 71 Mfumo wa Kisheria wa Tanzania unazingatia mambo mengi. Hii inamaanisha kwamba kuna Mifumo kadhaa ya Kisheria inayofanya kazi kwenye eneo moja la Utawala. Hivyo basi, kuna Sheria ya Kimila ambayo imeainishwa katika Amri ya Azimio la Sheria ya Kimila (CIDO) 1963, Sheria za Kiisilam, na Sheria ya Serikali. 72 Hadi hivi karibuni, LMA ililuhusu ndoa za Utotoni kwa Wasichana wakiwa na Umri mdogo wa miaka 14 au zaidi, lakini kukiwa na ridhaa ya mzazi. Mnamo mwaka 2019, Kesi ya Masilahi ya Umma ilifunguliwa mwaka 2016 amabako Mahakama Kuu ya Tanzania ilipinga uhalali wa Kikatiba wa Ndoa za Utotoni nchini Tanzania, na kudai Serikali iwape ulinzi sawa Wasichana chini ya Sheria. Mahakama Kuu iliamuru kwamba Ndoa chini ya umri wa miaka 18 ilikuwa haramu na kuelekeza kwamba Serikali iongeze umri wa chini hadi miaka 18 kwa wote Wavulana na Wasichana ndani ya Mwaka mmoja. Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikata Rufaa dhidi ya Maamuzi haya. Rufaa ilizingatia kwamba madai hayo yanaonyesha utofauti wa umri wa chini ulikuwa ni muafaka wa kimaadili ili kuweza kubeba maamuzi ya Kimila, Kitamaduni na Kidini kuhusu Ndoa. 73 Kama ilivyoonekena na Kamati ya Ubaguzi dhidi ya Wanawake (CEDAW) katika kikao chake cha 63, Aya ya 8, Kamati ya CEDAW ilihitimisha kilichoonekana kwenye Ripoti za pamoja za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. 31 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania 4.2 Mazingira ya Sera 4.2.1 Sera Muhimu Ahadi za Kitaifa za kushughulikia GBV zimetamkwa katika Mpango Kazi wa Taifa “Kubadilisha desturi za kijinsia zinazo- wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake husiana na wanaume kuwa na na Watoto Nchini Tanzania 2017/18 – haki juu ya miili ya wasichan na 2021/22 na Mpango kazi wa Kutokomeza wanawake na udhibiti wa tabia Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto zao ni mkakati muhimu sana wa kupata usawa wa Kijinsia, ku- Zanzibar 2017-2022. Zinatoa mfumo wa punguza ukatili, kuunda matunzo Sera wa jumla kwa kuzuia na kuitikia GBV na mahususi ya kuzuia na kushughu- (VAC) nchini Tanzania. likia mahitaji ya msaada.” NPA hizi zimetayarishwa na kuendana na - Nadharia ya Mabadiliko, Zanzibar Sera na Juhudi za Serikali kuhusiana na NPA 2017-2022 usawa wa Kijinsia, kukuza na kulinda haki za wanawake. Upeo wa Sera na Mwongozo wa Kitaifa unawezesha utekelezaji wa kimkakati wa NPAs. Zinajumuisha pamoja na vingine: Sera ya Jinsia Zanzibar (2016) na Mpango wa Utekelezaji Sera ya Elimu na Mafunzo (2014) ambayo inataka pawepo na upatikanaji sawa na Fursa kwa Elimu na Mafunzo kwa wavulana na wasichana. Sera ya Elimu Zanzibar ya mwaka 2006 ambayo inasisitiza upatikanaji na Fursa. Sera ya Hifadhi ya Jamii kwa Tanzania Bara; Sera ya Taifa ya Afya (2017) Sera ya Biashara Ndogondogo na za Kati (2006) Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia (2000) kwa ajili ya Tanzania Bara, na Mkakati wake wa Utekelezaji (2005); na Sera ya Taifa ya Nishati kwa Tanzania Bara (2015) Sera ya Hifadhi ya Jamiii Zanzibar (2014) Sera ya Maendeleo ya Ushirika Zanzibar (2014) Sera ya Elim una Mafunzo (2014) Mkakati wa Taifa kuhusu Elimu Jumuishi (2009-2017) Kamati ya Taifa ya Ukatili wa Kijinsia (Zanzibar) na Mwongozo wa Ukatili dhidi ya Watoto na Ukatili wa Kijinsia (2014-2016) Mkakati wa Kitaifa wa Kurasimisha Ulemavu (2010-2015); na Sera ya Ulemavu (Zanzibar, 2010). Sera ya Afya Mahali pa Kazi Zanzibar (2017). NPA za sasa pia hujenga juu ya kazi zilizopita za VAC na VAW, pamoja na Utafiti wa VAC wa mwaka 2009, na Mpango Kazi wa Sekta nyingi uliofuatia wa miaka mitatu wa Hatua za Kuzuia na Kuitikia kwa Ukatili dhidi ya Watoto (2013-2016), pia na Mkakati wa Taifa wa Zanzibar wa mwaka 2011 wa Kuzuia na Kuitikia Ukatili wa Kijinsia.74 Kwa kuunganisha juhudi za VAC 74 Wizara ya Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto, Mpango kazi wa Kisekta wa kuitikia ukatili dhidi ya Watoto 2011-15, 2011; na Wizara ya Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto, Mkakati na 32 Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia na VAW, NPA ilitamka kwamba “kwa mara ya kwanza mfumo uliotuunganisha na jumuishi ambao unafafanua muingiliano wa wazi baina ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto wakati ikitambua mahitaji binafsi mahususi ya waathirika.”75 Baadhi ya muingiliano huo ulioonekana katika NPA ni pamoja na: Visababishi vya hatari vilivyoshirikishwa katika ukatili dhidi ya wanawake na watoto kama vile vikwazo dhaifu vya kisheria dhidi ya ukatili, desturi za kijamii ambazo zinachochea kukosekana kwa usawa katika nyanja zote, ulinzi usiotosheleza wa haki za binadamu, pia na mwitikio dhaifu wa kitaasisi. Matokeo ya kawaida ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambao unaathiri afya ya kimwili, afya ya akili, na ufanyaji kazi kijamii. Desturi za kijamii ambazo hazikemei ukatili dhidi ya wanawake na watoto na kuzuia utafutaji wa msaada; na Kutokea kwa pamoja kwa ukatili dhidi ya wanawake na ukatili dhidi ya watoto katika kaya hiyo hiyo ambayo inarejea kwa kuwatendea vibaya watoto na mwenza wa karibu vikitokea kwenye kaya hiyo hiyo na muda huo huo.76 NPA pia ilitambua kwamba mara nyingi ni huduma hizo hizo ambazo huitikia kwa mahitaji ya watoto na wahanga watu wazima, na kuimarisha mipango ilikuwa ni fursa kimkakati ya kushughulikia kudurusu, mwiingiliano, na kukosa ufanisi. 77 Kwa pamoja NPA za Tanzania Bara na Zanzibar zimeipa kipaumbele kuwekeza katika kujenga mifumo ya kuzuia GBV na kuitikia mahitaji ya wahanga.78 Mbinu hii ya mifumo inahusisha kuileta pamoja miundo, kazi na uwezo katika sekta muhimu, pamoja na huduma za jamii, afya, sheria, usalama, na elimu kuanzia ngazi za kitaifa hadi maeneo husika.79 Utekelezaji pia umelenga kwenye kuimarisha ukusanyaji wa data na kuripoti, kujenga harakati, kuratibu na ushirikiano.80 Mbinu hizi na hatua zilizopendekezwa zinasisitizwa hapa chini, na kuelezewa kwa kina zaidi katika Kiambatisho 5. NPA pia zinasisitiza kanuni kadhaa muhimu zilizoungana na utekelezaji wa hatua zilizopendekezwa, ikiwa ni pamoja na kufika sehemu zote na fursa; usawa wa kijinsia; kujitegemea na uwezeshaji wa wanawake na wasichana; ushirikishwaji wa jamii na familia; kuendana na desturi za kimila; na kutambua mahitaji ya walewanaoishi katika mazingira hatarishi, pamoja na mengine.81 Mpango kazi wa kuzuia na kuitikia Ukatili wa Kijinsia Zanzibar, 2011. 75 Mpango kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Zanzibar, 2017-2022, p. 23. 76 Ibid, 24. 77 Ibid, 7. 78 Ibid, 9. 79 Ibid, 9. 80 Mpango Kazi wa Kitaifa Tanzania, ( NPA) unazungumzia mbinu za Utekelezaji zinazotumika kuendesha Mikakati (uk 12) na Zanzibar NPA unazungumzia Mwongozo wa kuelekeza Utekelezaji wa Mpango (uk 28). 81 Ibid. 33 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania Maeneo nane ya Utekelezaji wa NPA za Tanzania Matokeo matatu muhimu ya NPA za Zanzibar 1. Kuimarisha Kaya Kiuchumi 1. An enhanced enabling 1. Mazingira wezeshi yaliyokuzwa 2. Desturi na maadili 2. Muunganiko wa kuzuia na kuitikia; 3. Mazingira salama na 4. Kulea, msaada wa familia,na mahusiano 3. Huduma za msaada zinazojenga uwezo wa wanaume, wanawake, 5. Utekelezaji na kukazia Sheria watoto, familia na jamii.82 6. Shule salama na stadi za maisha 7. Huduma za mwitikio na msaada 8. Uratibu, ufuatiliaji, na tathimini. 4.2.2 Mapungufu na Fursa Muhimu kwenye Kwa ujumla, NPA ni jumuishi katika mbinu zao. Idadi kubwa ya mashauriano kabla ya kutayarisha NPA imepelekea kuwepo na maarifa mapana zaidi na kuelewa sababu za uwepo wa NPA. Mahojiano ya watoa habari muhimu yamethibitisha wadau wengi wana ufahamu wa vipaumbele vya NPA. Mhojiwa mmoja alitamka kwamba: “Wakati wa mashauriano mabishano mengi ya kuchangamsha kuhusu ni vipengele gani vitakubaliana na kila eneo la utekelezaji, kwa mfano watoto, wasiwasi wa ulemavu. Kwa kutumia modeli ya [WHO] INSPIRE, tuliweza kupata sababu za uchaguzi na kufikia muafaka wa maeneo nane ya utekelezaji. Watendaji katika nafasi hii walikuwa na uelewa imara wa mpango.”83 Hata hivyo, kwa sababu NPA zimeundwa kuzunguka maeneo ya kutekelezaji, hakuna sekta muhimu zilizo na usimamizi wa msingi wa vipengele tofauti vya NPA—hii inatofautiana na NPA-VAC. Cha kutambua, Wizara mama na wakala zimeelezewa katika nyaraka za gharama na zana za uendeshaji. Kwa upande mwingine, urasimishaji wa NPA kwenye Wizara umehimiza Wizara kujenga usikivu wao kwa GBV. Wahojiwa muhimu walizingatia kwamba kupitia watu wanaolenga jinsia katika Wizara mbalimbali, kuna dhifa za kitaifa ambazo, zinaratibiwa kwa pamoja kama vile Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Siku 16 za Harakati za Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake. Hata hivyo, Wizara na wakala hizo ambazo hazina wataalamu wa ulinzi wa watoto na jinsia, utekelezaji ni xhangamoto inayoendelea. 82 Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi Wanawake na Watoto Zanzibar, 2017-2022, uk. 34. 83 Mahojiano ya Mtoa Habari Muhimu WILDAF. 34 Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia Kielelezo 4: Gharama za NPA Zilizopendekezwa za Maeneo 8 ya Utekelezaji 2017-2021 Changamoto za utekelezaji zinafanywa kuwa mbaya zaidi na mapungufu makubwa ya fedha. NPA za Tanzania zilikuwa na gharama takribani Shilingi ya Tanzania bilioni 267.4 katika kipindi cha miaka mitano (5), kukiwa na matarajio kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara kadhaa zitatenga sehemu za bajeti zao kwa ahadi mahususi za NPA. Mapitio ya bajeti kwa mwaka 2017/2018 yalidhihirisha kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu haikuzipa kipaumbele NPA za Tanzania kupata fedha. MoHCDGEC haina mamlaka ya kuzifanya Wizara nyingine ziwajibike kama hazikutenga mafungu kwa ajili ya utekelezaji wa NPA. Uwezo dhaifu wa kitaasisi na miundombinu michache za kujikita na kutekeleza kikamilifu NPAs ni changamoto inayoendelea. Mapungufu ya rasilimali watu na fedha yalianishwa wakati wa mahojiano na watoa habari muhimu katika ngazi ya Serikali pia miongoni mwa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali. Sehemu kubwa ya fedha ya kufanyia Programu za GBV zimewezeshwa na Wabia wa Maendeleo. Hili sio jambo endelevu. Aidha, bajeti iliyopendekezwa imewekeza zaidi katika mabadiliko ya desturi za kijamii na uimarishaji wa kiuchumi wa kaya ukilinganisha na afua nyingine. Wakati utengaji huu wa fedha ni utambulisho unaokaribishwa wa umuhimu wa Programu za kuzuia, bado kuna haja ya kuhakikisha matumizi ya mwitikio na kuzuia GBV vyote kwa pamoja, kwa kutumia mbinu zinazotokana na ushahidi ili kuhakikisha matokeo ya juu kabisa.. 35 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania Kisanduku 1: Kisa Mkasa wa Utendaji Bora kuhusu Kuongezea Nguvu NPA: Mpango wa Mkoa wa Shinyanga Kumaliza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto84 Mkoa wa Shinyanga unawasilisha simulizi ya mafanikio kama Mkoa pekee nchini Tanzania ambao umeongezea nguvu NPA za Tanzania kwa kutayarisha Mpango wake mwenyewe wa Mkoa unaoitikia muktadha wake. Manufaa ya kuongezea nguvu ni pamoja na kuimarisha umiliki wa Mpango, uainishaji wa changamoto ambazo ni mahususi kwa muktadha husika, na kuendeleza afua za kuzuia na kuitikia GBV na VAC ambazo ni za kwetu wenyewe, pia na kutoa fursa ya utekelezahi wa haraka wa afua zilizolengwa za kumaliza GBV na VAC. Mpango unazingatia desturi za kitamaduni zenye madhara, maadili, na desturi ambazo bado zipo na zimechangia kwenye kuongezeka kwa baadhi ya aina za GBV katika Mkoa wa Shinyanga. Desturi hizi za kijamii na utendaji vimeendeleza mahusiano yasiyo sawa kwa misingi ya jinsia, kuwafanya wanawake na watoto kuwa katika mazingira hatarishi zaidi kwa ukatili wa kimwili, kingono na kisaikolojia kwenye nyumba zao na katika jamii zao. Mpango pia unazingatia kwamba sherehe za kitamaduni kama vile bukwilima na samba zinachangia kwa GBV. Kutokana na desturi za kitamaduni zenye madhara, Shinyanga ni mojawapo ya mikoa inayoongoza kwa ndoa za utotoni. Kufuatia kupitishwa kwa Mpango wa Mkoa, shughuli kadhaa zilifanyika kushughulikia matatizo ambayo ni mahususi kwa muktadha. Hizi zinajumuisha: Midahalo ya Jamii, mafunzo na afua za vyombo vya habari vinavyowalenga wanaume, viongozi wa dini, na viongozi wa kimila ilifanyika ili kuwahisisha kwenye mitazamo ya ukatili dhidi ya wanawake kuhusiana na desturi zenye madhara, na athari za desturi za kimila zinazowezesha ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Sheria ndogo kuanzia ngazi ya Mkoa hadi kata zilipitishwa ili kuhakikisha ufanyaji kazi wa mwitikio kuelekea desturi za kitamaduni zenye madhara na masuala yanayo shahibiana. Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ilitayarisha Mradi wa kuzuia ukatili sokoni ambao umetekelezwa katika masoko matano (Ngokolo, Ibinzamata, Kambarage, Mjini, na Lubaga) kwa lengo la kushughulikia ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika maeneo ya umma; na Juhudi za kuamsha ufahamu kuhusu kuzuia na mwitikio kwa GBV na VAC unaofanyika kupitia matumizi ya majukwaa ya umma ili kujenga ufahamu kuhusu masuala ya ukatili ambayo hutokea hadharani na maeneo ya faragha. 84 Mpango Mkakati wa Mkoa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto mkoani Shinyanga 2020/2021- 2024/2025. 36 Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia 5. Mifumo na Taratibu za Uratibu wa GBV Sura hii inaainisha mifumo muhimu inayowajibika kushughulikia GBV ncnini Tanzania uliotayarishwa katika ngazi ya kitaifa na kutumwa katika eneo husika kama ilivyoelekezwa ndani ya NPAs kwa Tanzania Bara na Zanzibar. 5.1 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 5.1.1 Mifumo ya Kitaifa Tanzania NPA ya Tanzania inahusisha sekta nyingi na ni mtambuka, na imepangwa katika ngazi ya taifa na eneo husika kama inavyoonyeshwa katika Kielelezo 5. NPA ya Tanzania inaanzisha Kamati Elekezi ya Kitaifa ya Ulinzi, Kamati ya Ufundi ya Kitaifa ya Ulinzi, na Vikundi Kazi vya Maeneo ya Utekelezaji ili kuwezesha uratibu wa mwitikio na kuzuia GBV. Kielelezo 5: Uratibu wa GBV chini ya NPA Tanzania Kamati Elekezi ya Kitaifa ya Ulinzi (NPSC) Mwenyekiti wake ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (PMO) na Sekretariati iko chini ya MoHCDGEC. NPSC inatoa Mwongozo wa Sera na uratibu wa NPA. Kamati hukutana mara mbili kwa mwaka ili kuhakikisha utiifu wa kitaifa kwa wajibu wa kimataifa, kurasimishwa kwa NPA, na rasilimali fedha za kutosha. Inawajibika katika kufanya mapitio na kuidhinisha mipango kazi ya mwaka na kutoa Mwongozo wa Sera kuhusu utekelezaji.85 Hadi sasa uwajibikaji upo katika Ofisi ya Waziri Mkuu, hii inamaanisha kuhakikisha ngazi ya juu kabisa ya utashi wa kisiasa, usimamizi, na ufanisi katika uratibu. . Kamati ya Ufundi ya Kitaifa ya Ulinzi (NPTC) Mwenyekiti wake ni Katibu Mkuu wa MoHCDGEC na hukutana mara nne kwa mwaka. NPTC hufanya mapitio na kuidhinisha ripoti za maendeleo za sekta na vikundi kazi vya maeneo ya utekelezaji na kutoa mapendekezo kwa ajili ya 85 Wajumbe ni Makatibu Wakuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Raisi-TAMISEMI, Wizara ya Mambo ya Ndani – Polisi, Mageleza na Uhamiaji (pamoja na Biashara ya Kusafirisha Binadamu), Wizara ya Fedha na Mipango (MoFP—Kamishna wa Bajeti), Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto (MoHCDGEC), Wizara ya Katiba na Sheria (MoCLA), Waizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (MoEST), Wizara ya Kilimo, Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, na Wawakilishi wa Wabia wa Maendeleo, Asasi za Kiraia na Mashirika ya Dini. 37 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania maboresho.Sekretariati iko kwenye jengo moja na Wizara. Sekretariati inaundwa na Wizara zinazotekeleza zikiongozwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara inayowajibika kwa Wanawake na Watoto. Sekretariati inahudumia kama katibu wa kamati za ufundi na elekezi, kuratibu mapitio, kufanya ufuatiliaji wa pamoja, na kutayarisha miongozo ya kuwezesha utekelezaji wa NPA katika ngazi zote. Vikundi Kazi vya Maeneo ya Utekelezaji (TWGs) vimepangwa kuendana na maeneo nane (8) ya Utekekezaji ya NPA Tanzania. Hukutana kila mwezi na kuchambua ripoti za utekelezaji, kuwezesha mawasiliano baina ya juhudi za wabia mbalimbali, hutoa mwelekeo wa juhudi za uratibu, na hutoa msaada wa kiufundi kwa wabia. Wakuu wa TWG hutoa ripoti za maendeleo kuhusu utekelezaji wa NPA kwa NPTC. 5.1.2 Mifumo ya Tanzania ya Ngazi Tofauti Katika ngazi za maeneo husika, uratibu wa NPA Tanzania upo katika jengo la Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambalo husaidia utekelezaji wa ufanisi katika ngazi za Sekretariati za Mkoa, Halmashauri, Kata, na Vijiji/Mtaa.86 Wajibu wa OR – TAMISEMI ni kuimarisha taratibu za kuripoti na mawasiliano katika ngazi za maeneo husika, kuwasilisha ripoti zilizokusanywa za mamlaka za Serikali za mitaa kuhusu utekelezaji wa NPA kwa NPSC na NPTC, kuitisha majukwaa ya wadau kila mwaka, na kuhakikisha kuunganishwa kwa afua za NPA na kuhamasisha upatikanaji wa rasilimali katika ngazi ya eneo husika. Sekretariati ya Mkoa inaratibu afua za NPA katika ngazi ya Mkoa na Mwenyekiti wake ni Katibu Tawala wa Mkoa.87 Sekretariati hii hukutana kila robo mwaka ili kujadili maendeleo, changamoto na tuliyojinza na kufuatilia utekelezaji, kuhakikisha mipango na bajeti zote za Halmashauri inajumuisha NPA na kuitisha vikao vya mara mbili kwa mwaka v ya wadau wa Mkoa. 5.2 Mifumo na Taratibu za Uratibu wa GBV Zanzibar Mpango Kazi wa Zanzibar umeandaliwa kwa kufanana na Kamati zilizoanzishwa katika ngazi za Taifa, Wilaya na Shehia (angalia Kielelezo 6 hapo chini). 86 Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto nchini Tanzania 2017/18-2021/22, uk. 29. 87 Kamati ya Kimkoa ya NPA inajumuisha: Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa, Afisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Afisa wa Serikali za Mitaa wa Mkoa, Afisa Elimu wa Mkoa, Mganga Mkuu wa Mkoa, Afisa Mipango wa Mkoa, Mwanasheria wa Mkoa, Afisa Uhamiaji wa Mkoa, Afisa Magereza wa Mkoa, Afisa Kazi wa Mkoa, Hakimu Mkazi, na Wawakilishi wa Asasi za Kiraia, Mashirika ya Dini na Vikundi vya Akina Mama. 38 Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia Kielelezo 6: Uratibu wa GBV Chini ya NPA Zanzibar Kamati ya Taifa kuhusu Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (NC-VAWC) ndio utaratibu wa juu kabisa wa uratibu uliopewa mamlaka ya kusimamia Utekelezaji wa Mpango Zanzibar. Mwenyekiti wa Kamati ni Waziri anaye wajibika kwa mambo ya Sheria na Makamu Mweneyeki wake ni Waziri anayewajibika kwa Wanawake na Watoto. Msimamizi wa ripoti na Habari kuhusiana na uendeshaji wa NC-VAWC ni Katibu Mkuu anayewajibika kwa Wanawake na Watoto. Kamati ya Taifa inaundwa na Mawaziri, Wakuu wa Miko ana Mikutano hufanyika mara mbili kwa mwaka ili kufanya mapitio na kutoa ripoti ya Maendeleo. Kazi kuu za Kamati zinajumuisha: Kutoa ripoti za mara kwa mara kuhusu utekelezaji wa Zanzibar NPA; kutoa mwongozo wa Sera na ushauri wa Kitaalamu kuhakisha Afua zinaendana na Sera na Mikakati ya Taifa; Kufanya utetezi wa Urasimishaji wa NPAVAWC ndani ya Mipango na Mikakati husika ya Serikali katika ngazi zote; Kusaidia utengaji unaotosheleza wa rasilimali; Kuharakisha uchakataji wa matukio yaliyoripotiwa ya Ukatili dhidi ya wnawake na watoto; na kutoa Msaada wa ushauri wa Wizara inayowajibika kwa wanawake na watoto na wadau wengine husika wa Kitaifa katika kutekeleza mamlaka zao ya kushughulikia Ukatili dhidi wanawake na watoto.88 Kamati Mbili za Uratibu wa Kiufundi Visiwani Unguja na Pemba zinawajibika kwa Uratibu na Usimamizi wa Utekelezaji wa Mpango. Mwenyekiti wa Kamati hizi ni Katibu Mkuu wa Wizara inayowajibika kwa wanawake na watoto Kisiwani Unguja, na Umakamu wa Mwenyekiti unashirikisha Wakuu wa Mikoa miwili Pemba. Msimamizi wa ripoti na habari hizi ni Katibu Mkuu wa Wizara. Kamati za Ufundi zinaundwa na Wakurugenzi na Wafanyakazi wa Ufundi kutoka Wizara husika zote za Serikali, Idara na Wakala, NGO na AZAKi. Kamati hufanya mapitio ya Mpango Kazi kila mwaka wa Wakala husika wa utekelezaji na kuhakikisha muunganiko wa hatua muhimu za kushughulikia ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Katika ngazi ya Wilaya, kuna Kamati za Wilaya ambazo Huripoti na husimamiwa moja kwa moja na Kamati husika za Uratibu wa Ufundi Unguja na Pemba. Zinawajibika kwa kuratibu 88 Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto, Zanzibar 2017/18-2021/22, uk. 5. 39 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania na kufuatilia utekelezaji wa Afua zote pia kutengeneza Mipango ya Wilaya ya kila mwaka ya kushughulikia Ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Zinatoa majukwaa kwa mawasiliano baina ya Mashirika tofauti yanayowakilishwa kwenye Kamati. Hukutana kila mwezi na Mwenyekiti wao ni Katibu Tawala wa Wilaya. Cha muhimu zaidi, Kamati katika ngazi ya Wilaya huangalia data za ulinzi na kujadili fursa na mapungufu ya kuzuia na mwitikio wa Ukatili. Kitini kilichoidhinishwa cha kuzoesha utendaji kinatumika kufundishia Kamati zote; hata hivyo, hutegemeana na Mazingira, hofu husika ya ulinzi katika ngazi ya Mkoa au Wilaya inaweza kuongezwa kwenye mafunzo ya Kamati.89 Katika ngazi ya Jamii kuna Kamati za Ulinzi wa Wanawake na Watoto (Kamati za MTAKUWWA), huundwa na waendesha ofisi na wanajamii wanaokutana kila robo mwaka na kushirikishana matatizo ya ulinzi katika uwanda wa ulinzi. 5.3 Mapungufu Muhimu na Fursa kwenye Mifumo na Uratibu Kipengele Kikuu cha NPA ni kwamba hukusanya miundo ya ulinzi kwa Wanawake na Watoto na kuifanya kuwa mfumo mmoja ambao hutoka kwenye ngazi ya Kijiji hadi Taifa. Muunganisho wenye nguvu kutoka OWM chini hadi kwenye ngazi ya Kijiji/Mtaa na Shehia huwezesha mbinu imara ya Afua za kuzuia na kuitikia GBV/VAC. Hii inaakisi na kuimarisha NPA kuweka kipaumbele cha kujenge mifumo. Taratibu za Uratibu zina ahadi ya Kuimarisha uwajibikaji kwa Matokeo kupitia utoaji wa Taarifa wa mara kwa mara. Kutoka ngazi za vijiji/kata na Shehia, ripoti za kila mwezi huzalishwa kutokana na Maendeleo yaliyofanywa, na Afua za kupunguza athari zilizopendekezwa; Katika ngazi ya mkoa, kunatakiwa kuwepo kwa ripoti za kila robo mwaka; na katika ngazi ya Taifa, ripoti za mwaka huonyesha mafanikio na vikwazo pamoja na maarifa yaliyoibuka. Hata hivyo, haikuwa wazi kiwango cha utoaji ripoti ulivyo. Kwa usahihi zaidi, pamekuwepo na Kamati 18,186 za MTAKUWWA zilizoanzishwa, ambazo zinasaidia uratibu imara baina ya watendeji muhimu na Sekta. Kama ambavyo idadi inavutia, lakini bado haiwakilishi utendaji Kitaifa. Aidha, kama ilivyo kwa vipenegele vyote vya Tanzania NPA, ufadhiri bado unabaki kuwa suala la uratibu. Kwa mfano, utafiti uliowakilishwa mwaka 2019 uliripoti kwamba OWM bado haijaelekeza au kutuma mafungu kwa ajili ya kuanzisha muundo wa kamati ya uratibu wa pamoja, kama ilivyopendekezwa katika NPA.90 89 Vitini hivi vinajumuisha lakini haviishii kwenye: Mwongozo wa Usimamizi kwa Wahanga na Kuitikia GBV/VAC wa 2012; Mwongozo wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto 2017/18- 2021/22; na Mwongozo wa taifa wa Malezi na Elimu na Mwongozo wa Sera ya Taifa kwa Sekta ya Afya wa Kuzuia na Kuitikia Ukatili wa Kijinsia, 2011. [[AQ: Tafadhali thibitisha kwmba Tafisiri iliyopo inahitajika katika maelezo haya ya chini (footnote)] 90 Dr. Rasel Mpuya Madaha, 2018. Uchambuzi wa Bajeti na Kufuatilia Ufadhili wa GBV: Kisa Mkasa wa Baadhi ya Wizara za Serikali zilizochaguliwa nchini Tanzania. 40 Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia 6. Programu za Mwitikio na Kuzuia GBV Sura hii inatoa kwa muhtasali baadhi ya vipengele vya msingi vya Programu za mwitikio na kuzuia GBV Tanzania. Haikumanishwa iwe ndio vipengele kamilifu, bali kutoa mwonekeno wa jumla wa miundo muhimu iliyopo katika kuhakikisha huduma kwa wahanga, pia na kutoa ufahamu wa baadhi ya Programu zilizopo za kushughulikia kuzuia GBV. Sehemu hii inalenga katika watendaji wanao ongozwa na Serikali na juhudi ambazo hufanywa na asasi za kiraia chini ya Mpango wa Utekelezaji kwa NPA za Tanzania Bara na Zanzibar, kama mahali pa kuanzia kwa Benki ya Dunia kuwashirikisha wabia wa Kitaifa. 6.1 Programu za Mwitikio 6.1.1 Mwitikio wa Sekta ya Afya Miundombinu mikuu kwa utoaji wa Huduma za kusaidia GBV kwa Wahanga Nchini Tanzania ni za Afya na Ustawi wa Jamii Kitaifa ambazo huendeshwa chini ya MOHSW.91 Kuna mfumo wa Rufaa Kitaifa wa huduma kwa Mgonjwa ambao unajumuisha: Zahanati za Jamii (4,679), Vituo vya Afya (481), Hospitali za Wilaya (95), Hosipitali za Mkoa (19), na Hospitali za Taifa za Rufaa (8) nchini. Kama sehemu ya Tanzania NPA, OSC zimeongezwa kutoka vituo 4 hadi 26. Huduma za Afya, Msaada wa Kisheria, na Huduma za msaada wa Kisaikolojia zinapatikana katika eneo moja, kukiwa na kusudio la kusaidia kuimarisha ushirikiano baina ya watoa huduma mbali mbali katika ngazi ya Jamii na Taifa. OSC huongozwa na Mwongozo wa Taifa wa Kujumuisha na Usimamizi wa huduma za OSC kuwa vituo vya Afya (2013). Wakati watoa habari muhimu wakionyesha kuunga mkono mbinu ya kutumia OSC, wasiwasi uliibuliwa kuhusu kukosekena kwa rasilimali fedha na uwezo wa rasilimali watu. Mwongozo wa Kitaifa wa Sera kwa Sekta ya Afya, kuzuia na kuitikia Ukatili wa Kijinsia (2001) unatamka, wajibu na majukumu ya Wizara na Wadau wengine katika kupanga na kutekeleza huduma jumuishi za GBV. Mwongozo unaofuatia wa Usimamizi wa Huduma za Kitabibu (2011) huagiza Mfumo wa Usimamizi wa Kitabibu uliothibitishwa wa matukio ya Ukatili wa Kijinsia na kulenga kuimarisha Rufaa. Huduma za Afya hujumuisha kupima wagonjwa wa dharura, kutoa huduma za tiba baada ya maambukizi (PEP) na Vizuia mimba vya dharura (ECP), ukusanyaji wa ushahidi wa kisayansi, na kutoa rufaa pale panapo stahiki. Ilipofika 2018, angalau watoa huduma za Afya na Maafisa ustawi wa Jamii 22,600 walipata mafunzo kuhusu viwango hivi kutoa Mikoa ya: Dar es Salaam, Mbeya, Dodoma, Shinyanga, Mara, Mwanza, Geita, Iringa, Njombe, Katavi, Rukwa, Ruvuma, Morogoro, Kigoma, Mtwara, Simiyu Pwani, Lindi, Mtwara, Songwe, na Kagera.92 Pia pamekuwepo na juhudi za kuunganisha GBV na mihula kabla ya kuanza huduma kwa Matabibu na Wauguzi, na kuhakikisha kwamba mafunzo ya GBV yanafika kwa wafanyakazi wa afya wa msitari wa mbele. Mikoa mingi imeendesha mafunzo kuhusu huduma kwa GBV na VAC, matibabu, usimamizi wa ushahidi kisayansi na ukusanyaji wa data. Hata hivyo, watoa habari muhimu walielezea hofu yao kwamba watoa huduma za Afya wanaweza kuwa bado wana mitazamo kwamba hawawasaidii wahanga. 91 Mwongozo wa Taifa wa Sekta ya Afya, uk. 6. 92 Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Beijing na kuendelea 25, uk. 15. 41 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania Kama anavyosema mmoja wa watoa habari muhimu: “kuendelea kuwepo watu wanao hukumu wenzao kwa mitazamo yao tu kuhusiana na wahanga kwamba kwa nini wajiweke kwenye hatari kabla ya yote?, hii hudhoofisha utekelezaji wowote unaowezekana wa vitini kwa wahanga vinavyotolewa na [watoa huduma za Afya].” 6.1.2 Mwitikio wa Sekta ya Saikolojia Kuna Simu ya Kuomba Msaada Kitaifa #116 ambayo inatoa Huduma bila Malipo kwenye Mitandao yote ya Simu za Kiganjani kwa Tanzania Bara na Zanzibar kwa Wanawake na Watoto ambao wapo kwenye hatari ya Ukatili, pia na Familia na Wanajamii wanaoripoti Watoto waliopo kwenye hatari. Simu hiyo ya bure imetengenezwa na Serikali kwa Ufadhiri wa Mfuko wa Watu wa Umoja wa Mataifa (UNFPA). Unahudumiwa na angalau washauri 55. Aidha, Mwongozo wa Sera wa Taifa kwa Sekta ya Afya unaelekeza kwamba msaada wa Kisaikolojia upatikane kwa Wahanga wa GBV. Mwongozo umewateua Maafisa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Jamii kupewa mafunzo ya kutoa huduma za msaada wa Kisaikolojia kwa Wahanga wa GBV, na kusisitiza haja ya usalama na ulinzi, ikijumuisha maeneo salama/nyumba salama.93 Hata hivyo, tathmini ilithibitisha kwamba wakati OSC zikitoa baadhi ya ushauri, kuna huduma chache rasmi za Kisaikolojia kwa Wahanga GBV nchini Tanzania. Hospitali ya Taifa Muhimbili (Hospitali inayofadhiliwa na Serikali) katika Jiji la Dar es Salaam hutoa Programu za ushauri kwa Wahanga wa GBV lakini Programu inalenga kwa Wahanga wa ukatili wa Kingono kwa watoto. Ushauri mwingi unaopatikana katika Hospitali za umma umelenga zaidi katika VVU na sio GBV. Wafanyakazi wa Sekta ya Jamii ni muhimu katika kuainisha hatari za GBV na VAC ndani ya jamii, na mara nyingi ndio sehemu ya kwanza ya mawasiliano kwa Wahanga na huratibu mwendelezo wa huduma. Wakati mafunzo ya Maafisa Ustawi wa Jamii yanafanyika, hayatoshelezi kwa idadi.94 Nchi ina upungufu wa asilimia 62 ya nguvu kazi ya Ustawi wa Jamii, na hivyo hutumia mbinu ya kuwatumia maafisa jamii waliopata mafunzo kama wafanyakazi wa mstari wa mbele katika kuitikia GBV na VAC.95 Aidha, wafanyakazi wa Ustawi wa Jamii waliopo hawajapata mafunzo vya kutosha katika kusimamia mwitikio wa Kisaikolojia. Kufuatia mlipuko wa UVIKO-19, MoHCDGEC, kwa msaada kutoka Shirika la UN Wanawake, waliandaa mafunzo ya kwanza ya kufundisha-wafundishaji kuhusu Afya ya Akili, GBV, na huduma za msaada wa Kisaikolojia. Maafisa Ustawi wa Jamii na Wanasaikolojia 33 kutoka Wizara ya Afya, Chuo cha Ustawi wa Jamii, Chama cha Wafanyakazi wa Ustawi wa Jamii Tanzania, Huduma za Mafunzo Segerea, na Wafanyakazi wa Idara za Maendeleo ya Jamii na Afya walihudhuria Warsha. Mashirika mengine kama vile Shirikisho la Watu wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) walitoa huduma bingwa za ushauri na msaada kwa Wahanga walio na mahitaji maalumu. 93 Mwongozo wa Sera ya Taifa kwa Sekta ya Afya: Kuzuia na Kuitikia GBV, uk 19. 94 Mwongozo wa Uwezeshaji kwa Watoa huduma za Afya na Maafisa Ustawi wa Jamii kuhusu GBV na VAC umeshatayarishwa na kusambazwa tangu Julai 2017. 95 Mahojiano na Mkurugenzi Msaidizi wa huduma za Ustawi wa Jamii, Idara ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii, na Lishe, Ofisi ya Raisi Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa. 42 Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia 6.1.3 Mwitikio wa Kisheria/Haki Mnamo mwaka 2008 na 2012, Wizara ya Sheria na Katiba ilifanya tathmini mbili muhimu ambazo zilielekeza maboresho ya sasa katika sekta ya Sheria, yaani, Tathmini ya Maboresho katika Sekta ya Sheria nchini Tanzania (2008), na Tathmini ya uwezo na mahitaji ya watendaji katika sekta ya Sheria visiwani Zanzibar, pamoja na Tathmini ya Mahitaji na Vikwazo visiwani Zanzibar (2012). Tathmini hizi ziligundua kwamba walengwa wa huduma za Sheria hususani Wanawake, Vijana, Wazee, na Maskini walipitia Vikwazo vikubwa katika kupata huduma, vinayojumuisha rushwa, kutokuwepo unafuu wa uwakilishi Kisheria, na shinikizo la jamii. Matokeo haya yaliungwa mkono zaidi na mahojiano ya watoa habari muhimu. Aidha, mashauri kadhaa ya unyanyasaji wa Kingono huripotiwa kwenye mfumo wa Kisheria, pamoja na “kudai pesa na kuomba ngono yakiwa ndio masharii ya kupata dhamana, upendeleo wa hukumu au manufaa ya ajira.”96 Shinikizo la jamii na rushwa katika mfumo wa Mahakama unamaanisha kwamba viwango vya mafanikio ya kuwatia hatiani Watuhumiwa wa GBV ni mdogo sana. Mashahidi na Wakatili wanaweza kuwa na udhibiti juu ya Wahanga, au Wakatili wanaweza kuwahonga mashahidi au vinginevyo kuingiza rushwa katika mchakato wa Haki. Katika mashauri mengine Wakatili wataomba msamaha na kudai kufidia na kuachana na tabia zao na hivyo shauri hilo litakuwa limesuluhishwa. Wahanga wanaweza wasiripoti wenza wao wa karibu kwa sababu hawataki wenza wao waende jela, kwa sababu ndio waingiza kipato pekee, au wanaogopa kisasi na adhabu kwa kuripoti.97 Kielelezo 7 hapo chini kinaangazia mielekeo hii.98 Kati ya jumla ya Mashauri 1,091 ya GBV yaliyoripotiwa katika Jiji la Dar es Salaam kati ya mwaka 2008 na 2012, Wengi wao (945) waliohusika ni watoto, na aina za ukatili zilikuwa kama ifuatavyo: Ubakaji (533), Usafirishaji wa Binadamu (275), Ufiraji (92) na Ukatili wa Kimwili (24). Chini ya 1 kwa 6 ya Mashauri yaliyoripotiwa katika mwaka wowote yalifikishwa Mahakamani, na Mashauri machache zaidi yalihukumiwa. Kielelezo7: Matokeo ya Mashauri ya GBV yaliyoandikishwa katika Mahakama kutoka Kituo Kuu cha Polisi (2008-2012) 99 Chanzo: Ripoti ya WiLDAF, 2012, p. 40. 96 Mpango wa Marekebisho ya Sekta ya Sheria. Tathmini ya Jinsia ya Taasisi za Sekta ya Sheria nchini Tanzania, Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria, Dar es Salaam, 2012, p. 37. 97 Programu ya Maboresho ya Sheria. Tathmini ya Jinsia ya Sekta ya Sheria ya Taasisi za Sekta ya Sheria nchini Tanzania, Wizara ya Katiba na Sheria, Dar es Salaam, 2012, uk. 37. 98 Kituo Kikuu cha Polisi, Dar-es salaam. 99 Ripoti ya WiLDAF, 2012, uk. 40. 43 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania Hata hivyo, maendeleo kadhaa yanafanyika. Kushughulikia usiri wa Mashauri ya GBV Mahakamani, Zanzibar imeteua Majaji watakaounda Mahakama Maalumu ya Familia ambayo itaharakisha kukamilika kwa Mashauri kwa ajili ya ususruhishi wa haraka. Serikali na Sekta binafsi wameongeza juhudi za kutoa huduma za bure au za gharama nafuu nchini Tanzania na Zanzibar. NGO kadhaa na AZAKi, zikijumuisha Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania, Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, na WiLDAF hutoa msaada wa Kisheria kwa kutumia watoa huduma waliopata mafunzo, hususani katika maeneo ya vijijini. Serikali pia imeanza kutoa msaada wa kisheria na kuongeza uwekezaji katika Programu za Haki za Mtoto kwa ubia na UNICEF na UNDP. Licha ya Maboresho haya Idadi ya Wanasheria wanaotoa Huduma za Msaada Kisheria haitoshelezi kuweza kumdu Mahitaji. 6.1.4 Mwitikio wa Usalama Jeshi la Polisi Tanzania (TPF) limeimarisha mwitikio wake kwa Mashauri ya GBV, ikiwa pamoja na kupitia kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania. Hatua za ziada zilizochukuliwa chini ya Mpango Kazi wa Miaka mitatu wa TPF (2013-2016) ulijumuisha kuanzisha Madawati ya Jinsia na Watoto 417, kutoa mafunzo kwa Maafisa ili watoe huduma zaidi zinazomlenga Muhanga, na kujenga Vituo vipya 13 vya Huduma zote Sehemu moja kwa Tanzania Bara kwa ajili ya huduma za GBV. TPF pia imetayarisha Mwongozo Jumuishi wa kuanzisha kwa Madawati ya Jinsia na Watoto. Wakati wahojiwa wakieleza kwamba pamekuwepo na Maboresho makubwa katika madawati haya tangu kuanzishwa kwa Mwongozo mpya, Maafisa wengi bado wanarudi kuhimiza maridhiano katika mashauri ya ukatili wa mwenza wa karibu. Kulingana na Mhojiwa mmoja muhimu: , ““Maafisa wa Polisi humkejeli mwanamke anayeripoti kupigwa na mwenza, hata kama imepigwa marufuku na Sheria. Mara nyingi watamhoji ni nini kimesababisha mume wake kumpiga.” Hata hivyo, mengi ya Madawati ya Jinsia na Watoto hayana Miundombinu Stahiki kwani siyo yote yamekarabatiwa kulingana na Mwangozo. Katika Matukio haya, faragha inayohitajika kwa wingi inapotea, na kupelekea kukosekana kwa ushahidi muhimu kuhusu maelezo ya kina ya uvunjifu wa Sheria. Pakiwa na Rasilimali Fedha chache kutoka Serikalini kwa NPA, haikuwezekana kufadhiri kuanzishwa kwa Madawati ya Jinsia na Watoto kwa kutumia mahitaji ya chini kwa yale yaliyopangwa. 6.1.5 Njia za Rufaa na Usimamizi wa Habari Kamati za MTAKUWWA zinahisiwa kuboresha Uratibu na kuongeza Rufaa kwenye Mashauri ya Ukatili, Kuwaunganisha Wahanga kwenye Huduma za Msaada. Watoa habari muhimu wameona kwamba pamekuwepo na mabadiliko chanya katika tabia za kutafuta msaada, kama zilivyotamkwa na Mhojiwa mmoja: “Kwa sasa, GBV ni hadharani zaidi kupitia utoaji mkubwa wa habari.” Kigoma iliangaziwa kuwa na wahojiwa wengi kuwa ni eneo la mfano linaloonyesha uwepo wa Kamati za MTAKUWWA changamfu na zilizofadhiliwa vyema, pia na jamii inayoandaa ufahamu na uhisishaji uliopelekea mfumo wa uendeshaji wa rufaa kwa wahanga wa ukatili na kuongezeka kwa kuripoti. Hata hivyo, kama ilivyotajwa kabla, kuna tofauti kwenye uwezo kwa Mikoa kufikiwa na Kamati. 44 Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia NPA pia zinajenga juu ya Mifumo iliyopo ya usimamizi wa mashauri (DCMS) na michakato ya kuendeleza mifumo Jumuishi ya ulinzi wa Wanawake na Watoto. Wakati Mifumo ya ulinzi wa mtoto ilipokuwa inaanzishwa wakati wa NPA-VAC, miundo ya kuzuia na kuitikia ukatili ilikuwa ama dhaifu au haikuwepo. Hapakuwepo na mbinu za pamoja na Polisi, Afya, na Maafisa Ustawi wa Jamiii; hivyo basi, Serikali ilianza uwekezaji katika Mfumo wa kusimamia Mashauri uliopangwa. Kuanzishwa kwa Timu za Kulinda Watoto kulitengeneza njia za Rufaa baina ya Polisi na Sekta zifuatazo: Ustawi wa Jamii, Afya, na Elimu, pia na huduma za dharura kwa Mashauri ya ulinzi wa watoto. Hata hivyo, kuanzishwa kwa Mfumo wa usimamizi wa mashauri katika Wilaya (DCMS) bado unaendelea. Kutoa Ufadhili kwa Uratibu ni Changamoto kwa vile njia mbali mbali za Rufaa huhitaji Rasilimali ili ziweze kufanya Kazi vizuri. Hii inajumuisha kufadhili ukusanyaji wa data na usimamizi. Kwa mfano, Mwongozo wa wafanyakazi wa Ustawi wa Jamii (kwa kutumia karatasi na peni) Mfumo wa kurekodi matukio ya GBV au VAC kwa kutumia karatasi na peni ni kikwazo. Mfumo uliotayarishwa unaotegemea mifumo ya Mitandao kwa usimamizi wa Mashauri kwa Wilaya, umeanzishwa kwenye Wilaya 36 kati ya Wilaya 185, lakini Sehemu ndogo inayohudumia huzuia fursa za kuboresha ufanisi katika kuitikia na kufuatilia mashauri ya GBV na VAC yaliyoripotiwa.100 Mifumo hii ya kutumia karatasi na peni pia inapatikana katika Madawati ya Jinsia na Watoto, Vituo vya Afya na Mahakama. Licha ya taratibu za Rufaa, Mapungufu yameibuka pale panapokuwa hakuna Mfumo rasmi wa Usimamizi wa Mashauri. “… kwa vile hakuna orodha ya ukaguzi (check list) --na pale ambapo ipo hurekodi na kuhifadhi kwa mfumo wa karatasi na peni-- wabia hawawezi kujua jinsi Muhanga anavyosaidiwa kupitia ngazi mbali mbali za rufaa. Kuna haja ya kuwa na mfumo unaojiendesha wenyewe na kuendana na mfumo wa kusimamia Mashauri ili kuwezesha kila mtu katika hifadhi za nyaraka kuweza kufuatilia Muhanga kwa ukamirifu”. . 6.2 Programu za Kuzuia GBV Programu za kuzuia GBV kwa sehemu kubwa zinatokana na jamii na kusukumwa na NGO, Viongozi wa jamii na Viongozi wa Dini. Juhudi hizi zinahitaji kukuza ufahamu na uhisishaji kuhusu GBV ndani ya Taasisi za kujifunza, Taasisi za Dini, na Maeneo ya Jamii. Mfano wa Programu ya kuzuia GBV ni Mradi wa CHAMPION, kampeni ya kuamusha ufahamu wa jamii uliobuniwa kupunguza GBV na kukuza ujumbe chanya na mabadiliko katika desturi za Kijamii. Mradi wa Utetezi Unaosukumwa na Data,101 ni mfano mwingine wa Afua unaolenga katika kuimarisha utetezi na kuendeleza ujumbe stahiki wa Mawasiliano, una vikundikazi vingi na umedhamiria kujenga uwezo wa AZAKi wa kuzalisha na kutumia Data ili kufanya utetezi wa mabadiliko ya Sera yanayohusiana na GBV. (Kwa mifano ya ziada ya Afua za kuzuia zinazotekezwa na NGO na AZAKi nchini Tanzania, angalia Kiambatisho 6.) Wakati Asasi za Kiraia zinawajibika kwa juhudi nyingi za kuzuia GBV nchini Tanzania, baadhi ya Programu za Serikali zimetekelezwa chini ya NPA, pamoja na Mkakati wa Kitaifa wa Mawasiliano na Huduma za kumaliza VAWC Vijijini. Mkakati unalenga katika kushughulikia desturi za Kijamii na kuzibadilisha na kuwa desturi za kijamii zilizo chanya na zinazokinga. 100 Ibid. 101 Mradi uliofadhiliwa na Freedom House na Pact Tanzania. WiLDAF ni mmojawapo wa Washiriki wa Mada kwenye Vikundi. 45 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania Mpango wa mawasiliano umepangwa kwa ngazi ya mkoa kwa msaada wa Asasi za Kiraia. Kulingana na Mhojiwa mmoja: “Kwa vile tunafanya shughuli za uhisishaji pamoja na Serikali, jamii imefurahishwa zaidi na imeshiriki kwa nguvu ince … ni dalili kwamba kuna fursa ya kusikiliza na kuunda upya desturi za kitamaduni zenye madhara.” Visiwani Zanzibar, Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto imezindua Sera ya Taifa ya Ulinzi wa Kijamii Zanzibar mnamo mwaka 2014, ili kuunda Mfumo wa Ulinzi kijamii na kusimamia hatari za kiuchumi kwa wanawake na uhatarishi wa kijamii katika kuhakikisha upatikanaji wa Huduma Muhimu za Msingi. Kujenga juu ya juhudi hizi, Sera ya Taifa ya Ulinzi wa Kijamii, Mpango wa utekelezaji wa Sera (NSPPIP) 2017-2022 bado uko chini ya matayarisho. Aidha, katika baadhi ya Mikoa, Afua zimetekeleza, kuanzisha na kuimarisha vikundi vya akina mama vya kuweka na kukopa na kutoa mafunzo kwa Familia kuhusu usimamizi wa Fedha. Afua nyingine ambayo imethibitika kuwa ya matumaini ni kuimarisha Mfumo wa Usalama wa Umiliki wa Ardhi ili kukuza umiliki wa mtu mmoja mmoja au kwa pamoja.102 Hii inajumuisha kujenga mazingira wezeshi zaidi kwa wanawake kuhodhi hati za Ardhi na kwa Wakulima wadogo, ikijumuisha wanawake vijana, kushiriki na kuwa wenye tija zaidi katika Sekta ya Kilimo. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Benki ya Dunia imetayarisha Mradi wa Maboresho ya Elimu ya Sekondari (SEQUIP), ambayo inalenga katika kuongeza upatikanji wa Elimu ya Sekondari, kutoa mazingira Sikivu kwa Wasichana na kuboresha ukamilishaji wa Elimu bora ya Sekondari kwa Wasichana na Wavulana. Utekelezaji wa Mradi wa SEQUIP unasaidiwa na Mpango Kazi wa GBV ambao unasisitiza vipengele muhimu kuhusu kuamsha ufahamu – na kuhamisha desturi na mitazamo ili kuzuia GBV. 102 Mradi wa pamoja wa Mashirika ya Umoja wa Matafa, UN Women na UNFPA, k.m., Mradi wa Ushirikishwaji wa Ardhi ya Kijiji katika Matumizi bora ya Ardhi katika Wilaya ya Ikungi, Utoaji wa Hati za Haki za Kimila za Umiliki ardhi kwa Wanawake na Wanaume (CCRO’s). 46 Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia 7. Mapendekezo Ikiongozwa na matokeo kutoka kwenye mapitio haya, Sehemu hii hutoa mapendekezo kadhaa ya ngazi ya juu yaliyopangwa kwa kuzingatia maeneo ya msingi ya uchunguzi kwa mapitio haya: Sheria na Sera; Mifumo na Uratibu; na Programu za mwitikio na kuzuia GBV. Mapendekezo hutoa Mambo muhimu ya kuzingatia ya jinsi Benki ya Dunia inavyoweza kusaidia juhudi za Programu maalumu za GBV nchini Tanzania na pia ime- kusudia kuongoza mikakati ya siku zijazo na kujenga usikivu kwa GBV katika Idara za Maendeleo za Benki ya Dunia. 7.1 Sheria na Sera Juhudi za ziada za NPA hufanya maboresho ya Sheria ambazo zinadhoofisha haki za wanawake na wasichana kuwa huru kutoka kwenye ukatili na ubaguzi, hususani kukuza utetezi kuhusu Sheria mahususi za Ukatili wa nyumbani na Kubaka katika ndoa ndani ya Makosa ya Jinai. Kuzingatia kuwezesha mkakati ambao unasaidia kuwa na ufadhili endelevu kwa NPA na utekelezaji wake ulioharakishwa, kama vile kupitia kuanzishwa mfuko Mkuu unaoongozwa na Serikali pamoja na misaada kutoka sekta binafsi na Wadau wa Maendeleo. Kuhakikisha kwamba mkakati huu unajenga dhamira na uwezo wa Serikali kukidhi majukumu yake ya kibajeti kupitia maendeleo na utekelezaji wa mikakati inayoendelea ya kuhamasisha upatikanji wa Fedha. Kusaidia kufanya tathmini ya NPA kwani zinakaribia kukamilisha miradi yao na zinaweza kutumika kama msingi wa kumwandaa mrithi (Warithi). Kujenga juu ya mfano wa Shinyanga, kusaidia juhudi za kuimarisha katika Tanzania NPA kwa ngazi ya mkoa kama njia ya kujenga umiliki na utekelezaji wa NPA Kimkoa. Kufanya mapitio ya Mpango wa Taifa wa Utekelezaji wa Ulinzi wa Kijamii: Kufanya tathmini ya juhudi za sasa za kuongeza uwezeshaji Kiuchumi kwa Wahanga wa GBV pamoja na wanawake na wasichana walio katika hatari ya ukatili, na kubuni Afua zaidi zinazolenga kwenye utulivu wa kiuchumi kulingana na matokeo ya tathmini hii. 7.2 Mifumo na Uratibu Kuimarisha mifumo ya kitaifa ya uratibu kwa kuwezesha mapitio ya haraka ya utekelezaji wa mfumo wa uratibu kwa NPA na kulenga kusaidia mapungufu muhimu katika ngazi ya kitaifa, kama vile MoHCDGEC, pia na Sekretariati ya Kamati Elekezi ya Taifa ya Ulinzi. Jumuisha katika hili uwezo wa kufuatilia na kuripoti uratibu katika ngazi zote za mfumo wa uratibu. Wekeza katika maboresho kwa mifumo ya usimamizi wa habari ya GBV ili kuhakikisha kuna data bora zenye viwango na ubora za GBV zinakusanywa nchi nzima. Hii inaweza kufanyika kupitia kuanzishwa kwa Mfumo wa Usimamizi wa Mashauri wa Wilaya (DCMS) katika zile wilaya ambako hazijaanzishwa. 47 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania 7.3 Mwitikio na Kuzuia Ongeza uwekezaji kuelekea maendeleo au kuimarisha uwezo wa mifumo, miundo, na taratibu za utoaji wa huduma/mwitikio kwa GBV ili kuhakikisha uwepo, upatikanaji, utumiaji, uitikiaji, na uwajibikaji wa huduma hizi katika mnyororo mzima wa utoaji huduma, hizi ni sekta ya sheria, afya, na ustawi wa jamii. Kubadili desturi za kijamii ambazo zinaendeleza kutoa ripoti hafifu za GBV kwa kukuza tabia za kutafuta msaada na kujenga uwezo wa watoa huduma ili kuwawezesha kuhakikisha kuna mbinu za GBV ambazo zinamlenga muhanga. Saidia maendeleo ya mfumo wa kitaifa wa kufuatilia ubora na uendelevu wa utoaji huduma katika OSC, pamoja na tathimini ya uwezo wa wafanyakazi na mrejesho wa ubora-wa- huduma wa wahanga wanaopata huduma. Wekeza katika mafunzo ya wafanyakazi kuhusu mbinu zinazomlenga muhanga na kupanua upatikanaji wa matunzo kwa watu wanaopata huduma finyu kupitia Kamati za MTAKUWWA. Jenga mkakati wa kujenga nguvukazi ya Ustawi wa Jamii na kuboresha uwezo wa wafanyakazi wa Ustawi wa Jamii wa kutoa huduma za kisaikolojia kama sehemu ya usimamizi wa mashauri. Wezesha mafunzo ya Polisi kupitia Chuo cha Polisi pia na kupitia mafunzo mahususi ya Madawati ya Jinsia ya Polisi kuhusu mwongozo uliopo wa madawati ya jinsia na watoto. Zingatia kufanya majaribio ya mfano ya Mahakama Maalumu ya Familia Zanzibar huku Tanzania Bara ili kujenga uaminifu katika michakato ya Mahakama na kuharakisha mashauri Kujenga uelewa wa kisheria miongoni mwa watu kupitia tafsiri za Sheria na Sera, pia na kusaidia shughuli za jamii za Mkoba na kuhisisha. Unganisha hili ili kusaidia msaada wa kisheria wa bure katika maeneo ambao kwa sasa haupatikani kwa wahanga. Saidia mapitio ya Mkakati wa Taifa wa Jamii na Huduma za Mkoba ya NPA ili kuhakikisha kwamba mbinu yake inaendana na utendaji bora kwa uzuiaji wa GBV, kupitia kubadili desturi za kijamii na kuzingatia kuongeza vipengele vya mkakati ili kusaidia mabadiliko ya tabia yanayopimika. 48 Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia Kiambatisho 1: Mahojiano ya Mtoa Habari Muhimu. Maswali ya Kuongoza: 1. Je umehusika katika kuendeleza na utekelezaji wa jumla wa Mpango Kazi wa Taifa 2017- 2022? 2. Je ni jinsi gani matokeo matatu muhimu yafuatayo yametekelezwa? Mazingira wezeshi– mazingira ya sheria na sera, rasilimali za kutosha, usimamizi wa data na habari na maboresho ya uratibu Kuzuia – kuimarisha desturi na maadili, kuimarisha kipato na uchumi, mazingira salama, msaada wa familia na mzazi, elimu, na stadi za maisha Huduma za Mwitikio na Msaada– taratibu zilizojumuishwa za ulinzi kitaifa zimeanzishwa, huduma za mwitikio na msaada kitaifa na mahali husika. 3. Katika kutayarisha matokeo ya NPA, kanuni muhimu za kuongoza ziliandikwa kwa muhtasari ili kuhakikisha mwitikio wa Mpango. Ni jinsi gani kanuni hizi zimejumuishwa katika utekelezaji wa Mpango? hususani, Kwamba mfumo unafikiwa na wanawake na watoto wote na kote Zanzibar pamoja na maeneo ya vijijini ambayo ni vigumu kuyafikia Usiri na faragha za wahanga unaendelezwa Usalama, uzima na uwezeshaji wa wanawake na watoto ni muhimu sana; uwajibikaji wa wakatili unasisitizwa na kutafutwa kupitia njia zote stahiki. 4. Kwa ujumla, Je, NAP-VAWC inaitikia vya kutosha katika kuzuia na mwitikio wa GBV/VAC? 5. Mwitikio wa kisekta uliotarajiwa katika Mpango huu unahusisha ubia wa sekta kadhaa pia uratibu na ubia baina ya sekta ya umma na binafsi pia na wadau wengine. Ni kwa kiwango gani ubia huu na jinsi gani wanaitikia kumaliza GBV? 6. Ni jinsi gani utaratibu wa uratibu wa kisekta unavyofanya kazi? Kufuatilia mafanikio, changamoto na tuliyojifunza. 7. Ni kwa kiwango gani rasilimali ziliweza kwa utoshelevu kuwezesha kufanikisha NPA-VAWC? 8. Mapendekezo ya kumaliza GBV? Ni kitu gani zaidi kinapaswa kufanywa ili Programu ziweze kufanya kazi kikamilifu? 49 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania Kiambatisho 2: Watoa Habari Muhimu Waliohojiwa 1. Rasheed Mufta –Huduma za Ustawi wa Jamii, Idara ya Afya 2. Anna Kakuta - WiLDAF 3. Mary Richards, Mkuu wa Programu, TAWLA 4. Anna Henga, Mkurugenzi Mtendaji, LHRC 5. Fulgence Massawe, Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho, LHRC 6. Hodan Addou -UN Women – Mkurugenzi Mkazi, UNICEF 7. Maud Droogleever Fortuijn- UNICEF 8. Stephanie Shanler - UNICEF Mashauriano ya Warsha Zanzibar 9. Bibi. Muhaza Gharib Juma -Ustawi wa Jamii 10. Hafidhuu Said – Ustawi wa Jamii 11. Jamila Mahamoud- ZAFELA 12. Abdallah Abeid- ZAFAYCO 13. Zahor Faki Mjaka- DAWATI LA POLISI 14. Amina Abdulrahma Yussuf- (JUMAZA) 15. Naila Abdulbasit – Mahakama ya Watoto 16. Ali Rashid Salim – Mshauri wa Vyombo vya Habari 17. Asha Aboud – ANGOZA 18. Onesmo Ole Ngurumwa 19. Ali Chirikira – UN Women 20. Salma Said- WAHAMAZA 21. Abeid – ZanzibLS 22. Hassan Issa – UKUEM 23. Hawra Shamte - TAMWA 50 Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia Kiambatisho 3: Sheria za Taifa Kuhusiana na GBV Sheria Muhtasari Katiba ya Muungano Kwa uwazi kabisa inapiga marufuku ubaguzi kwa misingi ya jinsia wa Tanzania 1977 pamoja na mambo mengine. Ibara 12-29 zinajumuisha Muswada wa Haki na Wajibu, ambao unaelekeza haki na wajibu wa msingi wa raia ambao kwa upana wake unathibitisha na kulinda dhidi ya GBV. Sheria ya Adhabu, Sura Imetumika hata kabla ya Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961103, 16 (imepitiwa mwaka inapinga makosa ya GBV kama vile uchokozi na kuwatelekeza watoto. 2002) Sheria ya Ndoa, Sura. Sheria hii ndio kuu ambayo hutawala aina zote za maswala ya ndoa 29 nchini Tanzania. Imekuwepo tangu 1977 ikifanyiwa marekebisho makubwa kwa mwenendo wa haki za binadamu kupitia CEDAW, Itifaki ya Maputo na sheria nyingine. Vyombo vya Sheria Sheria ya Mtoto (2009) Ilitungwa ili iwezeshe sheria za kimataifa za haki za binadamu kuhusu na Sheria ya Watoto haki za mtoto, vyombo vya sheria pia na taratibu za kuunganisha Zanzibar 2011 sheria zinazosimamia haki za watoto. Sheria pia imekuja kama suluhisho kwa madai na utetezi wa muda mrefu wa wadau katika haki za watoto. Inaanzisha taratibu za kisekta ambazo zinatoa viwango vya kutambua, kurejea, na kuitikia mashauri ya vitendo vibaya kwa mtoto na aina nyingine ya ukatili.104 Zinajumuisha vipengele vinavyohitajika kujenga mazingira ya ulinzi, pamoja na mfumo rafiki wa haki kwa mtoto. Sheria ya Mtoto inakataza kazi kwa mtoto, (Kifungu 78) na utumwa wa kingono kwa watoto (Kifungu 83). Adhabu ya utumwa wa kingono wa mtoto ni faini ya sio chini ya shilingi ya Kitanzania milioni 1 na au zaidi ya milioni 5 au kifungo cha si zaidi ya miaka 20 au vyote.. Sheria ya Ushahidi Sheria ya Ushahidi (Sura 6) imepitia marekebisho mengi tangu marekebisho SOSPA mwaka 1998. Kwa maana ya ukubalifu wa ushahidi, hii imepanuliwa ili kuruhusu ukubalifu wa ushahidi kutoka kwa watoto wadogo ambao ni wahanga wa ukatili. Sheria inatamka kwamba mtoto anaweza kutoa ushahidi wa matukio hata kama haukuwa shirikishi ili mradi Mahakama inagundua kwamba ushahidi huo unaaminika na umesaidia kuthibitisha thamani ya ushahidi unaotolewa na watoto katika makosa ya kingono. Hii inaweza kuwa imechangia kuongezeka maradufu kwa utoaji wa habari nchi nzima kwa Polisi kuhusu makosa ya kingono kwa watoto chini ya miaka 15 wakati wa kipindi cha 2004-2008.105 Sheria ya Makosa Ilitungwa ikiwa na lengo la kulinda utu na utengamano wa wanawake ya Kingono(Vifungu katika maswala kuhusiana na kubakwa, kuingiliwa, kinyume cha Maalumu) 1998 maumbile, unyanyasaji wa kingono, kufanya ngono na ndugu wa karibu, ukeketaji, vitendo vibaya kwa mtoto, na biashara ya kusafirisha watoto. 103 Kanuni ya Adhabu, Sura. 16 ni sehemu ya sheria zilizopokelewa za 1930. 104 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2011, Ukatili Dhidi ya Watoto Tanzania: Matokeo kutoka Utafiti wa Kitaifa wa 2009, uk. 110. 105 Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania, Mapitio ya Sheria na Sera zinazohusiana na Ukatili wa Kijinsia Tanzania Bara, uk. 18. 51 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania Sheria ya Kuzuia Sheria ya Kuzuia Biashara ya Binadamu 2008 hutekeleza majukumu Biashara ya Binadamu ya Tanzania chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa dhidi ya Uhalifu, Na. 6, 2008 Uhalifu Uliopangwa wa Kimataifa, ikiwa ni pamoja na Itifaki ya Kuzuia, Kukandamiza na Kuadhibu Biashara ya Binadamu. Hii inajenga kutoka kwa adhabu za uhalifu wa kufanya biashara ya watu iliyoanzishwa na SOSPA na kuweka ufafanuzi, adhabu, na ulinzi wa wahanga chini ya mwamvuli wa kisheria. Sheria ya Kuzuia VVU/ Inapiga marufuku unyanyapaa na kuainisha maambukizi ya VVU. UKIMWI Na. 28, 2008 Sheria ya Ardhi, 1999 Dhana ya kuwahusisha wanawake katika mali ya ndoa. Sheria ya Kuzuia na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa 2007 inaanzisha Taasisi Kupambana na Rushwa ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). TAKUKURU 2007 imepewa mamlaka ya kushughulikia aina zote za rushwa ikiwemo madai au kutoa upendeleo wa kingono kwa kubadilishana na huduma za kiofisi. Kifungu 125 cha sheria ya kupambana na rushwa inatamka kwamba “Mtu yoyote akiwa kwenye nafasi au mamlaka, ambaye katika utekelezaji wa mamlaka yake, anadai au kulazimisha upendeleo wa kingono au aina nyingine yoyote kwa mtu mwingine kama masharti ya kutoa ajira, kupandishwa cheo, haki, upendeleo au aina nyingine yoyote ya kutendewa kwa upendeleo anafanya kosa na atawajibika atakapotiwa hatiani kwa faini isiyozidi shilingi milioni tano au kifungo kisichozidi miaka mitatu au vyote.” Hii inatamka kwa uwazi kabisa ulinzi dhidi ya utumwa wa kingono na vitendo vibaya, kwa lugha isiyo rasmi huitwa ‘upokonyaji’ wa kingono. Sheria ya Ajira na Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi 2004 hueleza haki za Mahusiano ya Kazi, kazi na kuanzisha viwango vya msingi vya ajira. Sheria inapiga 2004 marufuku ubaguzi kwa misingi ya jinsi, jinsia, mimba, hadhi ya ndoa, ulemavu, VVU/UKIMWI au umri. Unyanyasaji wa kingono pia umepigwa marufuku kama ilivyotamkwa katika Kifungu 7(5). Sheria pia inapiga marufuku kazi za usiku kwa wamama wenye mimba chini ya mazingira fulani,110 wakati tunathamini likizo ya uzazi kama haki kwa wamama na likizo kwa wababa. Kanuni za Sekta ya Umma Zanzibar ya 2014, Kifungu 36(1) inapiga marufuku aina zote za ukatili wa kijinsia mahali pa kazi kwa waajiriwa na waajiri. Sheria ya Mwenendo Huzuia kila mtu anaetuhumiwa kwa makosa ya kingono kupata wa Makosa ya Jinai dhamana na imeongeza adhabu ambazo Mahakama inaweza 2007/8 kupasisha kwa mashauri yanayohusiana. Sheria ya Elimu 2016 Inapiga marufuku ndoa za utotoni kwa kutamka wazi katika kifungu 60 (1) kwamba ni kinyume cha sheria katika mazingira yoyote yale kwa a) mtu yeyote yule kumuoa au kuolewa na msichana au mvulana wa shule ya msingi au sekondari au b) mvulana wa shule ya msingi au sekondari kumuoa mtu yeyote. Ukiukaji wa sheria hii unastahili kifungo cha miaka 30 na pia inaeleza adhabu kwa kumpa mimba msichana wa shule ya msingi au sekondari kuwa miaka 30. Kwa yeyote anayesaidia. Kwa mtu yeyote anayesaidia, kupunguza, kutoa ushauri kwa mtoto anayeenda shule kuolewa au kuoa wakati aifuatilia elimu yake pia amefanya kosa na anastahili kifungo cha miaka 5 au faini ya shilingi milioni tano au vyote Sheria pia inatamka kwamba “kila mkuu wa shule ataweka kumbukumbu na kuwasilisha kwa Kamishina au mwakilishi wake ripoti ya kina ya kila robo mwaka ya matukio ya ndoa, na na hatua za kisheria zilizochukuliwa dhidi ya wakosaji.” 52 Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia Kiambatisho 4: Mifumo ya Kimataifa na Kitaifa Inayohusika kwa Dhamira ya Tanzania Kuhusu GBV Mifumo ya Kimataifa na Kitaifa iliyodhamiria kumaliza ukatili dhidi ya wanawake na Watoto Malengo Endelevu ya Maendeleo (SDG) yameweka malengo ya kufikia maendeleo yanayopimika kushughulikia ukatili dhidi ya wanawake na watoto: SDG 5 linataka kufikia usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake na wasichana wote na kuweka malengo kuhusu kutokomeza desturi zenye madhara. SDG 16 linaweka malengo ya kumaliza vitendo vibaya, utumwa, kusafirisha na aina zote za ukatili dhidi ya watoto. Hitimisho lilokubaliwa liloidhinishwa na Tume kuhusu Hadhi ya Wanawake (CSW) katika kikao chake cha 57 kilielekeza mwongozo zaidi wa kuanzisha huduma jumuishi, zilizoratibiwa, muingiliano wa kisekta, zinazofikika na endelevu kwa wahanga wote wa aina zote za ukatili dhidi ya wanawake na wasichana. Mikakati Iliyohuishwa ya Mfano na Hatua za Vitendo kuhusu Utokomezaji wa Ukatili dhidi ya Wanawake katika Tasnia ya Kuzuia Uhalifu na Sheria ya Adhabu zzinaelezea mapendekezo mapana ambayo yanagusa utoshelevu, taratibu na uendeshaji wa masuala ya sheria, wakati tukitambua umuhimu wa mbinu za ujumla, zilizoratibiwa kisekta. (Azimio la Baraza Kuu 65/457). Mkataba kuhusu Utokomezaji wa Aina Zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake (CEDAW, 1985 na Itifaki yake Mbadala (2006). Mapendekezo ya jumla 19 yanatoa kwa muhtasari ni nini nchi wanachama zinapaswa kufanya kushughulikia suala la ukatili dhidi ya wanawake. Azimio la Beijing na Jukwaa la Vitendo, 1995 na Maeneo yake 12 Muhimu ya Hofu. Serikali imeanisha maeneo manne ya utekelezaji kama vipaumbele vya nchi: kukuza uwezo wa kisheria wa wanawake, uwezeshaji kiuchumi wa wanawake na kutokomeza umasikini, uwezeshaji wa wanawake kisiasa na kufanya maamuzi, , na upatikanaji wa elimu na ajira kwa wanawake. Mkataba wa Haki za Mtoto (CRC), 1989 na Itifaki Mbadala Itifaki ya Kuzuia, Kukandamiza na Kuadhibu Usafirishaji wa Watu, hususani Wanawake na Watoto, 2006 Mkataba wa Afrika kuhusu Haki za Binadamu na Watu (ACHPR), 1984 Itifaki ya Mkataba wa Afrika kuhusu Haki za Binadamu na Watu kuhusu Haki za wanawake barani Afrika (Itifaki ya Maputo), 2003 Mkataba wa Afrika kuhusu Haki na Ustawi wa Mtoto (ACRWC) na Itifaki zake Husika 53 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania Dira ya Maendeleo Tanzania 2025 na lengo lake la amani na kuvumiliana kijamii inayojumuisha usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake katika nyanja zote za kijamii, kiuchumi na kisiasa. Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Zanzibar (MKUZA III): Unawezesha wanawake na kuwalinda watoto katika mageuzi ya kiuchumi na kijamii Inaweka malengo ya usawa wa kijinsia na fursa Inaweka malengo ya kuzuia na kuitikia dhidi ya ukatili. Kiambatisho 5: Kanuni Zinazoongoza na Mbinu za NPA Mbinu ya Utekelezaji Hatua Zinazopendekezwa Kufikia mfumo sahihi wa Sheria ya Ndoa kupunguza ndoa za utotoni kisheria Sheria ya Mirathi Sheria ya Mtoto kuainisha Ukatili dhidi ya mtoto kuwa jinai Kuimarisha mifumo mbadala ya sheria Kukuza mfumo wa sheria ulio sikivu na unaojali kwa watu wanaoishi mazingira magumu, hususani watoto wanaopishana na sheria, wanawake na watoto wenye ulemavu na watoto wenye ualbino . Mwitikio wa kisekta Ubia baina ya sekta mbalimbali, pamoja na afya, jinsia, ulinzi wa watoto,elimu, utekelezaji wa sheria, masuala ya mahakama na kijamii, sekta ya umma na binafsi, asasi za kiraia, na vyama vya wanataaluma. Mwitikio wa kukuza Uchambuzi wa uwezo na “mahali pa kuanzia” katika ngazi ya kitaifa na wilaya ili kuhakikisha tofauti za kijiografia hazitengenezwi/kuendelezwa. Kujenga mfumo jumuishi na ulioungwa kwa Wahanga wote wa Ukatili kama vile: Kamati za Ulinzi, Kituo cha huduma zote sehemu moja, Polisi, Madawati ya Jinsia na Watoto. Kuimarisha utambuzi, utoaji wa huduma na kuripoti. Kuelekeza Afya bora, Ustawi wa Jamii na Sheria za Jinai na huduma za msaada kwa wanawake na watoto ili kuitikia Ukatili. Mkazo kwenye Kuzuia Kazi endelevu kwenye desturi na maadili. Kujenge uwezo wa familia na jamii ili kuwawezesha na kuwalinda wanawake na watoto. Kulenga sababu za msingi za Ukatili katika hatua zote za maisha. Kuwashirikisha wanaume kama Wadau muhimu katika kushughulikia majukumu ya Jinsia yasiyo sawa. Kuhakikisha Watoto wako salama Shuleni. 54 Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia Kuimarisha Ukusanyaji Kuendeleza viashiria na zana za kupimia mielekeo111 ili wa Data, Uchambuzi na kuendana na ramani ya maendeleo ya Taifa, Ajenda 2063 na Kuripoti SDG, na kutatua kukosekena kwa data za msingi. Kujenga juu ya vyanzo vya data iliyopo na kurasmisha sekta zoto husika. Utendaji unaotegemea Ushahidi ili kufanya maamuzi ya Afua. Maridhiano ya utendaji bora yanayohusika katika muktatha wa kijamii na kitamaduni. Kujenga Harakati Kuongeza idadi na uanuai wa watendaji wanao fanya kazi ya kuzuia Ukatili katika ngazi zote. Kushirikisha miundo na michakato ya jamii ya kitamaduni. Kutafsiri mipango kuwa Kuunganisha Afua zilizowekewa gharama yake ndani ya Bajeti Mfumo wa Bajeti ya mwaka ya Taasisi husika zinazotekeleza. Kulenga wale wanaoishi Kulenga kwa wanawake na watoto wenye uhatarishi zaidi katika mazingira hatarishi Kushughulikia mahitaji ya wanawake na watoto walio katika mazingira hatarishi na wanaobaguliwa kwa sababu ya Jinsia, Kipato, Ulemavu, au Kadhia nyingine. Uratibu na Mashirikiano Kimarisha uratibu katika ngazi ya Taifa na ngazi za chini. Kukuza ufahamu kuhusu malengo ya Mpango wa mwaka na hadidu rejea. 55 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania Kiambatisho6: Mifano ya Programu za Kuzuia GBV nchini Tanzania 1. 1. KIVULINI: Uhamasishaji wa Jamii ili Kutokomeza GBV KIVULINI ilianzishwa mwaka 1999 na hufanya kazi kwa karibu na wanawake na wanaume kupitia vikundi kazi, wanaojitolea katika jamii, na vikundi vya kutokomeza ukatili. Kivulini hufanya kazi kushughulikia sababu za msingi za GBV kwa kuhamasisha jamii (vijana, wanawake, na wanaume) katika kipindi cha muda mrefu ili kubadili mitizamo. Kazi ya kuzuia GBV inategemea kwenye Kuhamasisha Jamii Kuzuia Ukatili wa Nyumbani uliotayarishwa na “Kupaza Sauti”. Vikundi vya Jamii viko katika mstari wa mbele wa juhudi na hutimiza wajibu muhimu katika ‘kutoa neno nje’ kwa wanawake wengine, wanaume, viongozi wa jamii na watoto. Kuna zaidi ya wanachama 300 wanaoongoza katika kupanga na kuendesha midahalo ya jamii, tafrija za umma, maigizo katika jamii, maonyesho ya video, na majadiliano yasiyo rasmi, n.k., ndani ya mitaa yao na jamii. Hawa wanajamii pia hufuatilia mashauri ya Ukatili, kusaidia wanawake wanaopitia Ukatili, kuendesha upatanishi kwenye familia na hutoa rufaa kwa wateja kwenda Kivulini au Taasisi nyingine husika inapotokea msaada wa ziada unahitajika. Lengo ni kujenga maridhiano kuhusu, na hatua dhidi ya Ukatili wa nyumbani. Wawakilishi wa vikundi vyote hukutana kila mwezi na wafanyakazi wa Kivulini ili kupanga na kufanya mapitio, kujadili changamoto, kutatua matatizo,na kupata mafunzo ya ziada. Wawakilishi hawa baadae hutoa mafunzo na kuwasaidia wanachama wengine kwenye vikundi. 2. AFNET: Watawa Wakatoliki wa Masanga na Ibada Mbadala Ufahamu na Utetezi wa FGM unaongozwa na Mtandao wa Kupinga Ukeketaji Tanzania (AFNET) ambao hujitahidi kujenga ufahamu wa madhara hasi ya FGM na umuhimu wa kuyatokomeza.106 Plan International, Tanzania, pia inaongoza muungano wa kujenga ufahamu, kutoa mafunzo, ushauri na kuwezesha Wahanga kuvunja duara la FGM na kufanya Utetezi wa mabinti zao na ndugu wasifanyiwe FGM.107 Kupitia Afua za ushirikiano kama vile mafunzo ya mwezi mzima kuhusu Haki za Binadamu, Afya ya Uzazi, Ufundishaji wa ziada wa Masomo ya Shule na Mafunzo chanya ya kimila, yakifuatiwa na Sherehe za kuhitimu, hii husimama kama mbadala kwa FGM kuwa desturi ya kuwafunda wasichana katika jamii. Hii imetendeka tangu mwaka 2007 na imepelekea kuhitimu kwa zaidi ya wasichana 2,000 ambao walihudhuria makambi. Mafunzo haya yanalenga kuwalinda wasichana dhidi ya FGM, ndoa za utotoni, mimba za vijana, na kuwabakisha shuleni. Chama cha Kutokomeza Ukeketaji katika Kituo cha Masanga kina Ibada Mbadala ambazo zilipongezwa na Serikali kama njia moja ya kuthibitisha kwa jamii uwezekano wa kuendeleza viwango vya maadili mema bila ya kuwashurutisha wasichana kufanya FGM. Mnamo mwaka 2019, iliripotiwa katika Gazeti la Kitaifa kwamba wasichana walioweka kambi katika Kituo cha Masanga wakati wa msimu wa FGM ufanyike katika maeneo mbalimbali ya Mkoa. Wasichana wengi walitoroka kutoka majumbani mwao kwenda kwenye Kituo baada ya kugundua kwamba wako katika hatari kubwa ya kulazimishwa kufanyiwa desturi zilizo na madhara. Kituo cha Masanga kimekuwepo tangu 2008, na kimeokoa takribani wasichana 106 Mtandao dhidi ya Ukeketaji (NAFGEM) 107 Amiri. A. Ukatili dhidi ya Wanawake nchini Tanzania: Ukeketaji (FGM), uk. 24. 56 Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia 3000 wasifanyiwe Ukeketaji. Kituo kipo kimkakati katikati ya jamii ambazo zinakumbatia FGM. Kinaendeshwa na Watawa wa Kanisa Katoliki chini ya Dayosisi ya Musoma.108 3. TANLAP: Vilabu vya Kupinga-GBV – Kubadilisha Desturi katika Miaka ya Kukua Mradi unawalenga watoto na vijana, haki za wasichana, na vilabu vya msaada wa Kisheria katika Wilaya zilizoteuliwa katika Mkoa wa Kagera, ambavyo vilianzishwa mapema mwaka 2019, kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa wa Kagera. Iliwezesha kufanyika kwa midahalo na kutoa mafunzo kwa wasichana wadogo kuhusu haki zao, ikiwemo haki ya kupata Elimu, umuhimu wa utawala wa Sheria na upatikanaji wa haki. Vilabu hivi vinavyoendelea pia hutoa Majukwaa/Fursa zenye manufaa kwa wasichana, wavulana, wasaidizi wa sheria, maafisa usitawi wa jamii na walimu kukutana na kujadili masuala yanayohusiana na haki za wasichana na huduma za msaada wa kisheria. Kwa ajili ya kukuza na kulinda wanawake, wasichana, na wavulana ndani ya jamii zao dhidi ya GBV. 4. Kutetea Usawa wa Kijinsia: Mradi wa CHAMPION wa Kuzuia Ukatili wa Kijinsia nchini Tanzania Kuwa Mfano wa Kuigwa (Be a Role Model) vyombo vya habari na kampeni za jamii za kuamsha ufahamu zilizinduliwa ili kushawishi mdahalo wa Kitaifa kuhusu GBV nchini Tanzania. Yakiwa yamesambaa kupitia Magazeti na mitandao (k.m., television, redio), kampeni ililenga kwenye ujumbe muhimu wa GBV ukijumuishwa na ujumbe wa kuhamasisha na wito kwa wanaume kuwa “role models” katika jamii zao. Aidha, Mradi wa CHAMPION ulitoa mafunzo kwa Wandishi wa Habari 125 kuhusu GBV. Shughuli nyingine za Mkoba zililenga maeneo ambayo wanaume hukusanyika kama vile mashindano ya Mpira na kwenye Baa. Mradi ulitoa msaada kiufundi na mafunzo kwa MCDGC kuhusu mikakati mizuri ya kushughulikia GBV, pamoja na uratibu wa Kisekta na juhudi za AZAKi kushughulikia Ukatili. Aidha, Mradi wa CHAMPION ulifanya kazi na MCDGC kutayarisha moduli ya ziada za GBV kwa ajili ya Mtaala wa Taasisi za Ufundi za Maendeleo ya Jamii, pia rasimu ya Mwongozo wa Kitaifa wa Uratibu wa Afua za GBV. Matokeo ya Afua za GBV yameonyesha thamani ya kuwekeza katika mazingira ya kijamii na kitamaduni ili kubadili mitazamo na Imani kuhusu Jinsia, Ukatili, VVU, na uhusishaji wa wanaume. Aidha: Mradi wa CHAMPION wa Afua za GBV uliwafikia takribani wanajamii 90,000 wakiwa kama mtu mmoja mmoja au Vikundi vidogo ambavyo vinatekeleza shughuli ya kuzuia GBV katika Wilaya zilizolengwa. Kuongezeka ufahamu wa GBV pia kulipelekea kuongezeka kwa idadi ya watu wanaotafuta msaada. Matokeo kutoka tathmini ya ubora ilionyesha kwamba mitazamo ya jamii na midahalo kuhusu GBV imeboreshwa katika muda kutokana na Mradi. Ujumbe mfupi wa Redio, Mabango, Mafunzo, na Programu za Mkoba kwenye jamii ulichangia katika mabadiliko mengi chanya. Kampeni ya vyombo vya Habari ya “Kuwa Role Model” ilikuwa ya mafanikio kwa kufanikisha lengo lake kuu la mabadiliko ya tabia: Kuongeza midahalo kuhusu GBV na kuhamisha desturi za kijamii kuhusu GBV zilizojikita nchini Tanzania. Matokeo yalionyesha kwamba inawezekana kubadili maoni na tabia kuhusu GBV, kama vile iwapo mwanaume ana haki ya kumpiga mke wake, anaamua kufanya mambo dhidi ya GBV, na kuanzisha mazungumzo kuhusu GBV na Familia na Marafiki, kupitia mawasiliano ya vyombo vya habari kwa Umma.109 108 Umoja wa Mataifa, Tanzania, UNFPA, Tanzania na Umoja Ulaya, Taarifa za FGM. 109 Engender Health (2014) Vinara wa Usawa wa Kijinsia: Mradi wa CHAMPION, Afua za Kuzuia Ukatili wa Kijinsia. JARIDA LA CHAMPION Na. 14. CHAMPION-Brief-14-GBV-Overview_lowres.pdf (engenderhealth.org) 57 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania Kiambatisho 7: Utendaji Bora katika Muktadha wa Ulinganifu Kuhusu suala la GBV linabaki kuwa juu Tanzania Bara na Zanzibar bila kujali Sera na Programu chanya za Serikali. Hata hivyo, Programu bunifu za Afua kutoka kanda ya Afrika na kwingineko zinaweza kuelezea mifano ya utendaji bora. Ushahidi kutoka muktadha nyingine zinaashiria kwamba mikakati ambayo inajumuisha vipengele vingi vilivyo chaguliwa kwa misingi ya muktadha wa maeneo na haja ya kushughulikia sababu za msingi za Ukatili, hupelekea katika Afua zenye mafanikio sana katika GBV na VAC. 1. Kuhamisha Wajibu wa Jinsia na Matarajio ya Kijamii ambayo hufanya VAW kuwa Jambo la Kawaida (Ethiopia) Baadhi ya vipengele muhimu vya Programu za kumaliza Ukatili dhidi ya wanawake vinajumuisha mbinu sikivu zinazoleta mageuzi kwenye jinsia. Mfano ufuatao: 116 Unatamka kwamba “Matumizi ya makusudi ya Sherehe za kahawa yalitoa fursa kwa wawezeshaji kujaribisha wajibu wa Kijinsia ambao sio wa kawaida, hukuza tabia za usawa na wakati huo huo kuongeza uhusika kijamii kwa Programu. Pia ilifanya kazi kama mahali pa kuingilia kwa ajili ya kujadili masuala mabalimbali yanayohusiana na desturi za Kijinsia, madaraka na Ujinsia.”110 Jiunge kwa Maisha Bora (UBL) Ethiopia Kusini Kuwafanya Wanaume Wapunguze Ukatili Dhidi ya Mwenza wa Karibu Wakati Wakinywa Kahawa Kwa kutumia shughuli ya kitamaduni ya wanawake, Sherehe za Kahawa, au UBL, hii ilikusanya wanawake na wanaume pamoja kwa ajili ya “majadiliano na shughuli zinazowahusu wote zilizolenga kwenye desturi za kijamii, ujinsia, mawasiliano na kusuluhisha migogoro, VVU/UKIMWI na IPV.” Cha kuzingatia zaidi, kila mshiriki alikuwa na fursa kutayarisha kahawa kwa Kikundi, na kitendo cha makusudi cha kugeuza desturi za Kijinsia111 kilidhaniwa labda kilichangia kuwepo kwa matokeo chanya ambayo tunayatoa kwa muhtasari kama ifuatavyo: Kwa uthabiti kupunguza Ukatili ulioripotiwa wa mwenza wa karibu (IPV) miongoni mwa wanufaika ambao sio wa moja kwa moja (wanajamii wa jamii kuu kwenye vijiji vilivyolengwa na Afua) zinapotolewa kwa wanaume. Kuhamisha desturi za kijnsia na tabia za hatari za VVU miongoni mwa wanufaika ambao sio wa moja kwa moja zinapotolewa kwa wanaume, wanawake, na wenza. Kwa ujumla, juhudi kwa wanufaika ambao sio wa moja kwa moja zinalingana na athari kwa wanufaika wa moja kwa moja ikiashiria kwamba ujumbe wa Afua umepenya kikamilifu kupitia jamii kuu. Afua za kufanya mageuzi ya jinsia yalifanyika katika mazingira ya vijijini pakiwa na elimu ngazi ya chini na vielekezi vya kijamii na kiuchumi pia vikiwa chini: Asilimia 75 ya wanawake na asilimia 50 ya wanaume hawajasoma; na Ujumbe uliotolewa kwa Wanaume umepenyezwa hadi kwa wasioshiriki.112 110 Ibid. https://gh.bmj.com/content/bmjgh/6/1/e004075.full.pdf 111 Ibid. https://gh.bmj.com/content/bmjgh/6/1/e004075.full.pdf 112 Leight J, Deyessa N, Verani F, et al. (28th January 2021) Afua katika ngazi ya Jamii za Kuzuia Ukatiki dhidi ya Mwenza wa Karibu, Maambukizi ya VVU katika nchi ya Ethiopia Vijijini. BMJ Global Health. https://gh.bmj.com/content/ bmjgh/6/1/ e004075.full.pdf 58 Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia 2. Kutumia Mbinu za Mawasiliano: Kwa ajili ya Kuendeleza Mabadiliko Chanya ya Kumaliza VAW – Katika nchi za Tanzania, Uganda, na Kenya Zana za Mawasiliano hutekeleza wajibu muhimu katika kuelimisha, kuhabarisha na kusaidia hatua za kumaliza GBV. Mifano mitatu ya utendaji mzuri unashirikishwa hapa chini ikisistiza ufanyaji kazi mzuri wa zana za mawasiliano ambazo hutambua jinsia na uanuai wa jumuiya. Tafiti za Afya ya Umma zinaashiria kwamba elimu, burudani, zimefanikiwa pale ambapo kampeni za habari zimeshindwa.113 Mifano miwili hapo chini—Kampeni za Elimu na Burudani za jamii nchini Uganda za kupambana na GBV na Kampeni ya Kenya ya Vioja ‘Tahidi’ kwenye TV ni – mifano thabiti ya mabaliko ya desturi za kimila kumaliza GBV na VAC kupitia matumizi ya vyombo vya habari vya kibiashara. Wasichana Balehe wa Shule Wamewezeshwa na Luninga nchini Kenya114 ‘Tahidi’, ni Tamthilia maarufu katika Luninga nchini Kenya iliyobuniwa mwaka 2007, kwa sasa inaonyeshwa katika muda ambao watu wengi huangalia TV na ilianza mwaka 2020. Katika mojawapo ya vituko vya hivi karibuni, mwanaume anamshawishi mwalimu mkuu wa shule ya wasichana kumruhusu msichana kijana ambaye amejifungua hivi karibuni kurudi shule kwenye masomo yake. Mwanaume huyu anamweleza mwalimu mkuu kwamba mustakabali wa mtoto mchanga wa Kenya unategemea elimu ya mama yake, na kwamba baba wa kichanga hicho ameruhusiwa kurudi shule..115 Masuala kadhaa kama hayo pia yamejadiliwa ambayo ni pamoja na Baba wa mtoto na Rafiki zake wa kiume, akidanganya kuhusu hadhi ya msichana na kuharibu sifa yake, masengenyo ya shule. Suala hili linatatuliwa kwa kumruhusu msichana arudi shule akiungwa mkono na mwalimu mkuu na rafiki zake wa karibu. Simulizi kama hizo, hata kama zimezalishwa kibiashara au kwa ufadhiri wa Wabia, zinaweza kuwafurahisha umati wa vijana na kuonyesha kuenea kwa changamoto hizo katika kila jamii, na ambazo watu wanakabiliana nazo wenye umri tofauti tofauti, na mabadiliko chanya yanaweza kuletwa kupitia utetezi wao wenyewe. 3. Kufikilia Upya Usalama: Mwitikio wa Kisekta Dhidi ya GBV/VAW (Israel) Wanawake na Watoto hudhurika mara mbili, mara ya kwanza kwenye mikono ya Mkatili na mara Pili anapolazimishwa kuondoka kwenye nyumba zao na kuanza maisha yasiyotabirika katika nyumba salama. Mbinu ya Israel pale Beit-Noam ni kutoa utulivu kwa mke na watoto badala ya kumuondoa Mkatili, lakini sio kupelekwa jela. Mkatili anaendelea na ajira yake na anaishi katika nyumba, Mke na Watoto waliofanyiwa ukatili wamezuiwa wasirudi nyumbani mpaka itakapo onekana ni salama kwa familia. 113 A. Banerjee, A. Ferrara, E. and Orozco, V. (2017); Burudani, Elimu, na Mitazamo kwenye Ukatili wa Majumbani https:// www.aeaweb.org/articles?id=10.1257/pandp.20191073. Green, D.P. Wilke, A. and Cooper, J. (January 31, 2019). Kupambana dhidi ya Ukatili wa Wanawake kwa kiwango kikubwa: Majaribio ya vyombo vya Habari katika Uganda Vijijini. https://www.poverty-action. org/sites/default/files/publications/GreenWilkeCooper2019.pdf, p.28. 114 Muundo wa Mwanafunzui wa Shule ya Skondari katika Maigizo ya Kileo katika TV ya Kenya: Kisa Mkasa cha Shule ya Tahidi, uk. 24. Wesonga O. Robert June 2011, Wesonga, Kenyatta University doc link 115 Watafiti wanatafiti Tamthiria na Simulizi ndogo kwenye Redio, wanakubaliana kwamba simulizi hizi za kileo zinashawishi maoni, na kupelekea watazamaji kufanya tafakali za maisha yao na kujitayalisha kwa mabadiliko ya Kijamii. Tamthiria zenye mhemko mkubwa kama vile Tahidi Hai hutegemea mvuto wa kimapenzi na sifa nyingine za uwasilishaji wa simulizi endelevu kutoa burudani inayoelemisha. (Robin Okuthe (Septemba 8, 2010) Agencies Take Soap Operas into Life Messaging Microsoft Word - Agencies Take Soap Operas into Life Messaging) (sfcg.org). 59 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania Mabweni ya Wanaume Wanaopiga Wake zao: Mbinu Mpya nchini Israel Mnamo mwaka 1997, Chama cha Beit Noam kilianzisha Kituo cha Matibabu cha Beit Noam, hili ni Bweni la wanaume wanaopiga wake zao ambao wanakabiliwa na mashitaka ya Jinai kutokana na Ukatili wa majumbani, na wale waliopewa rufaa kwa ajili ya matibabu. Rufaa kwenda Beit Noam mara nyingi hutolewa na Maafisa wa Majaribio na watumishi wa Ustawi wa Jamii. Mabweni ya Beit Noam yamebuniwa kutoa kwa wakazi wake Muundo wa Matibabu na Elimu. Wakati wanaume wanaopiga wake zao wanaendelea na matibabu ya kina kwa miezi minne pale Beit Noam, wake zao, wenza na Watoto wanabaki kwenye nyumba zao na hawalazimishwi kutafuta malazi nje ya jamii zao. Bweni linachukua wakazi 13 katika muda wote ule, na kila mmoja akikaa kwa kipindi cha miezi minne, akishiriki katika mchakato wa tiba ambao umeundwa kubadilisha tabia zao mbaya na kuwa wapole. Wakazi wa Beit Noam ni wale “sugu” wa tabia za ukatili nchini Israel, wakiwakilisha makundi ya rika tofauti kuanzia miaka 18 hadi 70. Wanaakisi mchanganyiko wa jamii ya Israel na wanawakilisha nyanja za Elimu na Uchumi na kujumuisha Dini na Makabila yote: Wayahudi, Warabu, Orthodox, na Wasio na Dini. Mfumo wa Tiba wa Beit Noam hutegemea: Kujenga Muundo ambao Unafanana na Mazingira ya Nyumbani. Kazi ya tiba hueneza uzoefu katika kuendesha na kushiriki katika kaya yenye usawa haki na Majukumu. Kaya hiyo huendeshwa kwa mashirikiano ya wakazi, ikiwataka kushiriana kazi, kuishi kwa usalama pamoja, na wakazi wengine, na kufanya juhudi za pamoja kutatua migogoro bila ya kutumia vurugu. Kutumia mchanganyiko wa mbinu za ukali na utambuzi. Watoa tiba huiona tabia ya ukatili kama ni matokeo ya vizuizi vya hisia na kuwaelekeza wakazi kupitia michakato yenye ngazi nyingi ambazo huwapelekea kuwajibika kwa vitendo vyao vya kikatili, na kuelewa matokeo yake, na kujenga mawasiliano mbadala, hii ni kuwa na uthabiti na uaminifu.116 4. Kuwezesha Mazingira ya Kisheria na Sera kwa Kutumia Teknolojia za Habari (DRC- Congo) Teknolojia Mpya za kidijitali zinatoa zana mpya za kuzuia na kuitikia VAW na GBV. Teknolojia hizo zimeboresha upatikanji wa habari na huduma kwa wanawake. Kwa mfano, Madaktari wa Haki za Binadamu walizindua MediCapt, Programu tumizi ambayo madaktari nchini Kenya na DRC Congo hutumia. Watoa huduma za Afya wanaweza kutumia MediCapt kukusanya Ushahidi wa kimatibabu, kupiga picha majeraha ya Wahanga, na kwa usalama kutuma data hizo kwa Polisi, Wanasheria, na Majaji wanaohusika katika mashtaka ya Uhalifu huo wa Ukatili wa Kingono. 117 Mfano mwingine wa jinsi upatikanaji wa msaada wa Kisheria unavyo wawezesha watu binafsi na jamii kukuza ulinzi wa haki za binadamu inaonyeshwa katika mfano hapa chini: 116 Chanzo: https://evaw-global-database.unwomen.org/en/countries/asia/israel/1997/beit-noam-residential- treatmentcenter-for-perpetrators-of-domestic-violence 117 Waganga kwa Haki za Binadamu (phr.org) 60 Upeo, Programu, Mapungufu na Mahali pa Kuanzia Mfumo wa Kidijitali wa Kuweka Kumbukumbu za Mashauri ili Kuwezesha Kubadilishana Habari katika DRC-Congo Katika DRC, mashariki, Mashauri mengi yaliyoripotiwa ya SGBV, hadi muda wanapofika Polisi katika eneo la tukio, Ushahidi mwingi unakuwa umeshapotea au kuharibiwa. Aidha, Mashauri amabyo yanachunguzwa mara chache hushirikisha ofisi ya Mwendaesha Mashitaka mjini Goma kutokana na uratibu usiotosheleza. Changamoto hizi hupelekea mashtaka kufanyika mara chache na kujenga mila ya kutokujali ambapo wakatili wanaaminishwa kukubali kwamba hawatawajibika. Kushughulikia Matatizo ya Mawasiliano na Ushirikiano ambayo yanazuia uchunguzi na kuendesha mashtaka ya Mashauri ya SGBV katika DRC Mashariki, Afua ya Utawala wa Sheria (Rule of Law Initiative of the American Bar Association) walifanya ubia na ofisi ya Mwendesha Mashtaka na kikosi maalumu cha Polisi, kilichopewa jukumu kwa wanawake na Watoto kutekeleza mfumo bunifu wa kidijitali. Mfumo huo wa kidijitali ulikuza ushirikiano baina ya Polisi na waendesha Mashtaka, kutoa msaada wa usafiri na kuwezesha maafisa wanaochunguza kuwasiliana na waendesha mashtaka kutoka eneo la Jinai katika muda halisi kupitia App. Kuanzia Oktoba 2013, Mfumo wa kidijitali umewezesha kazi baina ya Waendesha mashtaka huko Kivu Kaskazini (Masisi, Walikale na Kasaï Oriental) na Afisa wa Polisi, na kusababisha Mashauri zaidi kusikilizwa Mahakamani. Kazi hii ni sehemu ya Afua kubwa ambayo inatafuta kupanua uwezo wa ndani kuboresha upatikanaji wa haki kwa Wahanga wa SGBV Mashariki ya DRC, hii ni pamoja na kampeni za Elimu ya Sheria, Kongano za Msaada wa Kisaikolojia na Tiba, na Kliniki za msaada wa Kisheria.118 5. Kuwezesha Kuongeza Rasilimari kwa Usawa wa Kijinsia na Haki za Wanawake na Watoto (TimorLeste) Baadhi ya nchi zimejaribu kutoa gharama ya Kitini cha Huduma Muhimu za kuzuia na kuitikia Ukatili dhidi ya wanawake, ambayo ilitupa uelewa wa ukubwa wa uwekezaji unaotakiwa. Mifano ifuatayo kutoka Timor-Leste inaeleza mbinu ya kutathmini gharama za juhudi jumuishi za kuzuia GBV ikiwa ni sehemu ndogo ya GDP ya jumla. Kuhesabu Gharama: Timor-Leste119 Lao PDR na Timor-Leste zote zilipitia Ukatili ulioenea. Viwango vya kuenea katika Timor-Leste viko juu zaidi ya wastani Duniani, kwani takribani asilimia 59 ya wanawake waliripoti kwamba wamepitia Ukatili wa Kimwili na/au Ukatili wa Kingono uliofanywa na mwenza wa karibu au asiye wa karibu tangu walipokuwa na umri wa miaka 15, na zaidi kidogo ya asilimia 46 walishuhudia Ukatili katika kipindi cha miezi 12 iliyopita (UNFPA, 2017, p.2). Huko Lao PDR, Utafiti wa Taifa wa Mwaka 2015 wa wanawake 3,000 uliripoti kwamba takribani theluthi ya wanawake wamepitia Ukatili wa Kimwili, Kingono, na Kisaikolojia uliotekelezwa na mwenza (Duvvury et al., 2016, p.6). hata hivyo, gharama za Afua ziko chini kwa wastani. katika Lao PDR, gharama za kuanzisha na kuendesha Kitini cha huduma hizo katika kipindi cha miaka mitatu inakadriwa kwa Dola Milioni 13.5, au asilimia 0.25 ya GDP; Katika Timor-Leste, Kitini cha Huduma kinaweza kugharimu takribani Dola Milioni 6 katika kipindi cha miaka mitatu au asilimia 0.31 ya GDP. Katika hii ya Pili, hii ni chini ya asilimia 0.5 ya Bajeti ya Taifa kwa kuzingatia matumizi ya huduma za sasa na kiasi kwa asilimia 1.9 ya Bajeti za Wizara zilizounganishwa na zilizopewa jukumu la kutoa huduma hizi. (Duvvury et al., 2016, p.13). 118 Chanzo: Programu ya Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDP) na Ofisi ya Umoja wa Mataifa kuhus Madawa ya Kulevya, na Uhalifu (UNODC) Ripoti ya Utafiti wa Dunia kuhusu Msaada wa Kisheria, uk. 162. Umoja wa Mataifa, Oktoba 2016 https://www.unodc.org/documents/justice-andprison-reform/LegalAid/Global_Study_on_Legal_Aid_-_FINAL.pdf 119 Zainab Ibrahim, Jayanthi KuruUtumpala, na Jay Goulden (nd). Kuzingatia Gharama: Bei Ambayo Jamii Hulipa kwa Vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake. Sekretariati ya CARE International, Geneva Uswisi. https://www.care-international.org/ files/files/ Counting_the_costofViolence.pdf. 61 Tathmini ya Ukatili wa Kinjinsia Tanzania 62