Ripoti ya Mashauriano ya Wadau kuhusu Tathmini ya Jinsia na Ukatili wa Kijinsia Tanzania Bara na Zanzibar Kiambatisho kwa Ripoti Kuu Kiambatisho kwa Ripoti Kuu Ripoti ya Mashauriano ya Wadau kuhusu Tathmini ya Jinsia na Ukatili wa Kijinsia -Tanzania Bara na Zanzibar Kiambatisho kwa Ripoti Kuu Report No: AUS0002736 © 2017 Benki ya Dunia Anuani: 1818 H Street NW, Washington DC 20433 Simu: 202-473-1000; Barua – pepe: www.worldbank.org Baadhi ya Haki Zimehifadhiwa Kazi hii ni zao la wafanyakazi wa Benki ya Dunia. Matokeo, tafsiri, na hitimisho yanayoelezwa kwenye kazi hii si lazima yaakisi maoni ya Wakurugenzi Watendaji wa Benki ya Dunia au Serikali wanazowakilisha. Benki ya Dunia haitoi dhamana ya usahihi wa data zilizojumuishwa kwenye kazi hii. Mipaka, rangi, kiwango cha fedha, na taarifa nyingine zinazoonyeshwa kwenye ramani yoyote kwenye kazi hii haimaanishi maamuzi yoyote kwa upande wa Benki ya Dunia kuhusu hadhi ya kisheria ya nchi yoyote au kuidhinisha, au kukubali mipaka hjyo Haki na Ruhusa Maudhui kwenye kazi hii hutegemea Haki miliki. Kwa sababu Benki ya Dunia huhimiza utawanyaji wa maarifa yake, kazi hii inaweza kudurusiwa, ikiwa kamili au sehemu yake, kwa ajili ya madhumuni yasiyo ya kibiashara, ilimradi sifa kamili zinatolewa kwa kazi hii. Sifa —Tafadhali taja kazi hii kama ifuatavyo: “Benki ya Dunia. Machi 2022. Tathmini ya Jinsia Tanzania © Benki ya Dunia.” Maombi ya leseni, pamoja na haki tanzu yatumwe kwa Machapisho ya Benki ya Dunia,Taasisi za Benki ya Dunia 1818 H Street NW, Washington, DC 20433, USA; Nukushi: 202-522-2625; Barua pepe: pubrights@worldbank.org Machi 2022 3 Ripoti ya Mashauriano ya Wadau kuhusu Tathmini ya Jinsia na Ukatili wa Kinjinsia -Tanzania Bara na Zanzibar Muhtasari Rasmi Benki ya Dunia (WB) imefanya tathimini ya Jinsia na Ukatili wa Kijinsia nchini Tanzania ikiwa na malengo ya kusisitiza vichocheo vya mapungufu ya Kijinsia nchini Tanzania na fursa za maendeleo ya baadaye. Tathmini ilifuata muundo wa Mkakati wa Jinsia wa Taasisi za Benki ya Dunia (WBG) (Kwa Mwaka 2016-2023) ambao umejikita kwenye malengo ya kimkakati ka- tika: (1) karama za binadamu (elimu, afya); (2) fursa za kiuchumi (pamoja na kazi na umiliki/ udhibiti wa mali); na (3) kukuza sauti na harakati za wanawake na kuwashirikisha wanaume na wavulana. Tathmini ya Jinsia na Ukatili wa Kijinsia (GBV) inapatikana kwenye mtandao. Ripoti hii hutoa kwa muhtasari matokeo kutoka kwenye Mashauriano ya Wadau kwa Tanzania Bara na Zanzibar. Kuchagiza tathmini pana ya Jinsia na GBV, mashauriano kadhaa yalifanyika na Wadau wa Maendeleo (DPs), Asasi za Kiraia (Azaki), Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali (NGOs), na Wizara, Idara za Serikali, na Mawakala (MDAs) kati ya Agosti na Septemba 2021. Matokeo ya mashau- riano ya wadau yameandikwa kwa muhtasari ndani ya Ripoti hii. Wadau waliohojiwa walikuwa walionyesha upendeleo kwa Tanzania Bara, na mashauriano zaidi ni ya lazima kwa maana ya kujenga juu ya matokeo ya ripoti hii na kuhakikisha kwamba ni wakilishi. Mapendekezo yamepangwa katika maeneo makuu matano ya mada: 1) fedha, 2) kuongeza utendaji mzuri, 3) data na maboresho ya sheria, 4) ugatuzi na uratibu, na 5) uchambuzi wa desturi za kijamii. Mashauriano ya wadau yaliundwa kwa kutumia dodoso pana lililobuniwa kuchukua mitazamo kuhusu malengo ya kimkakati yaliyoainishwa katika Mkakati wa Kijinsia wa WB na utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (NPA-VAWC). Wadau walitambua mapungufu katika nyanja za mfumo, kuainisha masuluhisho yanayoweze- kana kwa ajili ya kushughulikia vikwazo ambavyo wanawake na wasichana wanakabiriana na- vyo, wakati pia wakisisitiza umuhimu wa kuwashirikisha wanaume na wavulana katika masu- luhisho hayo. Masuluhisho yalionyesha kwamba kwa sasa kuna upungufu wa urari na haja ya kuimarisha uratibu, kuboresha ufanisi na uendelevu wa fedha na kupambana na desturi. 4 Kiambatisho kwa Ripoti Kuu Utangulizi Benki ya Dunia (WB) imeendesha tathmini ya Jinsia na GBV nchini Tanzania kwa malengo ya kusisitiza vichocheo vya mapungufu ya Kijinsia nchini Tanzania na fursa za maendeleo zaidi. Lengo la tathmini hii ilikuwa ni kuainisha fursa zenye matumaini zaidi kwa ajili ya kuendeleza uwezeshaji wa wanawake na usawa wa Kijinsia nchini Tanzania kwa kuleta pamoja ushahidi wa hivi karibuni kuhusu: 1) mapungufu ya Kijinsia kwenye karama za binadamu, fursa za kiuchumi, umiliki na udhibiti wa mali, na sauti na harakati za wanawake; 2) vichocheo vya msingi vya ma- pungufu hayo ya Kijinsia; na 3) udhabiti wa sera imara na afua za Programu ambazo zinashughu- likia vichocheo vya msingi na/au vinginevyo vimeonyesha kufuta mapungufu ya Kijinsia. Tath- mini ilifuata muundo wa Mkakati wa Kijinsia wa WBG (Kwa Mwaka 2016-23) ambao unalenga katika malengo ya kimkakati kwenye: (1) karama za binadamu (elimu, afya); (2) fursa za kiuchumi (pamoja na kazi na umiliki/udhibiti wa mali); na (3) kukuza sauti na harakati za wanawake na kushirikisha wanaume na wavulana (angalia kielelezo 2). Mkakati umeasisiwa kwenye muundo wa dhana, uliotolewa mwaka 2012 na Ripoti ya Dunia ya Maendeleo kuhusu Usawa wa Kijinsia na Maendeleo ambayo ilipendekeza kwamba kaya, masoko, na taasisi (rasmi na zisizo rasmi, zote kwa pamoja), na miingiliano mingine yote ina ush- awishi kwenye usawa wa kijinsia na maendeleo ya kiuchumi.12 Tathmini ilipangilia vyanzo vitatu vya data- mapitio ya dawati, uchambuzi wa wingi, na mashau- riano ya wadau, kwa Tanzania Bara na Zanzibar. Mbinu kwa kazi hii ilijumuisha mapitio ya dawati ya fasihi (pamoja na ripoti za Serikali na zisizo za Kiserikali pamoja na fasihi za akademia (wasomi) kama vile tathmini ya athari ya afua husika), takwimu za ufafanuzi kuhusu mapungufu ya kijin- sia pamoja na kutoka kwenye vyanzo vikuu kama vile Utafiti wa Kitaifa wa Kaya na Viashiria vya Maendeleo ya Dunia, na uchambuzi wa mchanganuo wa wingi ili kutambua visababishi vikuu vya msingi nyuma ya baadhi ya matokeo makuu. Pale inapowezekana, ukichukulia kuna tofauti kubwa katika mapungufu nchini, data kuhusu ma- pungufu ya kijinsia yamewakilishwa yakiwa yametenganishwa kwa Tanzania Bara na Zanzibar, pakiwa na utenganisho zaidi kwa mikoa mmoja mmoja na vijiji/miji. Hatimaye, mashauriano ya wadau yaliendeshwa pamoja na DPs3, CSOs4, NGOs5, Wizara, Idara na Wakala za Serikali MDAs6. Matokeo ya mashauriano ya wadau yameandikwa kwa muhtasari ndani ya ripoti hii kwa ku- tumia muundo wa Mkakati wa Kijinsia wa WBG (Kwa Mwaka 2016-23). Ripoti hii ina sehemu saba: (1) muhtasari rasmi, (2) utangulizi, (3) mbinu, (4) karama za binadamu, (5) fursa za kiuchu- mi, (6) kukuza sauti na harakati za wanawake na kuwashirikisha wanaume na wavulana, na (7) hitimisho. Mbinu Wadau walichaguliwa kimkakati kuwa ndio watoa taarifa wakuu kutokana na uwepo wao na nafasi zao katika kufanya kazi kwenye masuala ya jinsia na GBV. Madhumuni ya mashauriano ya wadau yalikuwa ni kupata maoni na mitazamo kutoka kwa watendaji wakuu wanaofanya kazi katika uwanda wa usawa wa kijinsia, maendeleo na GBV. Aidha, mashauriano yalilenga katika kuchagiza mapitio ya fasihi kuhusu utekelezaji wa NPA-VAWC katika Tanzania Bara na Zanzibar. Mashauriano yanatoa uelewa wa kina kuhusu hadhi ya utekelezaji wa afua pamoja na maeneo ya kiutendaji na matokeo, pia kutoa utambuzi kuhusu utendaji, mafanikio, changamoyo, na mambo ya kujifunza. Kiambatisho Jedwali 3 kinaonyesha wadau waliochaguliwa kimkakati na 13 walioshiriki kwenye mashauriano. 1 Benki ya Dunia, 2011. Ripoti ya Maendeleo ya Dunia 2012: Usawa wa Kijinsia na Maendeleo. 2 The main assessment is available online (see World Bank Tanzania). 3 DP; Wadau wa Maendeleo. 4 CSO: Asasi za Kiraia 5 NGO: Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali 6 MDA: Ministries, Departmants and Agencies. 5 Ripoti ya Mashauriano ya Wadau kuhusu Tathmini ya Jinsia na Ukatili wa Kinjinsia -Tanzania Bara na Zanzibar Matokeo Mhimu Muktadha na Mazingira Wezeshi Mfumo wa Kisheria na Sera, kinadharia, una vipengele vingi vya Usawa wa Kijinsia; hata hivyo, mapungufu bado yapo na kuna changamoto ya kutafsiri ahadi. Kulikuwepo na makubaliano ya jumla kwenye mashauriano ya wadau kwamba mazingira ya kisheria na Sera ya Tanzania Bara na Zanzibar yalikuwa “wezeshi”. Aidha, japokuwa mapungufu yaliaanishwa kwenye mifumo ya Kisheria ambayo yanazuia usawa wa Kijnsia. Aidha, kulikuwa na ugumu katika kuhakikisha mifumo ya Kisheria inatafsiriwa kuja kwenye mipango madhubuti na baje- ti. Jedwali 1 linaonyesha muhtasali wa Sera wezeshi zilizojadiliwa na wadau, na mapungufu. Zaidi, ilitambulika kwamba wanawake wachache na wasichana wana uwezo wa kupata hudu- ma hizo za Kisheria, na hata wale wachache wanao pata huduma hizo hufika Mahakamani kupata haki zao Jedwali 1: Mfumo wa Sera na Sheria nchini Tanzania (Bara na Zanzibar) Mfumo wa Kisheria Mapungufu Sera ya Jinsia na Hii haijahuishwa wala Kufanyiwa Mapitio. Maendeleo (2002) Mashauliano ya Sheria za Kitamaduni na Kimila mara nyingi zinakinzana na Tanzania Haki za Kikatiba za Wanawake. Sheria ya Mtoto (2009) Sheria ya Mtoto inatumika na Wadau wanatambua umuhimu wa kujadili masuala ya Jinsia na Mtoto kwa ukaribu. Pia ili- tambulika kwamba Sheria ya Mtoto imetawala Mkataba wa Haki za Mtoto (CRC). Hata hivyo, Wadau walitambua ukinza- no wa vifungu kwenye Sheria hii na Sheria ya Ndoa. Sheria ya Mtoto inatamka kwamba Mtoto hufafanuliwa kisheria ni yule ambaye ana umri hadi miaka 18. Sheria ya Ndoa (1971) Sheria ya Ndoa (ikiwa kinyume cha Sheria ya Mtoto), inata- mka kwamba Mtoto Mvulana anaweza akaoa kuanzia mia- ka 18, lakini umri kwa Mtoto Msichana ni miaka 15 (Kifungu 13, kinatamka kwamba hii inaruhusiwa kukiwa na ridhaa ya wazazi/mzazi). Hili sasa limetatuliwa kufuatia shauri kubwa la Rufaa 204 ya 2017, Mwanasheria Mkuu dhidi ya Rebeca Gyumi. Aidha, Wadau walitamka haja ya kuwa na Bodi ya Upatanishi wa Ndoa. Sheria ya Ardhi (1999) Sheria zilizopo huwapa wanawake haki sawa za kupata na na Sera ya Ardhi (1995) kudhibiti rasilimali, ikiwa pamoja na Ardhi. Hata hivyo, mara nyingi Desturi za Kitamaduni hutawala katika masuala ya mirathi na umiliki wa Ardhi. Katika matukio ambayo Desturi za Kitamaduni hukinzana na Haki za Kikatiba za Wanawake, basi vifungu vya Katiba hutumika. Utekelezaji wa jambo hili linahitaji kuimarishwa. 6 Kiambatisho kwa Ripoti Kuu Afya Ilitambulika kwamba Tanzania ina Sheria na Sera nyingi zin- azohusu Afya ya Wanawake, upatikanaji sawa, na kuainisha ubora wa huduma. Hata hivyo, kuna Sera na mifumo mi- chache inayohusiana na kusaidia kufanya maamuzi salama kuhusu utoaji mimba na afya ya uzazi. Mdau (TAWLA) alitam- ka umuhimu wa kuidhinisha Mswada wa Uzazi Salama. Elimu Ilitambulika kwamba Tanzania ina Sheria na Sera nyingi zin- azohusu upatikanaji wa elimu kwa Wasichana na kumaliza na kumaliza kwa elimu bora. Hii inajumuisha kupiga marufuku ndoa za utotoni, Kifungu 60 cha Sheria ya elimu 2016. Hata hivyo, mapungufu muhimu yalikuwa kukosekana kwa Sera inayohusu kurudi shuleni kwa wasichana waliocha shule ku- tokana na kupata mimba7. Mpango Kazi wa Taifa Kupigwa marufuku GBV hupatikana kwenye Kanuni za Mako- wa Kutokomeza Ukatili sa ya Jinai (Imehuishwa 2002) kuhusiana na makosa ya kin- Dhidi ya Wanawake na gono ikijumuisha Ukeketaji (FGM). Sheria ya Ndoa pia inapi- Watoto ga marufuku kupiga mwenza (IPV). Hata hivyo, bado hakuna (NPA-VAWC) vifungu mahususi kumlinda mwenza kutokana na kubakwa ndani ya ndoa na ukatili majumbani. Wadau walitambua hili kama haja ya kupanua ulinzi dhidi ya GBV ili kukuza na kuim- arisha vitendo katika NPA-VAWC. Hii pia imetamkwa kwenye NPA-VAWC, lakini haijawa kamili. Makosa ya Kingono Licha ya kuongezeka makosa ya kingono, kunabaki kuwa na Sheria ya Vifungu changamoto kwa vile ripoti hutolewa katika kituo cha Poli- Maalumu si, ambako wengi hawajisikii salama na desturi za kijamii (SOSPA) na Ulinzi na kitamaduni bado zipo. Ukuaji wa Madawati ya Jinsia na kutoka Ukatili wa Watoto kwenye vituo vya Polisi, ni juhudi za wanawake na Kingono (Manyanyaso wasichana kupata haki sawa. Polisi wanaopokea mashauri ya Kingono) wanaweza wasiwe na mtazamo sawa na wanawake ambao wanatafuta hupata haki zao. Sheria hii inasaidia na kutam- Vimetamkwa kwenye bua unyanyasaji wa kingono kama kitendo cha jinai. Hata Sheria ya Kuzuia na hivyo, kupanua ulinzi dhidi ya ukatili wa kingono unahitajika Kupambana na Rushwa pia kutambulika kwa Sheria ya Ubakaji na Sheria ya kulinda 2007 ndoa kuhusiana na GBV. Mahakama Maalumu Kwa kutambua unyeti wa kesi za ukatili wa kingono, Zanzibar ya Familia (Zanzibar) imeteuwa Majaji kuunda Mahakama maalumu ya Familia ambayo pia huharakisha ukamilishaji wa kesi ili kupata usu- luhishi wa haraka. Fomu ya Polisi Namba Bado kuna changamoto kupata fomu za PF3 ambazo lazima 3 (PF3) zikamilishwe katika kituo cha Polisi ili kuthibitisha kwamba kweli shambulio lilitokea, na hii huwa sehemu muhimu sana ya ushahidi ili kuweza kumtia mtu hatiani. Pamekuwepo na harakati ili huduma za PF3 ziweze kutolewa katika vituo vya afya au katika vituo vinavyotoa huduma nyingi sehemu moja, ili kurahisisha utoaji wa taarifa na kukuza miitikio ya wahanga. 7 On November 24, 2021, the Government of Tanzania announced re-entry guidelines for children who drop out of school for different reasons, including girls dropping due to pregnancy. 7 Ripoti ya Mashauriano ya Wadau kuhusu Tathmini ya Jinsia na Ukatili wa Kinjinsia -Tanzania Bara na Zanzibar Ukeketaji (FGM) Maendeleo chanya kuelekea kukomesha FGM yametambu- liwa; hata hivyo, kuna tofauti kati ya Mikoa ambako desituri za kimila bado zinatumika, na hivyo desturi hizi zinaendelea. Hii inahitaji jitihada kubwa kuongeza ufahamu na kuchukua hatua za kutoa ulinzi wa kisheria. Wadau walitambua “Viwezeshi” kadhaa vya kushughulikia Mapungufu ya Sera na Sheria nchini Tanzania. Viwezeshi vikuu vinne viliaanishwa ambavyo vinaweza kuondoa mapungufu hayo: 1. Utashi wa Kisiasa: Wadau walitambua kwamba Wanasheria, Wabunge, na Viongozi wakuu kwenye Serikali wanahitaji kuwa na utashi wa kuwa msitari wa mbele na kuunga mkono utekelezaji wa mifumo ya Sheria ambayo inashughulikia kukosekena kwa usawa. Ilitambulika kwamba kunahitajika pawepo ushirikishaji bora wa Wabunge kuhusu haki za wanawake na wasichana, lakini pia utashi wa kisiasa kwa maana ya ufadhili wa muda mrefu. . 2. Kubadili Desturi za Kimila, Kijamii na Kidini: Ilitambulika kwamba baadhi ya taasisi zinazotekeleza Sheria zimefungwa ndani ya desturi za kimila na mitazamo ambayo hubeba hisia na mitazamo hasi kwa wanawake na wasichana. Kwa mfano, ukatili wa majumbani mara nyingi huchukuliwa na Polisi kama jambo la faragha linalopaswa kumalizwa nje ya Mahakama. Wakati kubadili desturi za kijamii hutambulika kama kitu kinachotokea kwa taratibu na kwa muda mrefu, huhimizwa vizuri zaidi linapoongozwa na viongozi wa kitamaduni katika jamii, viongozi wa dini na wazee wa Kijiji. Viongozi hao kama walinzi wa mila na tamaduni wapo katika nafasi ya kimkakati ya kushughulikia desturi hizi mbaya za kimila zilizotamalaki, na mitazamo iliyojikita katika mfumo dume kuhusiana na wajibu na majukumu ya wanawake na wanaume katika familia na katika jamii. 3. Harakati za Kijamii: Mara nyingi pamekuwepo na swali ni kipi kinaanza –Kati ya Mabadiriko ya Kisheria au Ufahamu ambao unapelekea kwenye mabadiriko ya Kisheria? Wadau wanatambua kwamba kuna rasilimali finyu za kusaidia utetezi na uhamasihaji wa jamii kwenye haki za wanawake na wasichana. Ilitambulika kwamba kuna haja ya kuwa na msaada zaidi katika kuhisisha na kujenga ufahamu; aidha, kupata wanawake wa kuigwa (role models) ni muhimu. Kuna uwezekano wa kuimarisha harakati za kijamii katika kutokomeza GBV kupitia Kamati 18,186 za sasa za Ulinzi wa Wanawake na Watoto (Kamati za MTAKUWWA) ambazo zinaweza kuongezeka na kusambaa nchi nzima. 4. Kuondoa Mapungufu ya Kisheria: Kiwezeshi cha mwisho kitahakikisha kwamba mapungufu ya Kisheria yanaondolewa ili kuhakikisha ubaguzi wa Kijinsia na kukosekana kwa usawa haviendelei kushamiri. Hususani, Sheria ya Ndoa inakubaliana umri wa chini wa ndoa vinaendana na hukumu ya Mahakama Kuu; amri ya azimio la Kimila inafanyiwa mapitio kuhusu Sheria ya Mirathi ya Wanawake, na Sheria za Watoto pia zinafanyiwa mapitio ili kuainisha ukatili dhidi ya Watoto kama kosa la jinai, pia kuwezesha utendaji wake kuwa wa ufanisi pamoja na kuimarisha mifumo mbadala ya haki.8 Ufadhili wa Muda Mfupi umekuwa nl desturi na umekuwa si endelevu katika kubadilisha mfumo dume. Usawa wa Kijinsia na mabadiliko ya mfumo dume yanahitaji uwekezaji wa muda mrefu. Hata hivyo, Wadau wamegudua ukweli kwamba pamekuwepo na ufadhili finyu wa muda mrefu, ambao kwa kawaida hufanywa na Serikali na Wadau wa Maendeleo nchini Tanza- nia kwa ajenda hii. Mfano, iliibuliwa kuhusu NPA-VAWC, ambao, licha ya gharama zake kufaha- mika, ni sehemu ndogo tu ya mahitaji ya ufadhili ambayo yamekidhiwa (Angalia kiambatisho, Kielelezo 3 kuhusu matumizi ndani ya maeneo mbalimbali ya kiutendaji ya NPA-VAWC). 8 Mifumo mbadala ya haki inarejea kwenye michakato ya usuruhishi wa migogoro nje ya mfuomo wa Mahakama, Pamoja na mifumo ya kijamiii ya kitamaduni, na mifumo isiyorasmi iliyojikita kwenye jamii. 8 Kiambatisho kwa Ripoti Kuu Licha ya uwekezaji wa kuanzisha Vituo vya Kutoa Huduma Zote Mahali Pamoja, (One Stop Cen- tres), pia ilitambulika kwamba pamekuwepo na uwekezaji mdogo katika kuhakisha maeneo salama kwa wanawake na hifadhi wanapoathirika na ukatili, na kuongeza simulizi za mafanikio. (Angalia TAWLA, Kisanduku 1). Hatimaye, Wadau walitambua kwamba ufadhili wa muda mre- fu unapaswa kuelekezwa kwa: (1) Uimarishaji wa Mifumo na Michakato, (2) Kujenga uwezo katika Wizara, Idara na Wakala za Serikali (MDA), na (3) AZAKI, Viongozi wa Dini na Viongozi wa Kitamaduni, wakifanya kazi kwa Karibu na jamii kuleta Uwajibikaji na Uwezeshaji (UNFPA, Kisanduku 1). Visababishi vyote hivi vilitambuliwa kama taratibu za kuhakikisha ufadhili katika usawa wa Kijinsia unaleta mabadiliko makubwa zaidi. Kisanduku 1: Fikra za kuhakikisha Ufadhiri kwa Usawa wa Kijinsia Unak- wenda Mbali zaidi Ufadhili wa Vituo vya Kutoa Huduma Zote Mahali Pamoja: “Tunao Wahanga wengi wa GBV, lakini hatuna mahali pa kuwaweka. Kuna maeneo machache sana ya kuwahifadhi nchini… [tunahitaji] kuanzisha vituo ambavyo vitamilikiwa na Serikali. … Vinaweza kufanya kazi kwa ubia na AZAKi. Hii itasaidia sana wanawake. … Tunapata wateja wengi sana katika kliniki zetu za msaada wa Kisheria lakini mwisho wake hurudi. Pia, kuna vituo vichache sana vya kutoa huduma zote mahali pamoja na (viko mbali) – TAWLA, Agosti 2021 Ufadhili wa Kuimarisha Mfumo katika Kipindi cha Muda mrefu: “uwezo wa kuongeza mafanikio au utendaji mzuri na mambo tuliyojifunza ya vitendo hivi … ni mambo ambayo bado hatujayaona. … Hii inahusiana sana na Ufadhili. … Kama ukiangalia Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano, mikakati mbali mbali ya Sekta ya Afya, Mpango mmoja [n.k.] vimejikita zaidi kwenye maboresho yanayotegemea vituo, Ni hospitali zaidi, hutumia mbinu ya kuimarisha mfumo wa Afya ambao ndio unaotakiwa, lakini pia kutambua visababishi ambavyo vinazuia wanawake na wasichana kutokufurahia haki zao za kingono na uzazi nchini Tanzania, haya yamejikita katika desturi hasi za kijamii na vitendo vinavyoumiza ni vitu ambavyo vinahitaji kushughulikiwa katika ngazi ya jamii na nje ya vituo... Kwa bahati mbaya, hatuoni kwamba kupata usikivu mkubwa na Ufadhili. [hiki ndicho ambacho tutatoa] matokeo makubwa. … Inahitajika Uwekezaji kwa kipindi kirefu cha muda.” – UNFPA, Agosti 2021 Ufadhili wa Muda Mrefu na Kuelekea Desturi za Kijamii: “Desturi za kijamii ni sehemu ya jamii, wazazi, n.k. Lakini pia watalaamu. Wakati mwingine tunachofanya tunawafundisha Polisi, Madawati ya Jinsia na Watoto … hushughulika na masuala haya nyeti (GBV na ukatili wa Watoto), lakini wakati huo huo … Wanaume na wanawake wamelelewa katika jamii ambazo sio muhimu kuzifanyia desturi hizi na maadili kuwa ya Kimataifa linapokuja suala la ukatili na ukatili wa Kingono … wanaweza kufanya hivyo katika kazi zao… lakini wakiwa nyumbani [desturi hizo hubaki]… unapaswa kuzifanya desturi na maadili hayo kuwa ya Kimataifa kwa watu ambao watafanyia kazi hili… huu ni mchakato wa muda mrefu.” – UNICEF, Agosti 2021 Kufadhili Huduma za Kinga: “… [tunahitaji] juhudi za kufanya uzuiaji … katika nchi nyingi kuna kutokuwepo kwa usawa katika mwitikio… [lakini kama tunavyojua] kinga ni bora zaidi kuliko tiba.” – UNICEF, Agosti 2021 9 Ripoti ya Mashauriano ya Wadau kuhusu Tathmini ya Jinsia na Ukatili wa Kinjinsia -Tanzania Bara na Zanzibar Maboresho ya Data yametoa Picha sahihi zaidi kuhusu hali ya Usawa wa Kijinsia nchini Tan- zania; hata hivyo, sio Data zote zimetenganishwa, na matumizi ya Data kwenya Sera ni Kido- go. Wadau wametambua kwamba pamekuwepo na uimarishaji katika mifumo ya Data husu- sani katika sekta fulani kama vile Elimu (kupitia Mfumo wa Kusimamia Habari za Elimu (BEMIS) kupitia OR-TAMISEMI). Kupitia BEMIS, viashiria vya elimu hutenganishwa kwa kutumia Jinsia. Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bara tayari inao msisitizo wa jinsia na juhudi zimefanyika kuten- ganisha data. Kwa Zanzibar, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali (OCGS) imeanzisha Kitengo cha Kamati ya Usimamizi wa Takwimu za Jinsia, ili kusimamia ukusanyaji, uchambuzi, na matumizi ya Tak- wimu za Jinsia. Kamati inawajibika kurasmisha viashiria vya jinsia katika Tafiti za Kitafa na Sensa ili kuhakikisha ufuatiliaji mzuri. Aidha, kwa sasa data za ‘matumizi-kwa wakati’ hukusanywa na zinaweza kunakili mzigo wa wanawake katika matumizi yasiyo sawa ya muda. Hata hivyo, kuna matumizi madogo ya data, na kuna haja kubwa ya kujenga uwezo wa kiuchambuzi wa Jinsia wa watendaji wakuu kuweza kuchambua data na kutumia matokeo ambayo yatatoa maamuzi sahihi ya Sera na Utendaji. (Angalia Uongozi, Kisanduku 2). Hatimaye, UNICEF ilieleza jinsi mapungufu yalivyokosekana kwenye data za desturi za kijamii (UNICEF, Kisanduku 2). Hata hivyo, kwa sasa wanafanya kazi na Serikali kupata hili suala na kuwezesha ufuatiliaji wa muda mrefu ili kuonyesha jinsi Programu zao zimebadili maarifa, mi- tazamo, na utendaji katika muda mrefu (Jukwaa la data katika ngazi ya Mkoa). Kisanduku Box 2: Maoni ya Wadau Kuhusu Mapungufu ya Data a) Ujuzi wa Kiuchambuzi kuongeza Thamani kwenye Data iliyopo: “Kuainisha zana sahihi za ukusanyaji na upimaji wa data ni muhimu, lakini pia ujuzi unahitajika. Kuna mapun- gufu ya Uchambuzi. Asilimia themanini ya data zilizokusanywa zinahitaji kuchambuli- wa…na data ambazo hazijatumika.” – Uongozi, Agosti 2021 b) Data Mpya kuhusu Desturi na Utendaji: “kuna data chache sana kuhusu desturi za Ki- jamii zenye Madhara na maandishi ya jinsi ya Kuzibadilisha,” – UNICEF, Agosti 2021 “In- aaminika kwa hali hasi sana, kwamba unapopata mtoto msichana ‘nusu yake’ ’ unataki- wa uendelee hadi upate mtoto mvulana… hivyo watakwambia kwamba lazima “urudie tena” kupata mtoto (mtoto mvulana). Hivyo, msichana anapolelewa, analelewa kama mtoto wa daraja la pili [mwananchi], na wavulana hupewa kipaumbele. Katika mila za Wasukuma kuna msemo unaosema kwamba mtoto mvulana kamwe sio mtoto mdo- go. […] hivyo, kutokana na muktadha huo, ni kikwazo kikubwa sana kwa msichana.” – LHRC, Agosti 2021 (Kuna data ndogo kuhusu vitendo mbalimbali vya mfumo dume kote Tanzania.) c) Kuboresha Mbinu za Ukusanyaji wa Data: Ni muhimu kutumia “utafiti unaozingatia ushirikishwaji na kujifunza kutoka ngazi za chini. … Hii inatuonyesha ni wapi Sera ina- fanya kazi au haifanyi kazi.” – TGNP , Agosti 2021 Mbinu hii ilitumiwa na TGNP ngazi za chini zaidi. Jinsia ilitambuliwa kwamba ni suala mtambuka; hivyo, kupambana na masuala ya Jinsia kwa kujitenga hakutaweza kwa ukamilifu kufikia lengo. Wadau walitambua juhudi za Serikali ya Tanzania ya kuboresha uratibu katika kupambana na masuala haya, kwa mfano: (1) ijapokuwa NPA-VAWC imetokana na Wizara ya Afya MoHCDGEC9 imetaka pawepo na uratibu kwenye MDAs, CSOs na DPs; (2) kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGA) na Kamati za MTAKUW- 9 Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto. 10 Kiambatisho kwa Ripoti Kuu WA, kuna juhudi za kuimarisha uratibu katika ngazi ya mkoa; na (3) MDAs na LGAs nyingi zina watu au vitengo waliojikita katika masuala ya Jinsia. Aidha, Wadau wa Serikali waliotoa ush- auri walieleza jinsi wanavyofanya kazi na Wizara nyingine kuhakikisha kwamba suala la Jinsia linashughulikiwa katika hali ya ujumla (kwa maana ya MoEST na MoHCDGEC, Tanzania Bara). MoHCDGEC, Zanzibar, ilieleza jinsi Kikundikazi kilicho na Wakurugenzi wa Mipango na maaf- isa wa Serikali kjljchanzishwa visiwani Zanzibar kuratibu, kurasimisha, na kutoa msaada wa kiufundi katika masuala ya Jinsia kwenye Wizara zote. Hata hivyo, uratibu unakutana na chan- gamoto katika mazingira ambapo rasilimali ni chache, rasilimali fedha na watu kwa pamoja. Uhaba wa fedha, na utegemezi kwa Wadau wa Maendeleo ulitambuliwa na Wizara. Inaweza kuwa wazo jema kwa Tanzania kujifunza kutoka Nchi nyingine ambazo zimeweza kwa ukamilifu kusimamia uratibu katika ngazi zote na wadau katika mazingira ambayo yana rasilimali chache. Karama za Binadamu: Elimu Uzoefu na fursa za Jinsia zinatofautiana katika sekta ndogo; hata hivyo, kwa ujumla kuna jitihada za kuelekea maboresho ya usawa wa kijinsia, hususani katika elimu ya msingi. Sekta ya elimu ilitambulika kwamba imepata mafanikio makubwa katika kuelekea usawa wa kijinsia katika elimu ya msingi na elimu rasmi. Sekta ya elimu ilitambulika kuwa ina sera na mikakati mingi katika kuvunja taratibu za kibaguzi ambazo zinazuia upatikanaji na ubora wa elimu, k.m., Mkakati wa Taifa wa Elimu Jumuishi (NSIE), Ulinzi wa Mtoto, Muongozo wa kuongoza na kutoa ushauri, na Sera ya Elimu ya Msingi bila Malipo (FBEP) (angalia MoEST10,kisanduku 3). Uboreshaji wa ziada ulitambulika kwamba unahitajika kwa ajili ya kuboresha mazingira ya ku- jifunzia ili kuhakikisha wasichana wanapata vituo vya ugavi stahiki wa maji, usafi wa mazingira na usafi wa mwili (WASH) na taulo za kike. Aidha, mbinu ya jumla ni muhimu katika kuhakiki- sha wasichana na wavulana wanasaidiwa katika kipindi chote cha elimu yao, na jinsi zote zina fursa sawa za kupita na kukamilisha ngazi zote zinazotakiwa za elimu. Wadau walirejea katika mfumo wa usimamizi wa ufanisi wa mashauri katika Mkoa wa Kigoma (angalia kisanduku 3) ambapo mbinu zilizoratibiwa zilitumika kuamsha ufahamu wa ukatili na kujibu. Mifumo ya kuthamini Jinsia inaendelea kuwepo katika sekta ya elimu na kuna haja ya ku- fanya mageuzi ili kubadili desturi. Wadau hata hivyo walizingatia kwamba kuna fursa kwa sekta kufanya mageuzi zaidi kwa kuanza mapema kuvunja desturi na kuishirikisha jamii kuu kuhamasisha mabadiliko. Kuna haja ya kufanya zaidi kwa wenye umri mdogo kuvunja desturi za kijinsia. Kuwekeza kwenye elimu mapema kunatoa fursa ya kuvunja majukumu ya kimila. Ilizingatiwa kwamba juhudi zaidi zilihitajika katika kuvunja desturi za kijinsia ndani ya mfumo usio rasmi wa elimu, ambao waliutambuwa kuwa unaendeleza na kujumuisha mifumo ya ki- jamii katika wilaya kwa wanaume na wanawake zaidi ya mfumo rasmi. Mafunzo ya mwalimu kuhusu jinsi ya kushughulikia masuala yanayohusiana na Jinsia ilitambulika kuwa ni utatuzi wa jambo hili. Aidha, wadau walizungumza kuhusu umuhimu wa kuwa na Muongozo wa kisheria kuhusu wasichana walioacha shule kwa ajili ya mimba na kuweza kurudi kwenye shule rasmi. Vyuo vikuu vilitambulika kuwa na changamoto kadhaa, hivyo kuwa na mifumo inayowajibika kwa malalamiko ni muhimu. Wadau kutoka vyuo vikuu walitambua kwamba wanawake walio- jiunga kwenye vyuo vikuu wanakabiliwa na changamoto ya kuandikishwa, lakini mara wanapo andikishwa, wanakabiliwa na mapambano ya ziada wanapoingia mazingira yaliyotawaliwa na wanaume kwa sehemu kubwa. Kuandikishwa kwa wanawake katika elimu ya juu bado kuko chini sana na hivyo kuna haja ya kuhakikisha kwamba mfumo unawajibika kwa malalamiko 10 Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia 11 Ripoti ya Mashauriano ya Wadau kuhusu Tathmini ya Jinsia na Ukatili wa Kinjinsia -Tanzania Bara na Zanzibar yanayo wakabili wanawake walioandikishwa katika elimu ya juu. Mdau kutoka chuo kikuu cha Dodoma alieleza jinsi mifumo ya malalamiko inahitaji kuwajibika na kuwawezesha wanafunzi kupaza sauti. Wadau walikubali kwamba utamaduni wa ‘kupaza sauti’ bado unahitaji kufanyiwa kazi kwani ni wachache wataibua malalamiko kama hayo, lakini ni muhimu kujenga uelewa kwamba ni jambo la kawaida na kuhakikisha kwamba wote wanawezeshwa kupaza sauti na kujua kwamba hatua zitachukuliwa. Mfumo wa malalamiko unahitaji kuwajibika na kuwa unaoitikia, ili ‘nafa- si’ ifanywe kuwa jumuishi. Hata hivyo, uundwaji wa kufanya nafasi hii iwe jumuishi hii bado unaendelea, kwani kwa kawaida nafasi hii ni ya dume, hivyo ujumuishi ‘unaruhusu’ wanawake kuingia kwenye nafasi. Kunahitaji kufikiria kidogo kuhusu ni jinsi gani mfumo unaowajibika na jumuishi utafanana? kuliko kutohoa nafasi hii kwa kuwaalika wanawake ili wakubaliwe. Nafasi hii bado inatawaliwa na mfumo dume. Kuna haja kwa sekta ya elimu kuhakikisha ujumuishi umeenea katika sehemu zote, na mahi- taji ya watoto wenye ulemavu yanakidhiwa. Ilitambulika kwamba ijapokuwa NSIE imefungua milango kwa watu wanaoishi mazingira magumu kujiunga kwenye ngazi mbalimbali za elimu, mahitaji anuwai ya watoto wenye ulemavu yalikuwa hayakidhiwi vya kutosha au kushughu- likiwa. Kuhakikisha ujumuishi unaenea sehemu zote, lilikuwa ni mojawapo ya mapendekezo kutoka kwa wadau. Kisanduku 3: Mafanikio ya Elimu na Mfano wa Uongozi na Ushauri mkoani Kigoma a) Mafanikio makuu kwenye sekta ya elimu “(1) Kielekezi cha Usawa wa Kijinsia cha 1:1 kimepatikana katika ngazi za chini za elimu (awali, msingi na sekondari ngazi ya chini); (2) upatikanaji/fursa za kupata elimu ni kwa wote wa jinsi zote; (3) Data za elimu zimeten- ganishwa kwa jinsia.; (4) Maendeleo na kutoa Mkakati wa Ujenzi wa Shule na Ukarabati (2019-2028), ambao hutoa viwango vya miundombinu ya kinjisia ambayo huitikia kwa jinsia, na (5) Kutoa Uongozi, Ushauri na Mwongozo wa Kulinda Mtoto kwa Shule na Vyuo vya Walimu (2020), ambao unalenga katika kuimarisha Vitengo vya Ushauri Shuleni, kushughulikia changamoto za kisaikolojia za wanafunzi (pamoja na GBV). –Habari ya maandishi iliy- otolewa na MoEST (Tanzania Bara), Septemba 2021 b) Kuanzisha mfumo wa kusimamia mashauri katika sekta zote ni muhimu: “Kuungan- ishwa kwa wanawake na watoto hakufanyi kazi kila mahali. … Mahali pekee ambapo [wadau wote muhimu wanafanya kazi kushughulikia masuala ya ukatili dhidi ya wana- wake na watoto kwa pamoja] ni Kigoma… na ndipo ambapo [sisi] pia tunaona mambo ya kufurahisha yanajitokeza. Kwa mfano, kutambua kwamba tayari kulikuwepo na mfumo wa kusimamia mashauri ya ukiukwaji ulinzi wa watoto unaongozwa na ustawi wa jamii, lakini haukuwepo kwa wanawake.… Hili bado halijatatuliwa. … Ni vizuri kwamba limetambulika [kutokana na ukweli] [sisi taasisi za UN] tulifanya kazi pamoja. … Mkoani Kigoma, tunaona matukio mengi yanar- ipotiwa kuhusu ukatili, lakini hatuwezi kujua iwapo viwango vinapungua, lakini ukweli kwamba mfumo unafanya kazi, matukio yanaripotiwa na kushughulikiwa, kuna ufahamu zaidi, uvumilivu mdogo, na kuna mwitikio ambao umeratibiwa zaidi. Ni mwanzo mzuri.” – UNICEF, Agosti 2021 12 Kiambatisho kwa Ripoti Kuu Karama za Binadamu: Afya Tanzania inaendelea kutumia mbinu ya utabibu katika utoaji wa huduma za afya. Wadau walijadili matokeo ya afya ya wanawake, kwa maana ya afya ya mama, afya ya waliobalehe, upatikanaji wa huduma, ubora wa huduma na zaidi – na kuibua wasiwasi kuhusu rasilimali za muda mrefu zilizo finyu lakini pia mbinu iliyojikita zaidi kwenye uganga, au utabibu ambayo bado inatumika nchini.. Ilitolewa hoja kwamba mbinu ya uganga haijali ukweli kwamba kukosekana kwa usawa kwenye upatikanaji wa huduma– desturi za kibaguzi za maisha yote zinazozuia upatikanaji na ubora wa huduma. Visababishi hivi vinahitajika kuwa sehemu kuu ya muundo wa afua za kuboresha afya za wanawake na wasichana. Pale yanapogunduliwa, maendeleo katika matokeo ya afya ya mama, kwa sehemu kubwa yametokana na ushirikishwaji wa mafanikio wa wanaume. Kwa maana ya afya ya mama, maendeleo yaliainishwa kwenye sehemu za Tanzania, lakini matokeo yalikuwa madogo. Moja ya sababu zilizotajwa kwamba zinachochea mabadiliko kidogo ilikuwa kwamba afua zinatumia mbinu ya ‘uganga’/’utabibu’ na kushindwa kuona afya ya mama kama inayoamuliwa kijamii, lakini pia ni matokeo ya michakato ya kibaguzi ambayo inasababisha kukosekana kwa usawa katika afya ya mama. Sababu ya pili ya kuwepo kwa mabadiliko kidogo ni uwekezaji mdogo (wa ndani na wa nje) katika kuboresha matokeo ya afya ya mama. Hata hivyo, mabadiliko chanya yanayoonekana kwenye sehemu chache za Tanzania, kunatokana na ushirikishwaji wenye mafanikio wa wa- naume. Kwa mfano, kwa upande wa Shinyanga (Bara) na Zanzibar, kama ilivyojadiliwa na UN- FPA, wanaume walishirikishwa kwa mafanikio. Hata hivyo, kulikuwa na changamoto ya jinsi ya kuongeza mafanikio haya (UNFPA: kisanduku 4). Kisanduku 4: Maoni ya Wadau kuhusu Mbinu ya Mifumo ya Afya Kuwashirikisha wanaume ili kupunguza viwango vya vifo vya Wakinamama: “Tumeona kwamba masuala yanayohusiana na vifo vya akina mama hayajaendelea kama tulivyofikiria. […] Hata hivyo, tunaanza kuona utumiaji mkubwa wa ANC12 na utoaji zaidi wa huduma kwa kutumia vituo vya afya, tunaanza kuona mabadiliko ya taratibu kwenye jamii kuhusiana na desturi na maadili hasi ya kijamii ambayo yanawazuia wanawake kutafuta huduma wakati wa ujauzito na kujifungua. […] Kwa bahati mbaya, hiki sio kitu kinachojitokeza katika viwango vya vifo vya akinamama. Kwa mfano. Tunaanza kuona viongozi wengi zaidi wa dini wakija kuunga mkono ajenda ya uzazi wa mpango, kwa mfano, visiwani Zanzibar na Bara. Tunaona viongozi wengi wa mamlaka za Serikali wakiunga mkono ajenda hii kwenye maeneo ya Programu ambako tunafanya kazi … [na] viongozi wa jamii wakiunga mkono dhana hii ya Haki na Afya ya Kingono na Uzazi na kutambua haja ya kuboresha upatikanaji kwa wanawake na wasichana kwa maamuzi haya. Lakini changamoto bado ipo kwenye maeneo machache tunayoyaona […] lakini hayajakuwa makubwa [au] hadi kufikia ngazi ya kutaasisiwa.” – UNFPA, Agosti 2021 Wasichana balehe wanaendelea kuwa katika hatari kutokana na desturi na nguvu zizizo kuwa na usawa. Wasichana balehe waliainishwa kuwa katika hatari mahususi, ikiwa ni mimba za utotoni, ndoa za utotoni, ukeketaji kwa baadhi ya maeneo ikiwa juu. Kwa sehemu kub- 13 Ripoti ya Mashauriano ya Wadau kuhusu Tathmini ya Jinsia na Ukatili wa Kinjinsia -Tanzania Bara na Zanzibar wa imetamkwa kwamba mimba za utotoni na kasi ndogo ambayo zinapunguzwa ni dalili za: (1) mgawanyo usio sawa wa uwezo na rasilimali, na (2) desturi za kimila ambazo zinaendele kuwalazimisha wasichana wadogo kwenye desturi hizi. Aidha, upatikanaji kwa wasichana wa habari zinazohusu haki zao za uzazi na afya zilikuwa finyu. Ili kuvunja kukosekana kwa usawa kwenye afya, mapendekezo ya wadau yanaweza kuwekwa kwenye makundi yafuatayo: (1) kuwawezesha wasichana kujua haki zao na kuweza kufanya maamuzi yao wenyewe, (2) kuimarisha ushirikishwaji wa wanaume na wavulana, kama vile kuwawezesha na kuinua ufahamu, na wavulana kuwaheshimu na kuwalinda wasichana, na kuwajumuisha wanaume katika majadiliano kuhusu nini wanaweza kufanya, (3) kukuza desturi chanya za kijamii na kuonyesha mfano wa watokeo, (4) kuimarisha uratibu wa sekta zote na ngazi zote (5) ahadi ya ufadhili wa muda mrefu, na (6) kuzalisha na kutumia data zilizotengan- ishwa Fursa za Kiuchumi: Upatikanaji wa Mali na Kazi Licha ya sheria zinazowezesha upatikanaji wa mali kama vile Ardhi, desturi za kitamaduni na mila zinaendelea kudhoofisha upatikanaji kwa wanawake. Ijapokuwa Sheria za Ardhi zipo zinazoruhusu upatikanaji sawa (na udhibiti) wa Ardhi na rasilinali nyingine, ni wanawake wa- chache wanaomiliki Ardhi. Aidha, ukubwa wa Ardhi inayomikiwa na wanawake ni mdogo ukil- inganisha na wanaume. Ilitambulika kwamba Sheria za kimila na kitamaduni zinaendelea ku- wabagua wanawake na wasichana, hususani kwa maana ya mirathi. Sheria hizi za kitamaduni zinaweza kukinzana na haki za kikatiba na kisheria. Wanawake wanahitaji upatikanaji bora wa miundo ya kisheria ili kuhakikisha haki zao zinapatikana (angalia kisanduku 5). Maeneo ya kazi yanayojali jinsia na upatikanaji sawa wa hafasi za uongozi yalitambulika kuwa ni muhimu katika kuhakikisha uwezeshaji wa wanawake mahali pa kazi. Wanawake walitambuliwa kuwa wana uwezekano zaidi wa kuajiriwa kwenye kazi zilizo na ujira mdogo. Mdau mmoja kutoka Chuo cha Uongozi alieleza jinsi ubaguzi wa kijinsia mahali pa kazi una- vyoweza kuwepo bila ya kugundulika, na itakuwa muhimu kuendesha mafunzo kuhusu uon- gozi wa kijinsia ili kuhakikisha wanawake wanajumuishwa kwa usawa. Mdau huyo aliainisha kwamba mabadiliko zaidi yanahitajika ili kuhakikisha wanawake wanaweza kupata nafasi za uongozi ambazo zinalipa vizuri. Ilijengwa hoja kwamba kuna haja ya: (1) hatua za makusudi za kuthibitisha wanawake kupata nafasi za uongozi; (2) mazungumzo yanayoendelea kusaidia kutoa maarifa na kuhoji hali isiyobadilika; (3) kutambua vinara ambao wanajenga mabadiliko ya mfumo; (4) kutetea uwepo wa mahali pa kazi panapojali jinsia; na (5) kuboresha ufahamu wa jinsia. Kisanduku 5: Umuhimu wa Kuboresha Upatikanaji wa Msaada wa Kishe- ria kama ilivyoshirikishwa na AZAKi Zinazosaidia Kutoa Msaada wa Bure wa Kisheria kwa Wanawake Kuboresha Upatikanaji wa Msaasa wa Kisheria: “[Asasi ilanzishwa kwa sababu kulikuwe- po na ukatili mwingi wa kijinsia dhidi ya wanawake, na wakati ule ha hata sasa, hawawezi kumudu gharama za huduma za Mahakama, mawakili na wengine. Kwa miaka mingi sasa, tumewasaidia [mamilioni ya11 ] wanawake kupata msaada wa kisheria na elimu.– TAWLA, Agosti 2021 11 Mdau asiyethibitishwa. Mdau aliripoti Mamilioni ya Wanawake walioweza kupata Huduma. 14 Kiambatisho kwa Ripoti Kuu Sauti na Harakati: Kuwashirikisha Wanaume na Wavulana Tanzania’s first female President remains a symbol of hope, however pockets of resistance Rais wa Kwanza Mwanamke anabaki kuwa ishara ya matumaini, hata hivyo maeneo ya up- inzani yapo. Wadau wote walizungumzia umuhimu wa ishara hii ya kuwa na Rais wa kwanza mwanamke, Mh. Rais Samia Suluhu Hassan. Uwepo wa Rais mwanamke uliainishwa kwamba unajenga mazingira wezeshi kwa kukuza viongozi wanawake na ushiriki wenye nguvu zaidi kwenye kufanya maamuzi. Aidha, baadhi ya vyama vya siasa vilitambulika kuwa ‘wazi’ zaidi kwenye kujumuisha wanawake, hususani wanawake walio kwenye nafasi za uongozi, na wameliweka hili kwenye ilani ya vyama vyao. Hata hivyo, ilitambulika kwamba bado kuna sa- fari ndefu kwani ushiriki wa wanawake bado ni mdogo na kuna upinzani kutoka kwa watendaji muhimu kuweza kuunga mkono kikamilifu ujumuishi wa wanawake. Kwa sehemu kubwa na- fasi ya uongozi bado imetawaliwa na wanaume, sio tu kwenye kazi, lakini pia katika kufanya maamuzi na siasa. Ushiriki wa wanawake kwenye siasa ni kidogo, ukiathiriwa na kujumuika kwao kwenye vya- ma vya siasa, lakini pia na uwezo wao unaotiliwa mashaka wa ‘kucheza mchezo wa kisia- sa’. Aidha, kwa fursa kwa wanawake kwenye siasa, ilitamkwa na baadhi ya wadau kwam- ba ‘mchezo wa kisiasa’ unawaweka wanawake katika nafasi ya kutofaidika. Rushwa ya ngono imeenea kwenye siasa, na pesa imebaki kuwa ni sarafu inayozungumza. Hivyo, ukweli kwamba wanawake wana mtaji mdogo wa pesa ukilinganisha na wanaume (na majukumu kama vile familia) hii ina maana kwamba hawawezi kuwekeza kwenye ‘mchezo wa siasa’ na hivyo ku- wakilisha sauti ya wanawake kwenye kufanya maamuzi. Ilitambuliwa kwamba wanawake wa viti maalum wanavyopewa Bungeni havina hadhi sawa kama viti vya kuchaguliwa. Inaweza kusemwa kwamba siasa nchini Tanzania imeendelea kuwa ni nafasi inayotawaliwa na wanau- me (angalia kisanduku 6). Kisanduku 6: Mchezo wa Kisiasa umeendelea kuwa wa Wanaume Kutengwa kwa Jinsia kwenye Siasa: “Hata kama una nguvu sana… na jamii ina kukubali… lakini kama huna pesa, Nimeona kwamba huwezi kupenya kiasi hicho… au kugombania… Hivyo, cha kufanya ni kuendelea kubadilisha mitazamo ya viongozi wetu, sio kuhusu pesa ni kuhusu [kuwa na] mtu mzuri kwa ajili ya jamii. … Ndio maana tunawaona wanawake wach- ache sana wanaoshiriki katika miundo hiyo.” – TAWLA Kubadilisha desturi za kijamii za nini mwanamke anaweza kufanya na kuwa ni muhimu sana. Programu za uwezeshaji zinazolenga kaya, jamii na mtu mmoja mmoja ziliainishwa kama utatuzi kwa kubadili mtizamo wa nini mwanamke anaweza kufanya (angalia kisanduku 7 na Kampeni ya Baba Bora Visiwani Zanzibar 12). Iliainishwa kwamba jamii, wanaume, wavulana na Taifa kwa ujumla wanahitaji kubadili fikra zao na mitazamo dhidi ya wanawake na wasichana. Kuna fursa kubwa ya mabadiliko baina ya vizazi kama Tanzania itasisitiza kuwatumia wanawake wa mfano (role model) ili kuhamasisha kizazi kijacho. 12 https://men-care.org/2015/09/30/in-tanzania-baba-bora-campaign-works-to-end-violence-against-women-and- children/ 15 Ripoti ya Mashauriano ya Wadau kuhusu Tathmini ya Jinsia na Ukatili wa Kinjinsia -Tanzania Bara na Zanzibar Kisanduku 7: Mifano Chanya ya Kuwashirikisha Wavulana na Wanaume Kuwashirikisha wanaume na wavulana katika kuzuia ukeketaji: “Nitakupa mfano wa Programu ya Ukeketaji Kaskazini mwa Tanzania (Mara, Mwanza na Arusha) … tulikuwa tun- awahusisha wakeketaji (ambao ni wanawake) lakini tulipofanya mapitio ya mradi… tuliona kwamba tumewaacha wanaume nyuma. Wanaume ndio ambao ni wakeketaji, sio kimwili, lakini kwa kuweka tarehe, kutoa rasilimali kwa ajili ya sherehe hizi za ukeketaji, na kila kitu. Wanaitwa ‘wazee wa mila’. … Ilikuwa na mafanikio sana, ukeketaji (kwenye mikoa hii) imepungua kwa kiasi kikubwa.” – LHRC, Agosti 2021 Kampeni ya NPA-VAWC ni Sera muhimu kuhusu sauti na harakati za wanawake nchini Tan- zania. Kuhusu majadiliano ya sauti na harakati za wanawake, tathimini ya kina ilifanywa ya NPA-VAWC. Iliangalia katika Sera kwa maana ya: (1) kubuni, (2) kuendana na miongozo ya kisheria, Sera na miongozo mingine ya kitaifa, (3) utekelezaji, (4) mambo tuliyojifunza, na (5) mapendekezo. Kampeni ya NPA-VAWC imekusanya mipango kazi minane iliyopita na kuwa mpango mmoja, kuwezesha uratibu bora na ufanisi katika matumizi ya rasilimali. Hii inaendana na Programu muhimu za Taifa, pia na Sera za kimataifa na Programu.13 Mafanikio mengi yamefanywa na NPA-VAWC hadi sasa, kwa kutegemea ahadi ya kuzingatia Programu na Sera za kitaifa na kimataifa (angalia kielelezo 1). Hata hivyo, kuna changamoto zinazotuzunguka: (1) fedha, (2) upatikanaji wa data, (3) kugatua kikamilifu mpango, na (4) desturi za kijamii zilizojikita. Wizara kiongozi (MoHCDGEC) haipati fedha za kutosha na hakuna bajeti ya Serikali mahususi kwa ajili ya utelezaji wa mpango, hususani kwenye LGA. Aidha, ili- hojiwa iwapo ‘malengo’ ya NPA-VAWC yalikuwa ya uhalisia tokea mwanzo. Kielelezo 1: Mafanikio na Changamoto za NPA-VAWC, kama zilivyoainish- wa na Wadau 13 For example, analysis of the GBV/VAWC was guided by different global tools from World Health Organization “INSPIRE” as well as strategies set out by the Global Partnership to End Violence Against Children. 16 Kiambatisho kwa Ripoti Kuu Mpango kazi wa sekta nyingi zilizokusanywa na kuwa mpango mmoja wa kushughulikia des- turi za kijamii zilizojikita ambazo zinachochea GBV/VAWC, unawakilisha fursa ya harakati nyingi zenye mafanikio ikiwa ni pamoja na rasilimali fedha; hata hivyo, inabaki kuwa ni ajen- da inayotoka juu kwenda chini badala ya kutoka chini kwenda juu. NPA-VAWC ilitambuliwa kuwa ni ya msingi katika kuwaleta pamoja na kutengeneza mpango jumuishi mmoja utakaoto- komeza GBV/VAWC, na kujenga mazingira ya VAWC ambapo watendaji wote watashikirishana Dira na Uwajibikaji kwa afua zilizopo kwenye maeneo ya utendaji. Kwa njia nyingi NPA-VAWC ni ishara inayoonyesha mwanzo mpya wa mpito wa kimila na kitaasisi wa kutokomeza GBV/VAWC. Hata hivyo, kulikuwa na haja inayotambulika ya kuimarisha afua na uwekezaji ambao utafuata msingi ya kutoka chini kwenda juu, ukiongozwa na ngazi ya kata, mtaa, na shehia. Hii ni muhimu kwa ajili ya kuimarisha majukumu ya kamati za ulinzi. Kwa vile Serikali kwa sasa inapanga kufanya tathimini ya NPA-VAWC, kuna haja ya kujifunza kutoka kwenye mafanikio na afua zilizoongozwa na mikoa tofauti kama vile Shinyanga na Kigoma. Kuiga baadhi ya mikoa yenye afua zilizofanikiwa ili iweze kurudiwa na itaweza kusaidia kujenga maarifa kwenye vipengele muhimu vya afua zitakazoweza kutokomeza VAWC. Aidha, mpito unahitajika kutoka muitikio wa utoaji huduma hadi kuzuia kwa kuvunja desturi za sasa kuanzia umri mdogo. Mapendekezo Mengi yamefanyika katika kuweka kwenye muktadha mwisho wa GBV na kusogea kuelekea usawa wa kijinsia. Lakini mapungufu bado yapo. Inatambulika kwamba sasa usawa wa kijinsia unawekwa kwenye muktadha zaidi ikiwa na istilahi kwa neno ‘mfumo dume’ (angalia TGNP, Agosti 2021) na mipango iliyopo ya kutokomeza GBV; hata hivyo, mipito zaidi ya kimila na des- turi inahitajika. Wengi wa wadau walitambua mapungufu kwenye usawa wa kijinsia na fursa kwenye nyanja mbalimbali, lakini pia waliainisha vikwazo muhimu kwa wasichana na wanawake kote Tanzania vinavyojumuisha: (1) mila na desturi za mfumo dume (kwenye ngazi na miundo mingi: kwa mfano, jamii, wazazi, shule na zaidi), 2) umasikini, na 3) kukosekana kwa mfumo wa kuzuia (na muitikio mdogo). Vikwazo hivyo vinaonyesha kwamba, nchini Tanzania, kadri wan- awake wengi wanavyoweza kupata mahitaji yao watakuwa wanatafakari aina ya mfumo am- bao wanawake wanaweza ‘kupata’ wanachohitaji. Wadau wengi wanatambua kwamba mfumo dume bado unatawala na hivyo mageuzi yanahitajika kwenye mfumo kama kuboreshwa kwa upatikanaji. Angalia Jedwali 2 kwa ajili ya mapendekezo yaliyowekwa kwenye muhtasari kutoka mashauria- no ya wadau. 17 Ripoti ya Mashauriano ya Wadau kuhusu Tathmini ya Jinsia na Ukatili wa Kinjinsia -Tanzania Bara na Zanzibar Jedwali 2: Mapendekezo kutoka Mashauriano ya Wadau Kubadilisha Jinsi Tuazvyowekeza kwenye Programu za Jinsia Programu nyingi Ahadi za Serikali na DPs kuwekeza kwenye Programu za muda mrefu, michakato na miradi ya kubadili mitazamo, miundo na za muda mrefu michakato inayoendeleza desturi za kibaguzi,. Kulenga kwenye Haja ya kuweka msisitizo zaidi kwenye “mchakato” pia na mchakato, “matokeo.” Aidha, kuna haja ya kuwa na mabadiliko kutoka matokeo na kwenye kulenga mwitikio/ athari kwenye kuzuia (angalia Kuzuia mapendekezo ya desturi chini). Mbinu ya jumla ambayo inahudumia wote (inazingatia tabaka za Kuboresha watu) ni muhimu. Kuongeza bajeti ya Serikali na kutenga kwa ajili ya Ajenda ya fursa na usawa wa kijinsia, na kuzuia GBV/VAWC. Mchakato wa kawaida wa uchambuzi wa kijinsia wa bajeti pia ulitambuliwa Kuongeza fedha kuwa ni zoezi muhimu kufanyika. na kujenga Kuboresha kujenga uwezo ndani ya MDAs kuhusu unyeti ns uwezo kukosekana kwa usawa; hii ni muhimu kwa wanataaluma na wafanya maamuzi. Kuimarisha mifumo ya uratibu na urasimishaji wa jinsia. Kushughulikia Vunja duara la umasikini kwa wanawake, hakikisha kwamba umasikini kwa wana mishahara iliyo sawa zaidi, thamani, na kipato cha kiuchumi wanawake na kinachofanana na wanaume. wasichana Kuongeza Utendaji Mzuri Afua nyingi za AZAKi, INGOs, na NGOs zinaonyesha ushahidi wa mafanikio na zinapaswa kuongeza kwa njia endelevu Uwezo wa kuongeza juhudi uzingatiwe. Kukuza ushiriki wa wanaume na kuonyesha mfano wa mabadiliko Kuongeza chanya. utendaji mzuri na ushahidi Kusisitiza na kuamsha ufahamu wa wanawake wa kupigiwa mfano kwenye nchi nzima na kuweka dhana ya ‘ujike’ kwenye muktadha wa Kitanzania na kutoa mifano chanya kwa wanawake. Utaratibu wa kufanya hivi haukujadiliwa lakini unaweza kujumuisha mpango mpana wa Serikali wa mawasiliano kuhusu wanawake wa mfano. 18 Kiambatisho kwa Ripoti Kuu Data and Legal Reforms Reforms are key – but they need to be participatory when made, involving MPs and citizens. Laws are not implemented due to lack of resources and capacity; therefore, it goes back to the recommendation for more long- Legal reforms term programs to be financed. (and their implementation) A special family court or fast-tracking on GBV cases is crucial for ensuring victims get the support they need as early as possible. A good example to follow up on is the recently designated judges in Zanzibar. See link for more information: https://dailynews. co.tz/news/2021-05-046091508a3a5f0.aspx Generate (and use) sex disaggregated data on a range of topics (human endowment, assets, economic opportunities, and voice/ agency), and support key actors with tools and frameworks for Data conducting gender analysis. This is a key tool for advocacy. To allow for frequent analysis), data on the above topics, but also in particular the social/cultural norms and practices, needs to be collected more regularly. Decentralization and Coordination (especially for the NPA-VAWC) Strengthened coordination and decentralization are key. This requires funding i.e., protection committees need funding for improvement. (Also advised to be separate from police station.) Interventions should be grounded in local decision-making (household level). Community engagement is key. MPs need to be involved, and the capacity of LGAs developed (especially ward level). This Strengthened links to findings on coordination. In general coordination was decentralization noted in this agenda, especially NPA-VAWC which was improved -- but government needs to take a stronger role (especially MoHCDGEC). The challenge was at the LGA level, especially where resources are constrained. A multi-sectoral (and decentralized) approach needs resources. It was explained how the protection committees are strong at the regional and district level, but weak at the ward and village level (over 8,000 villages has meant it is difficult to ensure accountability and a responsive system). Improved coordination at the MDA level requires financial and Coordination technical support. 19 Ripoti ya Mashauriano ya Wadau kuhusu Tathmini ya Jinsia na Ukatili wa Kinjinsia -Tanzania Bara na Zanzibar Deconstructing Negative Social Norms Patriarchy and male-dominated culture is a reality across Tanzania. This will take time to change; there remains to be negative perceptions of women in the community at large. Further work is required to ensure equality of rights and access Don’t forget and changing the patriarchal norms that are embedded in to work on the Tanzanian culture. norms Promote male involvement and show case positive changes. Conduct research with the perpetrators and recognize traditional beliefs and spirituality. Focus on Support programs targeting adolescent girls to empower them to stay in school, say no to early marriage, and say no to early adolescent girls pregnancy. Focus and invest in prevention of GBV (not only response) which requires two things: (1) start early, and (2) use education. Focus on We need to start with education and normalizing gender equality at the household/ family level. Women need to know their value prevention and be empowered from childhood. Need to start early. through education and The ward level and engagement with community is key awareness (awareness raising) but also addressing the root causes to raising prevent. Education is key for prevention – many recognized the role of education early to break gender norms and ideals. Positive examples that can be learnt, including from the HIV/ AIDS awareness raising campaigns. Normalize reporting of GBV There is greater awareness on GBV (and more people report) and recognize due to greater awareness. The two go hand-in-hand. GBV it as a crime Mapungufu ya Ushiriki wa Ziada Majadiliano ya Wadau yalitambua mafanikio mengi nchini Tanazania na fursa kwa maboresho ya ziada katika iwezeshaji wa kijinsia na kuzuia GBV. Mashauriano yanayoendelea yatapang- wa na Benki ya Dunia katika mchakato wa kubuni na kuanzisha Jukwaa la Jinsia na Ujumuishi. Aidha, utafiti wa ziada utafanyika katika maeneo yafuatayo: 1. Ulinzi wa Kingono kwa wanawake. Katika majadiliano, ni vitu vichache vilifanyiwa uchunguzi kwa maana ya ulinzi wa Kijamii. Kwa siku za baadae mkazo unaweza kuwa katika sababu za ushiriki mkubwa wa wanawake katika vikundi vya kusaidiana? 2. Mikopo Midogo, Pesa za Simu za kiganjani, na fursa za kiuchumi kwa wanawake. 3. Kuwaelewa Wakatili. 4. Kuelewa wajibu wa desturi za kijamii, na vizuri zaidi jinsi ya kuzibadilisha. 20 Kiambatisho kwa Ripoti Kuu Kiambatisho Kiambatisho Kielelezo 2 Mfumo wa Mkakati wa Jinsia wa WBG (kwa mwaka 2016-23) Kiambatisho Kielelezo 3 Uwiano wa Matumizi wa NPA-VAWC katika Maeneo Nane ya Kiutendaji Chanzo: NPA-VAWC, 2017-21 21 Ripoti ya Mashauriano ya Wadau kuhusu Tathmini ya Jinsia na Ukatili wa Kinjinsia -Tanzania Bara na Zanzibar Annex Table 3: Key Stakeholders Interviewed Wawakilishi wa Serikali 1. Wiazara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee na Watoto (Tanzania Bara) 2. Wiazara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee na Watoto, (Zanzibar) 3. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Wadau wa Maendeleo 4. Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake (UN Women) 5. Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) 6. Mfuko wa Kimataifa wa Shughuli za Watu (UNFPA) Benki ya Dunia na IFC (Sehemu ya timu kubwa) Sekta Binafsi IFC (Sehemu ya timu kubwa) Taasisi za Utafiti na Wasomi 7. Chuo Kikuu cha Dodoma 8. Taasisi ya Uongozi Asasi za Kiraia 9. Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) 10. Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika (WiLDAF) 11. Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) 12. Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) 13. JUWAUZA (Zanzibar) 22